Kigamboni: Polisi wadaiwa kuua raia

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Soma taarifa hii iliyosambazwa na kiongozi wa BAVICHA:



Katikati utekelezaji wa ahadi ya mkuu wa wilaya Kigamboni(Sarah Ally) iliyotolewa wiki hii tayari matunda yake tunaanza kuyaona.

Ikumbukwe juzi tuu ametoa ahadi ya kuwatia ulemavu watuhumiwa wote wataokamatwa kwa tuhuma za wizi(vibaka).

Juzi usiku Polisi walienda kutekeleza kazi zao Kata ya Mjimwema mtaa wa Kibugumo na walifanikiwa kumkamata kijana mmoja anayetambulika kwa jina la Ino na kuondoka naye wanakojua wao.

Leo hii asubuhi taarifa zisizo na Shaka zimenifikia kuwa kijana huyo amekufa akiwa mikononi mwa polisi. Jana mama yake alienda kumuangalia kituo Cha Polisi na kukuta kavunjwa miguu yote na Askari wakamwambia akamtafutie baiskeli ya kutembelea(wheel chair). Leo ameenda amekuta amekufa.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari, inasemekana marehemu baada ya kupigwa sana akawa analazimishwa awataje wezi wa Kibugumo na inasemekana akawa anataja watu hovyo mradi anusuru maisha yake. Hivyo basi kuna hatari nyingine kubwa itakuja ya mauaji kutokana na majina aliyoyataja marehemu.

Msiba upo kwao kibugumo na maiti huenda bado ipo Kigamboni hospital (Vijibweni).

Naomba watu wa haki za binaadamu muingilie Kati swala hili.

Stop killing innocent people

PRAY FOR INO

Mwenyekiti BAVICHA (W) Ilala

Michael Ernest kapama
michaelkapama89@gmail.com

=======

Gazeti la Mwananchi linaripoti habari za kifo cha kijana kilicho zua utata
_________
Hakuna kitu kinauma kama mzazi kumpoteza mtoto wake tena kupitia sehemu aliyokuwa akidhani ni salama.

Hali hiyo imemkuta Edna Clement, mama wa watoto wanne ambaye kwa sasa yupo katika kipindi kigumu cha kumpoteza mwanaye wa kwanza, Innocent Vitus kutokana na kile kinachodaiwa alishambuliwa na wananchi wenye hasira.

Edna na watoto wake wanaishi eneo la Kibugumo, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Ilikuwa Alhamisi saa 2:00 usiku nilisikia kijana wangu wa pili akaniita mama kaka kakamatwa na polisi, nilikimbia hadi kwenye lile gari na kuwauliza wanakompeleka mwanangu usiku wakaniambia mwanangu hayumo,” alisimulia Edna na kuongeza: “Nikamuuliza mdogo wake mbona simuoni akasema mama yupo huwezi kuona vioo ni vyeusi basi gari ikaondoka, kwa mbele kidogo ili igeuze nikasimama katikati ya barabara nikawaambia sitoki hadi mniambie mnakompeleka, wakasema kituo cha polisi.”
Alisema wakati ya gari linaondoka aliwasiliana na baadhi ya ndugu zake waliomsihi kutulia ili wafuatilie.

Hata hivyo, Edna alisema usiku huohuo aliamua kwenda kituo cha polisi na saa 4:00 usiku alishuhudia kijana wake akiingizwa mahabusu ya kituoni hapo.


Alisema alirudi nyumbani na Agosti 30 saa 4:00 asubuhi alimpelekea chai lakini alishangaa kusikia kuwa hawezi kutembea.

“Alipoitwa mmoja wa mahabusu aliniambia ‘mama huyu kaumia mguu hawezi kutembea’, hivyo akaingiza chai na kumpatia, niliomba RB nijue ni nani aliyemkamata na kosa lake,” alisema.


Alisema aliandikiwa jina la mpelelezi alipoingia ofisini kwake alimuuliza jina la mtuhumiwa, lakini alimwambia hana taarifa zake wala hajakabidhiwa jalada la kesi hiyo.

Alisema Agosti 31, alipeleka tena chai lakini kijana wake alipoitwa na askari wa zamu hakuiti, jambo hilo lilimfanya na yeye (Edna) kuanza kuita bila mafanikio huku mahabusu mmoja akijibu tena kuwa alitolewa tangu Alhamisi saa 10:00 jioni na hakurudishwa.
Alisema aliombe namba ya mpelelezi alipompigia alimweleza kuwa kesi ngumu hawezi kuisimamia kwa sababu haina jalada na kwamba, baada ya kufuatilia walimwambia walimtoa mahabusu akataka kukimbia.

Polisi watupiana mpira

Septemba 2, gazeti hili lilimtafuta kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kuthibitisha tukio hilo lakini alijibu: “Nipo likizo wasiliana na mtu niliyemuachia madaraka.”

Baada ya kuwasiliana na ofisi ya Mambosasa, walimwelekeza mwandishi kuwasiliana na kamanda wa polisi mkoa wa Temeke ambaye naye alidai hana taarifa hizo. “Naomba niwatafute eneo husika ambao ni Kigamboni niweze...uwe mvumilivu na kesho unipigie,” alisema Amon Kakwale ambaye ni kamanda wa polisi Temeke.

Septemba 3, simu yake ilipopigwa ilipokewa na msaidizi wake ambaye alidai kamanda yuko kikaoni huku akimtumia mwandishi namba ya simu ya mkuu wa kituo cha polisi Kigamboni kurahisisha upatikanaji taarifa. Hata hivyo, mkuu huyo wa kituo alisema: “Anayeweza kuzungumzia hayo ni RPC Temeke naomba umtafute kwa sababu ndiyo nasikia kutoka kwako, wasiliana naye ila mimi kwa kweli sijui.”


DC akataa kuzungumzia

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri alipopigiwa simu alisema msibani mkoani Mwanza. “Mambo ya kesi nendeni kwa OCD niko msibani Mwanza,” alisema Sarah.

Mazishi utata
Awali, Edna alikataa kuzika mwili wa kijana wake hadi atakapojua sababu za kifo na kukamatwa kwake. Hata hivyo, mjomba wa marehemu Jackson Vincent alisema wameamua kuzika kwa sababu waliambiwa kufanya hivyo na polisi waliowasindikiza kufanya uchunguzi.

“Tulikuwa na askari sita tulipoenda kufanya uchunguzi, tulipofika hata daktari mwenyewe hakupata nafasi ya kufanyia uchunguzi ule mwili bali askari ndiyo walitoa maelezo ya kuwa ni jambazi aliuawa akijaribu kukimbia mikononi mwa polisi, maneno hayo yalifanya tuanze kulumbana na wao kunipa kibali cha kuzika kwa lazima na kuambiwa fanyeni mazishi,” alisema.
 
Kama ni suala la vibaka na wezi, HAKUNA JINSI WAPOTEZWE TU NASEMA WAPOTEZWE TU
Watu tunashindwa kutembea kwa uhuru sababu ya wezi na vibaka,WATIWE ULEMAVU KABISA MAANA HAKUNA NAMNA.

Watu tunaibiwa na hawa mbwa,
HAKUNA NJIA NYINGINE WAVUNJWE VUNJWE KABISA NA WAPELEKA TAARIFA KWA WAZAZI WAO KUWA HAYO NDIO MATUNDA YA KILE WANACHOKITAFUTA KWA PANGA, VISU, BISIBISI NA BASTOLA WAKATI WENZAO WALIVITAFUTA KWA JASHO NA KUVUMILIA MATESO YA KAZI.

Hawa VIBAKA,ni sawa na VIRUSI katika jamii, wavunjweeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Na atakayewatetea vibaka kwa kusudio la kutetea haki za binadamu na yeye afanywe kama vibaka walivyofanywa
 
CHADEMA wanatetea ujinga wa hao vibaka,Mungu tunusuru na hiki chama cha kiharakati kinatuharibia nchi yetu
Kwa hiyo waue watu tu bila kupelekwa mahakamani?, na hao aliowataja nao wauawe tu bila kupelekwa mahakamani?, acha ushabiki wa kijinga
 
Baada ya kuona mwandishi wa hii taarifa ni mwanasiasa, nimejilaumu sana kupoteza muda wangu kusoma huu 'uharo'
 
Sasa kuua mtu kisa tuhuma za wizi tena polisi ndio wanaua? Hii si haki, labda kasingiziwa je?
 
Back
Top Bottom