Hakimu: Usipompa pesa mkeo akapendeza ni 'ukatili wa kiuchumi'

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Hiyo ni kauli ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Sanya Juu wilayani Siha, Janeth Mvungi, aliyoitoa katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kueleza kuwa upo ukatili wa kiuchumi kwa mwanamke ambao hauzungumzwi sana.

Akizungumza katika maadhimisho hayo leo Desemba 11, 2023 huko Sanya Juu, , Mvungi amesema kuna ukatili wa kijinsia ambao unasahaulika nao ni ukatili wa kiuchumi.

“Kuna ukatili ambao huwa unasahaulika sana nao ni ukatili wa kiuchumi na watu wanaongelea tu kipengele cha mwanamke kupewa nafasi ya kumiliki mali. Naomba niseme hata mke wako usipompa pesa unamkatili kiuchumi,”amesema.

“Sheria ya ndoa inasema mwanamume ana wajibu wa kumtunza mke wake na familia. Japo mwanamke naye anakuwa na huo wajibu kama amemzidi mwanamume kipato lakini mara nyingi familia zetu mwenye kipato ni baba,” amesema.

“Kwa mila na tamaduni zetu mwanamume ndiye anayesimamia familia. Mama Yeyooo (kinamama wa Kimasai) mnapewaga eeh? (sauti zikasika hapanaaaa). Wanasema hamtowi. Jamani tubadilike,”alisema Hakimu huyo na kuongeza:

“Kina baba kutowapa kina mama hela na matunzo ni ukatili wa kiuchumi naomba tubadilike mhakikishe mama anaoga vizuri, anakula vizuri anapaka mafuta mazuri anapendeza kwa pesa ambayo umeitoa wewe mwanamume,” amesema.

“Sio atumie tu pesa ambayo amehangaika nayo juani. Kuna matukio wengine kinamama wakitoka sokoni mnawanyang’anya hela. Jamani kweli hii ni haki? Najua sio wote lakini wapo.Unamnyang’anya pesa unaenda kunywa pombe,”ameeleza.

Chanzo: Mwananchi
 
Na kweli wengi waakishatoa pesa ya chakula mengine na bills zingine za nyumbani hayo ya kupendeza skjui kusuka kuvaa huwa hayawahusu ..kuna wanawake wanaishiwa hadi nguo za ndani na mwanaume hajali cha ajabu alimkuta anapendeza kabla hajamuoa.ila kuna wanaume wanaroho ngumu aisee anamkuta mkewe kapendeza na hajahusikakatika mchakato wa kupendeza kwake..kuna wale mabahili utaskia anakwambia usiposuka,usipopaka lotion unapendeza ...hela yake hatoi voluntary hadi uombe hata kama uanaona kuna uhitaji wa lazima..make mjamzito mimba anaiona hadi aombwe hela ya gauni..huo uzwazwa
 
Hiyo ni kauli ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Sanya Juu wilayani Siha, Janeth Mvungi, aliyoitoa katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kueleza kuwa upo ukatili wa kiuchumi kwa mwanamke ambao hauzungumzwi sana.

Akizungumza katika maadhimisho hayo leo Desemba 11, 2023 huko Sanya Juu, , Mvungi amesema kuna ukatili wa kijinsia ambao unasahaulika nao ni ukatili wa kiuchumi.

“Kuna ukatili ambao huwa unasahaulika sana nao ni ukatili wa kiuchumi na watu wanaongelea tu kipengele cha mwanamke kupewa nafasi ya kumiliki mali. Naomba niseme hata mke wako usipompa pesa unamkatili kiuchumi,”amesema.

“Sheria ya ndoa inasema mwanamume ana wajibu wa kumtunza mke wake na familia. Japo mwanamke naye anakuwa na huo wajibu kama amemzidi mwanamume kipato lakini mara nyingi familia zetu mwenye kipato ni baba,” amesema.

“Kwa mila na tamaduni zetu mwanamume ndiye anayesimamia familia. Mama Yeyooo (kinamama wa Kimasai) mnapewaga eeh? (sauti zikasika hapanaaaa). Wanasema hamtowi. Jamani tubadilike,”alisema Hakimu huyo na kuongeza:

“Kina baba kutowapa kina mama hela na matunzo ni ukatili wa kiuchumi naomba tubadilike mhakikishe mama anaoga vizuri, anakula vizuri anapaka mafuta mazuri anapendeza kwa pesa ambayo umeitoa wewe mwanamume,” amesema.

“Sio atumie tu pesa ambayo amehangaika nayo juani. Kuna matukio wengine kinamama wakitoka sokoni mnawanyang’anya hela. Jamani kweli hii ni haki? Najua sio wote lakini wapo.Unamnyang’anya pesa unaenda kunywa pombe,”ameeleza.

Chanzo: Mwananchi
Marriage Contract versus Marriage Business Contract.

NB: Marriage is not an employment contract nor the source of income for either part of the marriage.
 
Back
Top Bottom