Chama cha walimu Kilindi wasaidieni walimu waliopewa uhamisho wa dharura waliotajwa hapo juu na sio kujiunga na ofisi ya DED Kilindi

Nguva Jike

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
853
1,005
Habari za mchana great thinkers wote.

CWT KILINDI TENDENI HAKI

Chama cha walimu Kilindi wasaidieni walimu waliopewa uhamisho wa dharura waliotajwa hapo juu(BONDO NA PARAKUYO) na sio kujiunga na ofisi ya DED KILINDI kuwakandamiza na kuwapa vitisho mkumbuke zama hizi sio za vitisho na mkumbuke kuwa hizo supu za kuku mnazochemsha kila asubuhi ni michango yetu na sio yenu.


OFISI YA DED KILINDI

Baadhi viongozi wa cwt waliwatonya wanachama wao kuwa ofisi ya DED na DPEO mpaka kufikia mwezi December 2023 ilikuwa na pesa inayotosha kuwapa chochote walimu hawa wa uhamisho wa dharura lakini hawakupenda kuwapa hata gari kuwahamisha.

Kingine yule ofisa anaetoa vitisho kwa walimu hawa wanaodai tayari mchana huu leo tarehe 01.02.2024 ameripotiwa kwenye mamlaka husika athibitishe kuwa anaeandika habari hapa Jamiiforum kuhusu hawa walimu ni mwl fulani(audio ipo akimtaja mwalimu huyo).

Ofisa huyu akishindwa kuthibitisha atalipa faini kali ambayo hajawahi kulipa tangu azaliwe.

Mwisho nasema hivi ukijiona unacho kikubwa cha kupoteza be careful na mtu ambae hana cha kupoteza kwani huyu hataacha kuanika vile unavyoviogopa sana na anavyo vingi sana tena na ushahidi usio na shaka
 
Back
Top Bottom