polisi walibaka wanafunzi UDOM?

kweleakwelea

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
3,065
1,535
Ndugu wanaJF!

jana katika pita pita nilikutana na mzee mmoja ambaye alinihakikishia kuwa kutoka kwenye chanzo cha uhakika amepata habari kuwa kuna polisi walirape wanafunzi wakati wamewatawanya na mabomu ya machozi katika vichaka vya Makulu - maeneo ya UDOM.

kutokana na utata / uzito wa suala lenyewe mara nyingi wanaobakwa huwa ni wazito kusema na hujikalia kimya waklibubujikwa na machozi!

tunaomba wenye info zaidi watuhabarishe! au kama kuna mashirika / asasi ambazo zinaweza kufuatilia suala hili walifuatilie na tujue mwisho wake!

naomba kuwasilisha!
 
Kama una ukweli ni vema wadau wakafuatilia maana mhanga anaweza kweli kuficha kwa ajili ya privacy yake but wahusika wanatakiwa kuchukuliwa hatua kali kupunguza kama siyo kuzuia matukio mengine kama hayo.
 
Kama ni kweli, tunaokoelekea si kwenyewe, yaani nchi imepotea njia. Walioapa kulinda raia kwa nguvu zao zote leo tena wanabaka raia? wameona mabomu na virungu havitoshi? nikiwa mwanamke nalaani kitendo hicho na Namuomba Mungu ninayemuamini akifunue kitendo hicho kwani yule aliyekifanya atakamatatwa tu, kama si leo basi siku zijazo!!!
 
Unategemea nini unapoajili wengi wao wakiwa wamefeli form4 na bila kuangalia maadili tatizo ni mfumo mbovu wa kuwa recruit ccp ndo wanafundishwa tabia mbaya zote matusi umalaya na maadili mabovu yote!
 
Hizi ni shutuma nzito sana na hazipaswi kufumbiwa macho. Tatizo katka suala la ubakaji mara nyingi ni vigumu kupata ushahidi hasa ikiwa zimepita siku nyingi, na zaidi ikiwa wahusika ni polisi wenyewe. lakini hakuna anayepaswa kuwa juu ya sheria. Kwa hivyo ninawaomba wana JF tulifikishe suala hili TAMWA ili walishughulikie.
 
Back
Top Bottom