Polisi wafufua kitengo cha kuchunguza uhalifu mtandaoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wafufua kitengo cha kuchunguza uhalifu mtandaoni

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Sep 19, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  JESHI la Polisi limeunda timu ya kuchunguza matukio ya uhalifu kwa njia ya mitandao, simu za mikononi, ATM za mabenki na huduma nyingine za mitandao cha Ant cyber crime Unity ili waweze kubaini watu wanaotumia mitandao hiyo, kinyume na taratibu.
  Hatua hiyo, imekuja baada ya kutokea matukio ya wizi katika ATM za benki, wananchi kutumiana ujumbe wa matusi kupitia mtandao na simu za mikononi na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, (DCI) Robert Manumba alisema matukio hayo, yameibuka nchini hivi karibuni na kusababisha baadhi ya wananchi kupata matatizo.
  Alisema wananchi wengi wamekuwa wakitumia mitandao hiyo, kinyume na taratibu, na kusababisha upotevu wa fedha.
  Alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo litawashughulikia wananchi wote watakaobainika kufanya vitendo hivyo, kinyume na taratibu.
  “Kuna baadhi ya wananchi wanatumia mitandao vibaya, baadhi ya wanatumia ili waweze kuwatukana wenzao, wengine kuiba na kusababisha malalamiko mengi kutokea,” lisema Manumba.
  Alisema timu hiyo, itahakikisha wanaofanya vitendo hivyo, wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
  Manumba alisema hivi sasa wanaboresha timu hiyo ili iweze kufanya kazi na kwamba anaamini mpango huo, utafanikiwa.
  Alisema timu hiyo, ilikuwepo muda mrefu, lakini ilishindwa kufanya kazi kwa sababu matukio ya wizi kwa kutumia mitandao, haikuwepo.
  Wakati huo huo, Manumba alisema hivi sasa wanakichunguza chama cha kiislamu kinachojishughulisha na kutetea haki na maslahi ya waislamu nchini.
  “Kuna baadhi ya kundi la watu linalojishughulisha na masuala ya siasa ndani ya dini, jambo ambalo linaweza kusababisha mvutano kwa wananchi, kutokana na hali hiyo, tunatakichunguza kwanza ili tuweze kubaini undani wake na kazi wanazozifanya na ikabainika wamekiuka taratibu, watachukuliwa hatua za kisheria,”alisema.
  mwananchi


  http://www.mzalendo.net/polisi-wafufua-kitengo-cha-kuchunguza-uhalifu-mtandaoni
   
 2. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,464
  Likes Received: 1,404
  Trophy Points: 280
  ila bado wana kazi kubwa sana kwa kuwa jeshi letu huwa halina taratibu ya kutaka msaada kutoka kwa wataalam wazawa
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Sep 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  mbona wanavumbua kikosi hicho bila kuwa na sheria za mitandao ?
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Sep 19, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tatizo la utendaji kazi nchini kwetu huwa tunasubiri matukio ndio tufanye kazi! Huwa hatu-foresee matatizo kabla hayajaanza. Kwa ujumla wahalifu wana vision kubwa kuliko serikali yetu! Serikali ilikolala ndiko wahalifu walikoamkia!
   
 5. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Hao ni NATO (No Action Talking Only)

  Utawezaje kudhibiti uhalifu wa mtandaoni (cyber crime) bila kuwa na legal framework kwenye electronic media? Hivi unajua kuwa huwezi kutumia e-mail kama ushahidi mahakamani? Sasa huyu Manumba anaongea nini, au ni kuhadaa watu?

  Kama wangekuwa wanaona mbali, basi wangeanza ku computerize police stations .. angalau basi makao makuu!

  Ukienda kwenye kituo cha police, hapa pale central police, kila kona kumejazana karatasi, hata photocopy machine hakuna, achilia mbali hiyo internet.

  Hivi huyu jamaa, anajua anachozungumza kweli?
   
Loading...