Polisi wafuata ushauri wa Kinana bila shuruti

Polisi wafuata ushauri wa Kinana bila shuruti

Mi naona waondolewe wote,wabaki stendi za mabasi,tuone kama kuna shida yoyote au mnasemaje wadau wa barabarani?
Halafu tukifanya hivyo,mwakani mwezi kama huu,turudi tutoe mrejesho wa kuishi barabarani bila trafiki,endapo tutakua hai baada ya MBANGA za maana kunako rodi.
 
Bora iwe hivi maana wanajifanya wanaijua Hela kuliko ukimpa 5,000 anatakaa anakwambia nipe 10,000 Sasa wasubiri mishahara Tu.
 
Nimeamini kuwa chama ndiyo kinashika hatamu hapa nchini.

Kufuatia ushauri wa Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Kinana kwa Polisi kupunguza idadi ya Askari wa Traffic barabarani.

Leo hii Polisi wamesema kuwa watatekeleza maagizo hayo mara moja.

Hakika CCM imejichimbia sana kwenye taasisi zetu za Serikali.

Ndiyo maana leo hii tunawaona wastaafu wa Jeshi hilo wapo kwenye uongozi wa chama hicho kikongwe.View attachment 2308152
#katibampya
 
Ajali za barabarani zilizokuwa chinja chinja miaka ya nyuma zitarudi kwa kasi sana

mswahili kama mbuzi tu usipomsimamia kaisha

Waliopendekeza wanasafiri na ndege au wanasafiri na misafara ya ulinzi. Hatari za barabarani hazitawagusa. Ni wanyonge wanaosafiri kwa mabasi ya abiria na magari binafsi ndiyo watateketea.
 
Wakiwapeleka kwenye mabenki na sehemu nyinginezo,atakayekua anapima ajali ni nani,maana lazima wananchi tujiandae kisaikolojia kwa yatakayofuata,yaani ajali za kutisha.Mi naona jeshi la polisi liangalie namna,wasifuate ushauri tu,watulinde sisi na mali zetu yaani vyombo vyetu,hakuna haja ya kuwapunguza sana trafiki.
 
Ajali za barabarani zilizokuwa chinja chinja miaka ya nyuma zitarudi kwa kasi sana

mswahili kama mbuzi tu usipomsimamia kaisha
Naafikiana nawe.
Huenda jambo hili ni jema lakini naomba litazamwe kwa makini kabla ya kulitekeleza.
Sina hakika iwapo kuna tahadhari ya kutosha kwa watumiaji wa barabara.

Ninapokwenda Burundi au Rwanda naona wanakagua mambo yote yanayohusu gari.
Maji ya kuosha kioo cha mbele,
Tairi,
Taa zote - nilitozwa faini kwa kuwa taa ya kuwasha namba ilikuwa haiwaki.
Nk
Tuchukue tahadhari.
 
Na ajali za barabarani zikiongezeka kwa fujo za barabarani msilaumu. Viongozi wanaosafiri na ulinzi barabarani au wanasafiri kwa ndege hawataathirika. Ila watu wa kawaida wanaosafiri na mabasi na magari binafsi ndiyo watapata shida.
Sheria zipo na adhabu zipo za kutosha kwenda zako huko mla Rushwa wewe
 
Itakua safi sana kwa sie tunao cruise na vyuma mikoani...ila ajali zinaweza ongezeka kiaina....
Wanaopunguzwa ni wa mijini tu kwa mujibu wa kero ilivyowasilishwa na Kinana, wewe wa mkoa tu mkoa tochi zipo pale pale. Kuwa mpole
 
Nimesikia Jeshi la Polisi linafanyia kazi Ushauri wa Kupunguza idadi ya Askari wa Usalama barabarani.Binafsi nadhani Wangeongezwa badala ya Kuwapungaza ili kuwakabili Madereva wengi wanaosababisha Ajali na ukizingatia Kuna idadi kubwa ya Ongezeko la Magari barabarani.Hofu ni Kwamba ASKARI wa Usalama wakipunguzwa basi kuna Madereva hawatafikiwa kabisa na Mkono wa Sheria pale watakapovunja Sheria za Barabarani.
Traffic Mla Rushwa wewe Koma Tafuta namna ingine ya kuishi
 
Sheria zipo na adhabu zipo za kutosha kwenda zako huko mla Rushwa wewe Traffic wa barabarani mshenzi wewe

Unaongea utumbo. Madereva wahuni tangu lini wanafata sheria? Wewe subiri utaona ajali zitakavyozidi halafu ndiyo utajua kama kuna sheria na adhabu.
 
Back
Top Bottom