Polisi wafuata ushauri wa Kinana bila shuruti

Polisi wafuata ushauri wa Kinana bila shuruti

Hongera Kijana, Leo kwa Mara ya kwanza nimeendesha gari kwa utulivu Sana, hizi jamaa zinaboa Sana, kazi zao wanafanya with no logic
Logic kwao ipo maana wanakuwa wanafanya makusanyo na jioni wanapiga maheaabu
 
Nimeamini kuwa chama ndiyo kinashika hatamu hapa nchini.

Kufuatia ushauri wa Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Kinana kwa Polisi kupunguza idadi ya Askari wa Traffic barabarani.

Leo hii Polisi wamesema kuwa watatekeleza maagizo hayo mara moja.

Hakika CCM imejichimbia sana kwenye taasisi zetu za Serikali.

Ndiyo maana leo hii tunawaona wastaafu wa Jeshi hilo wapo kwenye uongozi wa chama hicho kikongwe.View attachment 2308152
TUNAPOSEMA POLICCM ndio Tafsiri yake hiyo Wenye Akili kubwa Tunajua Siku nyingi ndio Maana Tunataka KATIBA MPYA
JamiiForums1966179623.jpg
 
Hongera Kijana, Leo kwa Mara ya kwanza nimeendesha gari kwa utulivu Sana, hizi jamaa zinaboa Sana, kazi zao wanafanya with no logic
Subirini mtaona impacts... Tukutane hapahapa!!
 
Kuna trafic vijana wanavaa uniform za kaki wamenda magomeni ni hatari sana.Mimi nilipanga kuhama CCM kisa trafic.
 
Traffic wanapaswa kubaki kwenye vivuko (Zebra Cross) kuwasaidia watoto kuvuka barabara kwa usalama zaidi.

Wengine wapelekwe kulinda Bank na kupambana na Panya road.
Hapo kwenye panya road ndiyo wengi wataomba kustaafu
 
Na ajali za barabarani zikiongezeka kwa fujo za barabarani msilaumu. Viongozi wanaosafiri na ulinzi barabarani au wanasafiri kwa ndege hawataathirika. Ila watu wa kawaida wanaosafiri na mabasi na magari binafsi ndiyo watapata shida.
 
Hawa jamaa wamejikaanga wenyewe kwa kujaza vijana wadogo, vilaza na wasiojua maisha barabarani. Yako makosa ya kutoa onyo la kawaida au ni sehemu ya defensive driving ila wao wamekuwa wakiyakomalia bila kujua kundi la wenye magari Tanzania wengi wao ndio hao hao walioko sehemu mbali za maamuzi Serikalini. Sasa watu washafanya yao. Kama mjini wamezidi unadhani watapelekwa wapi? Kukamata baiskeli kule sikonge? Simply waende kulinda mabank sasa. Sangoma zamu yao kula zile zilizopatikana kupitia za kubrashia viatu.
 
Nimesikia Jeshi la Polisi linafanyia kazi Ushauri wa Kupunguza idadi ya Askari wa Usalama barabarani.Binafsi nadhani Wangeongezwa badala ya Kuwapungaza ili kuwakabili Madereva wengi wanaosababisha Ajali na ukizingatia Kuna idadi kubwa ya Ongezeko la Magari barabarani.Hofu ni Kwamba ASKARI wa Usalama wakipunguzwa basi kuna Madereva hawatafikiwa kabisa na Mkono wa Sheria pale watakapovunja Sheria za Barabarani.
 
Hii ndio Taarifa mpya iliyotufikia hivi punde , Kwamba baada ya Mzee Kinana kupendekeza polisi wa Trafiki kupunguzwa barabarani , kwa vile ni wengi mno kiasi cha kuwa kero (rushwa), Mchakato wa upunguzaji ushaanza .

Hii ni baada ya Msemaji wa Jeshi la Polisi kukiri kupokea ushauri wa Mzee Kinana na kwamba ushauri huo unafanyiwa kazi .

Hakuna atakayefutwa kazi bali wengi watapangiwa Ulinzi wa Mabenki , fukwe , madaraja na masoko , ni masuala ya kubadilishiwa maeneo ya kazi tu .
 
Back
Top Bottom