Jamani ngoja nimtetee Polisi mnayedai anawachekea hao watuhumiwa, ukimwangalia kwa makini utagundua kabisa chuki ya kizalendo aliyonayo dhidi ya hao jamaa, tena utagundua kuwa hajafurahishwa kabisa na kitendo chao kukumbatiana ila tu hana namna inabidi atimize amri. Mwangalieni kwa makini mtagundua kitu. Pia huyo mwanadada siyo kuwa anafikiria nyumbani kwake bali kitendo cha hao watuhumiwa kukumbatiana tena mbele yake kimemchefua kiasi cha kuamua kuangalia pembeni ili asije akawarukia bure, yakawa mengine.