Kwanini TCRA na Jeshi la Polisi wasiweke utaratibu maalum wa namna watu wanavyoweza kuuziana vifaa vya mawasiliano pasipo kuhusishwa na uhalifu?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya thanks to God the Almighty.

TCRA na Polisi waweke utaratibu maalum wa namna watu wanaweza kuuziana vifaa vya mawasiliano pasipo kuhusishwa na uhalifu.

Unakuta kwa mfano Athumani ananunua simu kutoka kwa Alexander alafu baada ya mwezi mmoja Athumani anakuwa tracked na wataalam wa TCRA pamoja na Police kisha anakamatwa nyumbani kwake Mbagala kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi.

Unaweza kukuta si Athumani wala Alexander ambao ni wezi, ila kwa kuwa umekosekana utaratibu mzuri wa kufanya transactions za secondhand communication devices, unakuta baadhi ya watu wanaingia katika mkenge wa kujihusisha na uhalifu pasipo kujijua.

Unakuta huyo Alexander alinunua simu mwaka 2017 miaka miwili iliyopita jambo ambalo kwa hali ya kawaida ya kibinadamu na maisha yetu ya kiafrika ni ngumu mtu kutunza receipt ya manunuzi, hivyo na yeye pia ilimlazima auze simu ile pasipo kukabidhi original receipt.

Kwanini sisi watanzania tunashindwa kujiwekea utaratibu mziri wa maisha yetu mpaka tusubiri wazungu waanze na sisi ndio tuige?

Mbona TRA wanao utaratibu mzuri sana wa kufanya motor vehicle transfer kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ilhali wamiliki wa magari na wachache sana ukilinganisha na wamiliki wa simu za kiganjani?

PROPOSED SOLUTION: Kabla ya kuuza handset, mtu anapaswa kufuata clearance letter kutoka police itakayoonesha ya kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa kifaa hicho na hakijawahi kuhusika katika tukio lolote la kihalifu.

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

IMG_20190925_182650_132.jpg

VODACOM WAME-COPY "CONSTRUCTIVE IDEA" YANGU. WANILIPE.
 
Yeye anakimiliki kwa muda gani.? Kama ni mtu wa karibu lazima utafahamu historia ya kifaa. Alianza kukimiliki lini na alikipata kwa njia gani?
Ukinunua kichwakichwa tunakupoteza kwa kesi ya kichwa.
Boss, kitendo cha wewe kutumia neno "tunakupoteza" inaonesha ya kuwa wewe ni mtu wa mabavu na sio muungwana. Wewe sio problem solver. Dunia ya sasa ya science and technology inahitaji akili sana katika kukabiliana na watu kuliko mabavu na nguvu
 
Hili lipo kwenye ustaarabu au mabadiliko ya tabia zaidi kuliko sheria mkuu.
Hata hivyo tukiendesha vizuri zoezi la kusajili line za simu kwa vitambulisho vya simu, hili tatizo la kuuziana simu za wizi litapungua sana.
 
Hili lipo kwenye ustaarabu au mabadiliko ya tabia zaidi kuliko sheria mkuu.
Mkuu, ata uhalifu wa ubakaji umetungiwa Sheria kwa maana watu wameshindwa kuwa wastaarabu au kubadilika tabia. Kesi za kununua simu za wizi zimekuwa ni nyingi mno. Serikali ije na utaratibu maalum kama vile TRA wanavyofanya motor vehicle transfer
 
Usiwatwishe watu majukumu yasiyo na mashiko mshikwe tu kama unajua kuna maswala hayo ya kuingia matatani why hutumii akili unakurupuka kibwege kununua vitu bila utaratibu,mnalalamika tu sio watu walio jela wana hatia saa nyingine ni uzembe kama huu,kitu kinachoweza kukuokoa ni risiti sasa wewe huna risiti watu watakuamini vipi.Kuhusu swala la kutunza risiti waafrika wengi huwa hatuzingatii vitu kama hivi tunapuuzia.Mimi hapa mpaka leo nina risiti za simu niliyonunua 2009
 
Huo utaratibu wako wa kuja na shikamoo utakuja kuamkia hata watoto wa shule ya msingi,unakuja humu unasema wakubwa zangu shikamoo kumbe wewe ndio mzee kuliko wote humu JF
 
Back
Top Bottom