Infopaedia
JF-Expert Member
- Oct 28, 2011
- 1,231
- 1,487
Habari zenu wana jamii. Leo nimeona tuongeee kidogo kuhusu hawa askari wetu wa úsalama barabarani.
Ukiangalia hicho kiambatanisho hapo juu, hilo ni Kosa la barabarani ambalo askari amemuandikia dereva. Japo kuwa hilo Kosa inaonekana ni la kujitungia tu, lakini shaka yangu si juu ya hilo. Kinachonisikitisha ni weledi na namna ya kufikiri ya huyu askari wa barabarani. Kumbuka huyu amepewa dhamana ya kusimamia sheria za barabarani na kutupunguzia kero watumiaji wa hizi barabara.
Kwa kichwa cha huyu askari, hakuna msaada wowote ama tija kwetu sisi au wateja wake. Ameandika kwamba Kosa ni "kushindwa kufunga mkanda wa úsalama" au "kushindwa kuvaa kofia ya úsalama". Hapa sijui wana jamii mnaelewa nini. Yawezekana mimi ni huu uzee ndio unanifanya nisielewe.
Hayo makosa yana asili ya gari na pikipiki na haiwezekani mtu kuwa na gari na kufanya hayo makosa mawili. Ni wazi aliamuwa kutunga tu. Nina uhakika anajua haya ni makosa ya vyombo viwili tofauti, lakini bado akaamuwa kuandika. Hapo ndipo ninapotia mashaka sana juu ya jeshi letu la police.
Kama nilivyosema awali, kwa police kuamua tu kutunga Kosa hainisikitishi sana. Kinachotia hofu na simanzi ni weledi na mawazo ya huyu askari wakati anaandika hili Kosa na adhabu yake. Aliandika akijua si kweli lakini anaamini huyu mtanzania atalipa tu.
Kama ni hivyo ndugu zangu, kuna shida kubwa katikati ya hili jeshi letu la úsalama barabarani. Shida ya kimfumo, weledi, na maadili. Kuna haja ya kuliangalia upya hili jeshi. Jeshi haliwezi kupata ama kuwa na tija iwayoyote kutoka kwa askari wenye mtazamo na akili kama hizi.
Watanzania wengi hatupendi usumbufu, kwa tabia yetu hiyo police kama hawa na wengine wengi huamua kututumia, ama kwa faida yao au kwa ujinga tu na kuridhisha kiburi chao.
Binafsi katika pilika zangu za kusaka tonge, huwa natumia muda mwingi nikiwa na raia wa kigeni. Ninapokutana na maafisa wa serekali nikiwa na hawa raia wa nje, huwa naipata wakati mgumu sana kuanzia kuitetea serekali yetu kwa hawa wageni. Yaani ni lazima mtu wa serekali afanye kituko cha kipumbavu tu. Huwa sependi kukubali serekali yetu ionekane ya kijinga kwa wageni.
Basi naanza kujitutumua na kiingereza changu cha kuungaunga. Jamani mnatuchosha sana.
Kwa Kosa kama hilo hapo juu naanzaje kulitetea jeshi letu!!! Hapo pana tatizo kubwa la kimfumo, weledi, na maadili.
Lakini endapo atatokea kiongozi wa jeshi kuelezea hilo Kosa, a naweza akaja na maelezo mepesi sana kiasi kwamba unaweza dhani muandishi wa hiyo fine na huyo kiongozi wa jeshi, ni mtu mmoja.
Wakatabahu
Infopaedia