Ipo haja faini za barabarani zinazohusu speed kwenda automatic kwenye simu ya mmiliki

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,533
Ili kuondoa mianya ya rushwa, mabishano nakadhalika. Polisi Usalama Barabarani wabaki kukagua mambo mengine, zitegwe speed detectors, ukizidisha mwendo message inakuja tu kwenye simu yako unapambana na hali yako, askari wapungue road wabaki vehicle inspectors tu na wakaguzi wa makosa mengine ambao wanakuwepo kwenye vituo maalumu tu. Hawa wanaohangaika na speed wasiwepo.

Pia, magari mabovu yasiruhusiwe kutembea barabarani.

Twende tukajifunze Rwanda. Ustaarabu, usalama barabarani na usafi wa nchi yetu unaanza na hatua hii. Pia Serikali itaokoa mapato mengi yanayopotelea kwa wazee wa ya kubrashi viatu.
 
Kesho tu unakuta speed detector camera imepuliziwa Rangi ya spray na mtu aliyevaa mawani kubwa usoni
 
Yani nilipe 30k wakati nayajenga na mdau nampa 5k ananiachia naenda?

Acha mambo yako mjomba ukiendesha toka dar mpaka mbeya utapigwa tochi zaidi ya mara 30 njiani, imagine hamna traffic ni hizo speed detectors tu kila ikikupiga inakupa notification ya fine, mind you Kuna baadhi ya traffic sio wote ukiutengeneza uwongo vizuri anakusamehe, Kuna wengine wanachukua hata buku 2 sasa hilo jini unalolitaka kama unafanya safari ndefu na hizi barabara zetu za kila Kona 50kmH mbona balaa.
 
Hii itasaidia sana hata wamiliki wa magari ya kibiashara kufahamu mienendo ya madereva wao wanaowatia hasara😇
 
Mi utaniua kutembea mchana kero kama zote na mbaya zaidi ukitii hiyo 50 ndo unakutana picha unaonyeshwa umezidi speed 55 badala upewe onyo au achukue ya kubrush viatu ndo kwanza anaomba leseni akuandikie fine.

Night raha sana kikubwa uijie njia na gari liwe zima!
 
Siku ukiharibikia kona za Iyovi makao makuu ya popo bawa ndo unaweza kusema mkate ni chakula kamili kama Somalia. Risk sana kusafiri usiku aisee
 
Ili kuondoa mianya ya rushwa, mabishano nakadhalika. Polisi Usalama Barabarani wabaki kukagua mambo mengine, zitegwe speed detectors, ukizidisha mwendo message inakuja tu kwenye simu yako unapambana na hali yako, askari wapungue road wabaki vehicle inspectors tu na wakaguzi wa makosa mengine ambao wanakuwepo kwenye vituo maalumu tu. Hawa wanaohangaika na speed wasiwepo.

Pia, magari mabovu yasiruhusiwe kutembea barabarani.

Twende tukajifunze Rwanda. Ustaarabu, usalama barabarani na usafi wa nchi yetu unaanza na hatua hii. Pia Serikali itaokoa mapato mengi yanayopotelea kwa wazee wa ya kubrashi viatu.
Wacha mambo yako wewe! Unataka sisi tukale wapi?
 
Back
Top Bottom