Polisi Tanzania wabana waachia, sherehe za Pasaka ruksa

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Jeshi la Polisi leo April 2, 2021 wametoa ufafanuzi juu ya kauli waliyoitoa kuhusu shamra shamra za kusheherekea sikukuu za Pasaka.

‘Taarifa ya Jeshi la Polisi niliyoitoa jana (pamoja na mambo mengine) ilisema tuna imani kama kila Mwananchi atafuata Sheria na kujiepusha na vishawishi vya kufanya uhalifu, Ibada ya Pasaka itamalizika salama na hatutegemei zile Sherehe na Shamrashamra tulizozizoea kipindi cha miaka ya nyuma kuwepo katika kipindi hiki, kwa bahati mbaya taarifa hiyo ilipokewa na tafsiri tofauti kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku Sherehe za Pasaka”– David Misime-SACP, Msemaji wa Polisi

“Jeshi la Polisi halijapiga marufuku Sherehe za Pasaka na ndio maana hata jana Ibada ya Sikukuu ya Alhamisi Kuu ilifanyika Nchi nzima bila bughudha yeyote na Askari wetu waliovaa sare za Polisi na waliovaa kiraia walikuwa doria kuhakikisha amani, utulivu na usalama unakuwepo”

“Jambo ambalo hatutegemei kuliona ni zile shamrashamra kubwa kama vile Matamasha na Makongamano ya Pasaka na kwa bahati nzuri wanaoyaandaa kila mwaka kwa utu wao wa Kitanzania, hekima na busara zao hatujasikia wakitangaza maandalizi ya Matamasha hayo”

“Ibada za Sherehe za Pasaka kwenye Makanisa, Sherehe za Kifamilia, Hitma, Familia kuungana na kwenda kutembelea sehemu mbalimbali na kusherehekea Pasaka hakuna aliyekataza ili mradi unachofanya kinaendana na kufuata utu, busara, hekima, Sheria , kanuni na taratibu za Nchi”

PIA SOMA:

CHANZO: Millard Ayo
 
Tatizo wanapenda sana kujitoa ufahamu. Kabla ya kukurupuka na lile tangazo lao la kujipendekeza, walitakiwa wajiongeze kwanza kujua nini maana ya siku 21 za maombolezo ya kifo cha Rais wa nchi.

Mimi ningesherehekea tu Pasaka hata kama wangejifanya kukaza shingo zao.
 
Tatizo wanapenda sana kujitoa ufahamu. Kabla ya kukurupuka na lile tangazo lao la kujipendekeza, walitakiwa wajiongeze kwanza kujua nini maana ya siku 21 za maombolezo ya kifo cha Rais wa nchi.

Mimi ningesherehekea tu Pasaka hata kama wangejifanya kukaza shingo zao.
Serikali inaendelea na teuzi na tenguzi halafu wananchi wasishangilie Ukombozi wa Bwana Wetu Yesu Kristo

Walilogwa haswa na naniliiii
 
Haa 😂😁
Kosa Moja Linaweza Kulitikisa Jeshi Zima La Police Tanzania
 
Mwanakondoo ameshinda...

Polisi waache unafiki yaani vitendo vya uhalifu vifananishwe na shamrashamra,hebu wajifunze kuwa waungwana kwani ukisema tulikosea utakufa.
 
Mtangulizi aliwaachia sana
Mama alisema 'Niwatakie Pasaka Njema hakusema Muendelee na Maombolezo....
Wajinga ndio waliwao mpunguze kuropokaropoka kama nchi yenu haya sasa Fullu Aibu....
Hapana, hakuwaachia!
Walikuwa wakitimiza matakwa yake.

Kwa hili wamejisahau na kudhani bado wanamfurahisha yeye, kumbe yeye hayupo tena.
 
Serikali inaendelea na teuzi na tenguzi halafu wananchi wasishangilie Ukombozi wa Bwana Wetu Yesu Kristo

Walilogwa haswa na naniliiii
Ni kweli kabisa, lakini tusisherehekee kupita kiasi na kusababisha ajali au kutumia Sikukuu ya Pasaka kusheherekea yasiyohusu Sikukuu hiyo.
 
Hawa Polisi wa Tanzania huwa wanafanya maamuzi kama watoto wadogo waliovaa pampasi ambao hawajui la kufanya.
 
Back
Top Bottom