Diva Beyonce
JF-Expert Member
- Mar 6, 2014
- 12,913
- 11,292
Mtoto wacha kupaka matope jeshi letu tukufu
Jeshi takatifu linapokea rushwa labda virse versa
Mtoto wacha kupaka matope jeshi letu tukufu
Nashangaa wote mnatoa tuhuma kwa polisi kupokea rushwa sijaona hata mtu mmoja akiwahimiza madereva wasiwape polisi rushwa wakati kila mmoja wetu tunafahamu kuwa mtoa rushwa na mpokeaji wote wanahatia. Nadhani kuikomesha rushwa ni kitu kidogo nikuwambia madereva waache kutoa rushwa kwa askari kinyume cha hapo tutabaki kuimba wimbo wa rushwa kama wendawazimu.
Jeshi takatifu linapokea rushwa labda virse versa
Hilo wazo zuri. Lakini pia ni vema watu wa TAKUKURU kujaribu kuingia field. Yani nina uhakika lazima watamkamata trafiki hasa kipindi hiki cha sikukuu. Kutoka Dar wakifika Chalinze tayari watakua wameshakamata tukio la Rushwa maana haya mambo yanafanywa nje nje bila kificho.
Polisi wamezidi njaa
Inawezekana pia watoa rushwa hawana elimu ya kutosha kuhusu haki zao. Lakini upande wa polisi wao ndio wanajua lakini kwa nini wao wanavunja sheria hadharani? Hivi asilimia 99% ya magari ni mabovu kama unavyodai ndio ticket ya kupokea rushwa?
Difficult to track down and prosecute since raia kazi yao kupiga kelele kwenye mitandao.
piga kelele kwa serikali iwaongezee masilahi huenda kero hizo zikaishaKwanza mimi sio mtoto nimeshuhudia kwa macho yangu. Ikaniuma kwa ajili ya nchi yangu. Kwa nini rushwa imekua hadharani kiasi hiki? Tunaipeleka wapi nchi yetu? Trafiki hawana hata aibu.
unaona wanafaidi sana? wivu tu nenda na ww ukaombe kazi hiyoKama gari bovu sheria si zipo? Kwanini kujishusha hadhi kazi yao kwa ajili ya sh 2000? Hata kama njaa polisi wamezidi. Na Kwanini usimamishe gari halafu unazunguka nyuma ya gari?
Nimekuwa safarini siku mbili hizi na nimeshuhudia rushwa nje nje imekuwa kama tuko Nigeria vile. Yaani traffic police wanasimamisha magari halafu hawaji kwenye gari konda anazunguka nyuma ya gari anampa hela. Na hiki kipindi naskia wanatafuta hela ya sikukuu ni wamejaa humo barabarani usiseme.
Kilichoniuma ni kuwa kimsingi polisi ndio wasimamizi wa sheria lakini wanachukua rushwa huku raia wakishuhudia. Hali hii inatisha. Mbaya sana. Hata watoto wadogo wanaona wanajifunza nini? TAKUKURU Wapo na hawaoni haya yanayotokea. Mbaya!!!
Kwahyo raia wakipiga kelele ni haki yao kuchukua rushwa na njaa zitawaua kuomba mara ya chai
Mkuu kilichobaki kwa wewe ni kudeclare interest kuwa na wewe ama ni mmoja wao au una maslahi na hawa polisi.
Takukuru ni wasanii wale, kama wangekuwa wanafanya kazi zao basi rushwa isingeendelea kushamiri nchini.
Wamezidi sasa maana hata madereva wanalalamika maana imebidi apunguze dau alianza na buku mbili akashuka hadi jero kaona karibu kila kituo wapo. Na traffic wasivyo na haya wanachukua tu.