Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,411
Jeshi La Polisi idara ya TRafick inafanya kazi kwa weledi wa hali ya Juu.
Hawa Polisi ambao wale wa vyeo vya chini huvaa sare nyeupe za kupendeza na kuonyesha unadhifu wa hali ya juu nje ya mwilina ndani ya roho sijui lakini pia wale wa vyeo vya juu huvaa nguo za kaki za kupendeza wanyonge huku wakiwa na mikanda viunoni ya ngozi za ngombe.
OPERESHENI:
1. STIKA YA NENDA KWA USALAMA: Hii ni biashara rasmi ambapo lengo kuu ni gari lipelekwe trafick section na kukaguliwa, likikidhi vigezo basi dereva alipie stika na liendelee na safari lakini imekuwa utaratibu stika kuuzwa kwa elfu 5 kama ukienda kituoni na kama ukiitaka barabarani inauzwa elfu 10.
Hakuna ukaguzi unaofanyika wa gari lolote na kichaka tu cha upigaji cha wau wachche sana ambao wanaishi kama wafalme.
2. LESENI/LENA. Ili kupata leseni yakupasa kupitia shule za udereva na kufanyiwa majaribio, lakini baada ya kufuzu pia kuna hatua za kupita, huko kila hatua niutoa hela zisizo na risiti wala control number.
3. DALADALA/TAX-UBER-BOLT Leo jumamosi wamejipanga kona zote za jiji, hakuna gari kupita bila kusimamishwa, pale magomeni kanisani wamekaba, oystebya mbuyuni wamebna, kwa azizi ali wamebana, wanasimamisha lila daladala, dereva ama utingo anashuka unamuona anenda nyuma ya gari ghafla anarudi mbio na gari inaondoka, utaskia konda akilalamika kwa dereva kwamba " nimebidi nimpe jala[elfu tano] maana jana hatukutoa: Baadae utaona anachukua kijitabu/diary na kuweka rekodi ya gari iliyotoa hiyo hela:
Kila mtu yupo kimya tunataka tufike ilipo NIGERIA KWA RUSHWA?
Hayo magari yameoza , magari yameoza.
Daladala ya Mwananyamala kwenda STESheni zimeoza kabisa na kunguni na hayafai hata kubebea mbolea lakininyapo katikati ya jiji na ukija nagari yako mpya kuomba TLB hupewi, ni hawa hawa wapendwa wetu ndio wanamiliki hizo daladala, well hawanyimwi kufanya biashra ila ni kinyume na maadili ya umma kutokana na kuwa na mgongano wa kimaslahi.
SAMIA alimtumbumbua mkurugenzi wa TTCL kwakuwa ana kampuni yenye tenda TTCL sasa ingependelewa, hili naomba SSH uingilie kati maana limesemwa sana.
4. KUVIZIA FINE BADALA YA KUELIMISHA. Trafiki badala ya kuzuia na kuelimisha wamegeuka watu wa maokoto. Haiwezekani say mtu umetoka mataa ya morroc unaendesha IST nyuma yako ipo gari kubwa na ipo spidi badala ya trafick kuzuia ajali yeye anasimamisha bila kujali aliye nyuma yako ako na spidi ya kiasi gani, ajali nyingi wanasababisha wao.
5. UHAMISHI Ufanyike mzunguko wa ma-trafikc, mfano kuna mmoja ni mwanamama mweusi bonge anaka mnazi mmoja ana kauli mbaya sana, aamishiwe kwa wakurya huko akafunzwe adabu.
Mataa ya st peters kuna mweupe hivi kijana, naye anajiona ni IGP na achunguzwe.