Baadhi ya trafic polisi wa Msata wanakula sana rushwa

Baadhi ya trafic polisi wa Msata wanakula sana rushwa

mkamandume

Senior Member
Joined
Dec 31, 2016
Posts
116
Reaction score
120
Inasikitisha sana kwa baadhi ya traffic polisi kukosa maadili mema ya kiutumishi. Ndugu zetu hawa jukumu lao ni kulinda raia na mali zao lakini baadhi yao hafanyanyi hivyo. Wamekuwa wanachukua rushwa pasipo woga. Imenitokea leo mitaa ya Bago karibu na Msata - Bagamoyo.

Nilisimamishwa na traffic kwa ajili ya speed ambayo ilikuwa 54 basi jamaa akaanza kumuambia kuwa nimeova speed hivyo lazima niandikiwe nilepe faini. Niliomba msamaha afande akanigomea na kunisisitizia lazima nilipe. Nikaona isiwe tabu wacha tu nitii sheria bila shuruti.

So alivyoona nimekaa kimya akaniambia nimpe pesa aniachie alisema "toa pesa uende zako" nikasema siwezi toa pesa wewe andika tuu basi akaniandikia kwa bahati mbaya akakosea namba ya gari akaandika namba ya gari nyingine ambapo nilijua hilo baada ya kuondoka katika tukio.....

Nilipo rudi nyumbani nikawaeleza jamaa kuhusu tukio hilo na wao walisema "baadhi ya trafic polisi wa Msata wanakula sana rushwa tena wanaomba uvunje tu sheria ya barabarani ili wafanye bargaining..." Tena kuna trafic mmoja anaitwa afande Bwile is one among the most corrupted officer. Rai yangu kwa IGP kufanya ufuatiliaji wa hawa watu kwa kuwa wanalidhalilisha Jeshi......na hawa traffic wa Msata wafuatulie.....
 
Mkuu si ungetoa tu hiyo ya kusafishia viatu ukaondoka na kumnusuru hata huyo gari yake imepewa deni? Huoni umechangia kumtia mtu kwenye deni ambako hausiki hata kidogo?
 
Mmmmm ila mkuu nawe ni sehemu ya tatizo hapa, huoni kuwa umefanya dhambi kwa asiyehusika kupigwa faini ambayo hakustahili? Sasa nenda TRA systems ikasaidie kumpata huyu aliyepigwa faini ili wewe uilipe hiyo faini.
 
Mmmmm ila mkuu nawe ni sehemu ya tatizo hapa, huoni kuwa umefanya dhambi kwa asiyehusika kupigwa faini ambayo hakustahili? Sasa nenda TRA systems ikasaidie kumpata huyu aliyepigwa faini ili wewe unlike hiyo faini.
Ukute limepaki zake juu ya mawe. Ila matrafiki tumewaendekeza sana, mbona mishahara yao inafanana na kada nyingine Serikalini lakini wao kutwa rushwa kama vile bila hiyo hawawezi kuishi!

Kuna wale wana mradi wao wa kukamata kila daladala JKT Mlalakuwa asubuhi na kutengeneza jam zisizo na msingi.
 
hata mlalamike vipi hiyo chain ya mgao wa yakubrashia ni ndefu ndio mana wanajiamini kuchukua mchana peupe
 
Back
Top Bottom