Jeshi takatifu linapokea rushwa labda virse versa
Kama gari bovu sheria si zipo? Kwanini kujishusha hadhi kazi yao kwa ajili ya sh 2000? Hata kama njaa polisi wamezidi. Na Kwanini usimamishe gari halafu unazunguka nyuma ya gari?
kama una chombo cha moto siku usahau leseni nyumbani uone jinsi utakavyokua unambembeleza achukue buku 5 ili akuachie uende bila kulipa faini
NB; Polisi sio wala rushwa ni wasumbufu tu rushwa ya buku jaribu kufanya utafiti kwenye halimashauri, miladi mbali mbali Bot nk kama hujatoroka nchini!
Nakuunga mkono, 5000 sio rushwa kabisa hyo ni kama kumpa pole ya usumbufu.
Rushwa ya kweli ipo humo idara nyeti, hela inaanzia kwa hosea hadi takukuru nzima
Lakini kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha na leo akidai pesa unayoiita ya usumbufu ipo siku atashirikiana na majambazi kufanya uhalifu. Wazungu wanasema two wrongs don't make it right. Kosa ni kosa hata kama linafanywa na wengi.