Polisi nchini Uingereza wazuru darasa la yoga baada ya kupokea taarifa ya mauaji ya halaiki

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,142
6,947
Polisi nchini Uingereza wamezuru kwenye darasa la yoga katikati ya jiji baada ya raia mmoja kutoa taarifa ya mauaji ya halaiki.

Maafisa walikimbilia mahali hapo huku ving’ora vya gari vikilia na kuwakuta washiriki wa darasa hilo wakitafakari kimyakimya.

Hoteli ya Seaside inayotazamana na Bahari ya Kaskazini huko Chapel St Leonards ilisema mwananchi mmoja aliyekuwa na wasiwasi alitoa taarifa ya tahadhari ya mauaji ya halaiki usiku wa Jumatano.

"Ikiwa mtu yeyote alisikia wingi wa ving'ora vya polisi katika Chapel St Leonards saa 9:30 usiku wa jana basi asiwe na mashaka kuhusu hali ya usalama," chapisho la Facebook lilisema.

"Walikuwa wakielekea kwenye chumba kimoja baada ya kupokea ripoti ya mauaji ya halaiki katika jengo letu, uhalisia ni kuwa baadhi ya watu walikuwa wamelala sakafuni, katika darasa la yoga kama sehemu ya kutafakari". Mgahawa huo mara kwa mara huwa na madarasa ya yoga jioni.

Polisi wa Lincolnshire walithibitisha kuwa taarifa hiyo ilitolewa na raia mmoja kwa nia njema.
 
Back
Top Bottom