Polisi na mahabusu wapoteza maisha ajalini Mwanza

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Watu wanne wakiwemo askari polisi wawili na mahabusu wawili - waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya kigaidi pamoja na mauaji, wamepoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea jana Jumatano jioni Aprili 27, 2022 katika Kijiji cha Ibanda barabara ya Geita-Sengerema.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la polisi aina ya Toyota Landcruise yenye namba za usajili PT 3798 lililokuwa likitokea mkoani Mwanza, kukata ‘sterling rod’ na kuhama kutoka upande wake na kwenda upande mwingine na kugongana na Lori aina ya Scania lenye tela namba. T.865 mali ya kampuni ya Nyanza Botling.

Ajali hiyo pia imejeruhi watu wanne na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita huku miili ya askari hao wawili ikihifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

Screenshots_2022-04-28-12-14-30.png
 
Watu wanne wakiwemo askari polisi wawili na mahabusu wawili wamepoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea jana Jumatano jioni Aprili 27, 2022 Kijiji cha Ibanda barabara ya Geita-Mwanza.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

View attachment 2203462
umemaliza kutuhabarisha au tusubir update
 
hili issue ya 'ku-overspeed + reckless driving' kwa madereva wa magari ya serikali limekuwa ni kaburi kwa wasio kuwa na hatia na kibaya Zaidi hakuna kiongozi yoyote anaye likemea, ona sasa yaani askari mzima ana overtake kwenye 'blind corner' sehem ambayo hajui mbele yake kuna anaenda kukutana na nini na siku ya mwisho jeshi la polisi wanamkamata na kumfungulia mashitaka aliye gongwa, pole kwa mahabusu/ watuhumiwa walio fariki ….
 
Watu wanne wakiwemo askari polisi wawili na mahabusu wawili wamepoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea jana Jumatano jioni Aprili 27, 2022 Kijiji cha Ibanda barabara ya Geita-Mwanza.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

View attachment 2203462
Kuna mtu miongoni mwa waliokuwemo alinusulika kwenye ajali hyo kweli??!
 
Pombe Kali zote ziandikwe:
"don't drink and drive.
Inapoteza kumbukumbu.
120kph inaonekana kama 20kph, hasa kama umefunga vioo vya gari"
 
Wao wanajua mwendo kasi na kutotii sheria uwa inalet mdhara kwa raia ila kwao ni muhali
 
Watu wanne wakiwemo askari polisi wawili na mahabusu wawili - waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya kigaidi pamoja na mauaji, wamepoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea jana Jumatano jioni Aprili 27, 2022 katika Kijiji cha Ibanda barabara ya Geita-Sengerema.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la polisi aina ya Toyota Landcruise yenye namba za usajili PT 3798 lililokuwa likitokea mkoani Mwanza, kukata ‘sterling rod’ na kuhama kutoka upande wake na kwenda upande mwingine na kugongana na Lori aina ya Scania lenye tela namba. T.865 mali ya kampuni ya Nyanza Botling.

Ajali hiyo pia imejeruhi watu wanne na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita huku miili ya askari hao wawili ikihifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

View attachment 2203582
tumesoma kuhusu kuhifadhiwa kwa miili ya askari wawili waliofariki,vipi kuhusu miili ya watuhumiwa wawili waliofariki katika ajili hiyo?
 
Back
Top Bottom