Tabora: Mathias Maganga, adaiwa kufia mahabusu ya polisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Na Abdallah Amiri – Igunga

Mathias Maganga (31) mkazi wa Kitongoji cha Kinambuga Kijiji cha Majengo, Kata ya Chabutwa, Tarafa ya Simbo Wilaya ya Igunga mkoani Tabora anadaiwa kufia Kituo kidogo cha Polisi Simbo.

Baba wa marehemu, Maganga Hanga (67) akizungumzia kifo cha mwanawe juzi, alisema Usiku wa Septemba Mosi mwaka huu alipokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema wakimjulisha kuwa mtoto wake, Mathias Maganga anashikiliwa Kituo cha polisi Simbo.

Alisema kwakuwa ilikuwa usiku hakuweza kwenda muda huo na kulipopambazuka alimtuma mwanawe mkubwa kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kujua sababu za kukamatwa kwa kijana wake.

“Mwanangu mkubwa alipofika Kituo cha Polisi Simbo aliambiwa mdogo wake yupo mahabusu lakini alipoomba kumuona Mkuu wa Kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Sajenti Omari alimkatalia bila kuambiwa hata kosa la nduguye.

“Hata hivyo baada ya kuhangaika sana hatiamaye aliruhusiwa kumdhamini ndugu yake kwa masharti

mawili ikiwa ni pamoja na barua kutoka kwenye uongozi anakoishi pamoja na Sh 70,000.”alisema baba mzazi wa marehemu.

Mzee Hanga aliongeza kuwa licha ya kukamilisha taratibu za barua walizoelezwa awali Mkuu huyo wa Kituo cha Simbo aligoma kutoa dhamana.

Alisema ilipofika siku ya tatu, yaani Septemba 3 mwaka huu bila mwanawe kupatiwa dhamana polisi walikusanyika ndugu pamoja na wanakijiji wengine na kwenda kituo hicho cha polisi Simbo kushughulikia suala hilo.

“Hata hivyo mkuu wa kituo aliendelea na msimamo wake wa kutukatalia kumuona kijana wetu wala kutoa dhamana.

“Lakini katika hali ambayo hatukutarajia, tukiwa nje mahabusu mmoja aliyekuwa ndani alichungulia dirishani atatunong’oneza tusiondoke mpaka tujue hatima ya suala hilo kwani mtoto wangu alishafariki tangu jana yake na yumo mule mahabusu.

“Huyo mahabusu aliyekuwa ndani alitwambia kwa kutunong’oneza, jamani mbaneni huyo mkuu wa kituo cha polisi kwani mtoto wenu tunaye humu mahabusu lakini amefariki tangu jana na ndiyo maana mkuu wa kituo anawapiga chenga.

Alisema baada ya kupata siri hiyo ndipo wanafamilia na wananchi walianza kupiga kelele na kupaza sauti wakishinikiza kumuona mtoto wao.

“Tukiwa pale tulisogezwa mbali na kituo na baadaye tulishuhudia gari likiwa hapo kituoni kabla ya kuondoka kwa kasi na kuelekea Kituo cha Afya Simbo kilichopo jirani na eneo hilo.

“Baada ya muda mfupi tuliitwa na mkuu wa kituo hicho cha polisi na kutueleza kuwa mtoto wangu amefariki dunia.”alisema Mzee Hanga.

Taarifa zaidi kutoka kwenye familia ya marehemu zilieleza kuwa mwili wa kijana huyo ulifanyiwa uchunguzi na kubaini kuwa aliuawa kwa kupigwa na kitu chenye ubutu.

Marehemu ameacha watoto wawili, Sabina Mathias (7) na Brighton Mathias (3) mke Furtunata Helman (30) ambaye ni mjamzito.

Kufuatia kifo hicho wazazi wa marehemu wamemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillius Wambura kufuatilia tukio hilo na kutoa fidia kwa familia ya marehemu ambayo imebaki bila kuwa na mtu wa kuitunza.

Mmoja wa wanakijiji wamelaani unyama uliofanywa kupitia kwa mkuu wa kituo cha Simbo hakipaswi kufumbiwa macho, huku wakiziomba taasisi zinazohusika na masuala ya haki jinai kukitupia macho kituo hicho pamoja na wialaya ya Igunga kwa ujumla.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Constatino Mbogambi alithibitisha kufariki kwa kijana huyo na kwamba alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika kituo cha afya Simbo.

“Alisema jeshi hilo wanamshikilia mtu mmoja kuhusika na tukio hilo sanjari na kumhamisha mkuu wa kituo hicho kutokana na kulalamikiwa sana na wananchi wa eneo hilo.
 
Kazi ya laana hii wazungu wanawapinga risasi watu weusi kisa ubaguzi wa rangi nanyi ngozi nyeusi tatizo nini kuwaua wenzenu bila sababu?polisi nchi hii wako juu ya sheria jamani mtu wa kuwakemea mimi binafsi sijawahi kuona mkuu wa kituo wilaya akifikishwa mahakamani na kufungwa
 
Huwa hawaishi milele!
 
Wamtafute huyo mkuu wa kituo wamuue kwa nmna yoyote Ile maana hyo kauli ya kuwa alifariiki akifanyiwa matibabu sio ya kweli la msingi wauze N'gombe wadeal nae wamezidi Hawa maku
 
Policcm wanapenda sana kulindana na kuteteana kwenye matukio ya aina hii. Mimi ndiyo maana hawa jamaa huwa sipendi hata kupishana nao tu njiani.
 
Siku ikikutana na polisi au ukafikishwa kituoni ukaambiwa toa chochote uachiwe huru wape baba vinginevyo banghe mfukoni mwako segerea miaka 30
Ningekuwa na mamlaka, hili jeshi ningelivunja na kuliunda upya. Maana halina tofauti na jeshi la Kikoloni nililofundishwa miaka hiyo.
 
Kazi ya laana hii wazungu wanawapinga risasi watu weusi kisa ubaguzi wa rangi nanyi ngozi nyeusi tatizo nini kuwaua wenzenu bila sababu?polisi nchi hii wako juu ya sheria jamani mtu wa kuwakemea mimi binafsi sijawahi kuona mkuu wa kituo wilaya akifikishwa mahakamani na kufungwa
Wazungu wapi hao
 
Kwa taarifa hii mkuu wa kituo ni tatizo
Mkuu wa kituo siyo tatizo. Narudia, mkuu wa kituo siyo tatizo. Tatizo ni sisi wananchi kwa umoja wetu kukubali kuiacha CCM iendelee kututawala. Hili nalo litapita, na siku mbili tatu, mwingine atauawa tena.
Socrates aliwahi kusema “The heaviest penalty for deciding to engage in politics is to be ruled by someone inferior to yourself”
 
Mwingine huyu 🤔
Screenshot_20230916-075249.png
 
Back
Top Bottom