BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limesema kuna ongezeko la vitendo vya ubakaji na ulawiti vinavyohusisha wanafunzi wenye umri chini ya miaka 18 wanaotendana ukatili huo wanapokuwa shuleni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama alibainisha hayo mjini hapo wakati alipochangia mada kuhusu vitendo vya ubakaji na lawiti vinavyoongezeka mkoani humu wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Morogoro (RCC).
yanaongezeka kwa kasi mkoani Morogoro, waathirika wakubwa wakiwa ni watoto wakiwamo wanafunzi wenye umri wa kuitwa watoto.
NIPASHE