Polisi Mbeya wafunga Makanisa 6 ya Ufufuo na Uzima

Polisi Mbeya wafunga Makanisa 6 ya Ufufuo na Uzima

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeyafunga makanisa sita ya Ufufuo na Uzima yaliyopo eneo la ZZK Mbalizi, Mtaa wa Mnadani Rujewa VWilaya ya Mbarali, Wilaya ya Chunya, Rungwe, Kyela na Jijini Mbeya.

Taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini Kuzaga amesema wameyafungia makanisa hayo Kufuatia tamko la serikali lililotolewa Juni 02, 2025 kupitia msajili wa jumuiya za kiraia nchini la kufunga makanisa ya Ufufuo na Uzima kutoendelea kutoa huduma katika matawi yake yote yaliyopo nchi nzima.

Sacp Kuzaga amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kufanya ufuatiliaji ili kubaini uwepo wa makanisa hayo na kuchukua hatua za kisheria.


#WasafiDigital
 
Kufuatia tamko la serikali lililotolewa Juni 02, 2025 kupitia msajili wa jumuiya za kiraia nchini la kufunga makanisa ya Ufufuo na Uzima kutoendelea kutoa huduma katika matawi yake yote yaliyopo nchi nzima, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya mnamo Juni 05, 2025 limeyafunga makanisa sita ya Ufufuo na Uzima yaliyopo eneo la ZZK Mbalizi, Mtaa wa Mnadani Rujewa Wilaya ya Mbarali, Wilaya ya Chunya, Rungwe, Kyela na Jijini Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kufanya ufuatiliaji ili kubaini uwepo wa makanisa hayo na kuchukua hatua za kisheria.

Sambamba na hayo, katika jitihada za kuzuia na kudhibiti ajali za barabarani Mkoa wa Mbeya kwa kipindi cha mwezi Mei, 2025 jumla ya makosa ya ukiukaji sheria za usalama barabarani 7,624 yalikamatwa kati ya hayo magari 6,613 na Pikipiki/Bajaji 1,011. Aidha, jumla ya magari 6,613 yalikaguliwa kabla ya kuanza safari na kwenye checkpoint za Polisi hasa zile zilizopo maeneo tete kama vile Inyala, Shamwengo na Iwambi.

Pia, jumla ya madereva 02 walifikishwa mahakamani kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani kwa kuendesha vyombo vya moto kwa uzembe na kuhatarisha maisha ya watumiaji wengine wa Barabara, Madereva 08 wamefungiwa leseni ya udereva kutokana na makosa hatarishi ikiwemo kusababisha ajali, mwendo kasi na kuyapita magari mengine katika maeneo yasiyoruhusu (Wrong Overtaking).

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa baadhi ya wananchi wanaojihusisha vitendo vya ukatili kuacha mara moja kwani havina nafasi kwenye jamii. Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawataka madereva kuheshimu na kufuata sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali na makosa mengine yanayosababishwa na uzembe, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya halitasita kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria madereva watakaobainika kuzembea.

Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
 
Back
Top Bottom