Polisi Mbeya wafunga Makanisa 6 ya Ufufuo na Uzima

Polisi Mbeya wafunga Makanisa 6 ya Ufufuo na Uzima

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeyafunga makanisa sita ya Ufufuo na Uzima yaliyopo eneo la ZZK Mbalizi, Mtaa wa Mnadani Rujewa VWilaya ya Mbarali, Wilaya ya Chunya, Rungwe, Kyela na Jijini Mbeya.

Taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini Kuzaga amesema wameyafungia makanisa hayo Kufuatia tamko la serikali lililotolewa Juni 02, 2025 kupitia msajili wa jumuiya za kiraia nchini la kufunga makanisa ya Ufufuo na Uzima kutoendelea kutoa huduma katika matawi yake yote yaliyopo nchi nzima.

Sacp Kuzaga amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kufanya ufuatiliaji ili kubaini uwepo wa makanisa hayo na kuchukua hatua za kisheria.


#WasafiDigital
Kamanda wa mbeya anajitafuta sana.
 
Kazi inaendelea kimyakimya.... Mikoa mingine pia mambo yamechemka, amri ya serikali sio ya kufanyia mchezo. Wachungaji tukalime sasa, ujanja ujanja unaelekea mwisho
Screenshot_20250606-182353.jpg
 
Vipi kama misikiti 6 ingefungwa pangekalika hapo mbeya kweli? TISS angalieni hili kwa hekima kubwa
Pangechimbika balaa. Ila uzuri wa wafuasi wa Kristo huwa hawana haraka z vita hupiganwa na Yeye mwenyewe. Ila hakika Dkt Samia katukwaza sana wana CCM. Ila uzuri siku akiondoka madarakani iko namna atakuja kujutia. Kama siyo yeye basi kizazi chake. Sikutegemea kabisa kama hakika angeshughulika na vitu vidogo namna hii badala ya kutafuta kura anapoteza kura. Uzuri hii mifumo ni mtifuano na mfumo wa Mungu siku zote hushinda. Ni kama Yesu Kristo alivyoteswa na kuuawa wale watesi walijiona wameshinda ila hawakujua atafufuka na kuwa na mamlaka makubwa zaidi.
 
Nawaza mfano siku Shekhe akienda kinyume na Serikali watafungia misikiti mwe kitawaka kuliko wanavyo fikilia 😁😁
 
Back
Top Bottom