Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,413
UkitazamaTV, kusikiliza radio ama kusoma magazeti ukakutana na habari inayolihusu jeshi letu la police lazima, habari hiyo lazima itakuwa ni ya kihalifu ama kutoa makatazo ama matamko.
Mimi sijawahi kuona kwenye media eti police wametoa msaada wa kitu ama huduma fulani kwa jamii kwa lengo la kujenga uhusiano mwema na general public. Mbona ikulu wanatoaga mbuzi, unga na michele walau mara moja moja (sio vibaya) kwa vituo vya watoto yatima wakati wa sikukuu na sherehe za kitaifa.
Hii inashindikana vipi kwa police? Kitengo na mahusiano ya jamii (PR) kipo kweli ndani ya jeshi letu la police? Kama kipo mbona sioni kama wanafanya kazi yao kwa ufanisi? Kama wanafanya kazi zao inavyopaswa wanafanyia wapi? Mbona hatuwaoni kwenye media (tv, magazeti na redio) kwa kuwa through media ndio njia pekee Police wanaweza kuitumia kujisafisha.
Mimi naona wakati ndio sasa kwa kamanda sirro kuboresha utendaji wa idara ya PR ya Police ama kuunda idara hiyo kama haipo ( mimi sijui kama ipo).
Nawasilisha.
==========
Follow my other threads;
Should "Mercy killing" be practiced in Tanzania?
Are spies made or born?
Bodi ya wahasibu N.B.A.A mnatutia aibu kimataifa, badilikeni sasa