Polisi: Kigwangalla hajampiga risasi mlinzi Jumanne

Koffi Annan

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
1,235
3,194
1685186297994.png

Polisi Mkoani Mwanza wametoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa mitandaoni kumhusu Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini na Mmiliki wa Kiwanda cha kuchakata Pamba kitwacho Mwalujo Ginery kilichopo Kijiji cha Mwalujo, Wilaya ya Kwimba, Hamisi Kingwangala kudaiwa kumpiga risasi Mlinzi wake Jumanne Omary Misango (66) katika mguu wa kulia, ambapo imebainika Jumanne hakupigwa risasi bali haliwaongopea Polisi.

RPC wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amesema taarifa za awali zinaonesha kulitokea wizi wa mali kiwandani ikiwemo Gear Motor HP Radio made 02, Electrical Motor 05 na nyaya za umeme @ Armored Cable Mita 25 vyote vikiwa na thamani ya Tsh 28,525,000.

“Mei 22, 2023 saa 11:00 jioni Kigwangala alifika kiwandani kwake na kukatokea majibizano kati yake na Mlinzi wake, Mlinzi huyo alitoa taarifa Polisi kuwa alishambuliwa na kupigwa risasi mguu wa kulia, Askari walifika eneo la tukio na kufanya ukaguzi ambapo hakukuonekena viashiria vyovyote vya matumizi ya silaha ya moto”

“Hata hivyo Jumanne alipewa PF3 na kwenda Hospitali ya Wilaya ya kwimba kwa uchunguzi wa kitabibu, Hamisi Kigwangala alihojiwa na kufunguliwa kesi ya shambulio na yupo nje kwa dhamana”

“Uchunguzi umebaini kuwa hakuna jeraha wala mvunjiko wowote wa mfupa katika mwili wa Jumanne na hivyo amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Afisa wa Polisi na kuzua taharuki kwa Jamii kuwa amepigwa risasi, upelelezi wa kesi hizo mbili unaendelea na utakapo kamilika Watuhumiwa wote wawili watafikishwa Mahakamani, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi”

Credit: MillardAyo
 
Kwamba huyo mtu ni mwendawazimu hadi akatoe taarfa za uongo polisi kuhusiana na mtu mwenye kufahamika kama kigwangala ?🤔🤔 Na hiyo pf3 alipewa ya kazi gani kama hakushambiliwa na kuumizwa?🤔🤔 Basi inabidi apimwe akili kama zimetimia sawa sawa, lakini ni kama kuna uvundo unafichwa hapa
 
Kwamba huyo mtu ni mwendawazimu hadi akatoe taarfa za uongo polisi kuhusiana na mtu mwenye kufahamika kama kigwangala ? Na hiyo pf3 alipewa ya kazi gani kama hakushambiliwa na kuumizwa? Basi inabidi apimwe akili kama zimetimia sawa sawa, lakini ni kama kuna uvundo unafichwa hapa
Taarifa za Majeruhi aliyepewa PF3 sizilitakiwa kutolewa na Dr aliye mtibu!? Au mi hapa hata sielewi!!
 
Kwanini serikali hii inatumia nguvu kubwa kuficha ujinga?

Waziri ameua mchepuko kwenye ajali ikafichwafichwa, Kigwangala ametandika mtu nayo inafichwafichwa!!

Arusha kuna ufisadi wa mabilioni ya pesa lakini mkuu wa mkoa analindwa na serikali!
Wewe kwa sasa hueleweki,kama ni mpinzani ama ni CCM. Nyie masalia ya mwendazake chagueni moja..mnajicontradict mnooo
 
Kwa nini serikali hii inatumia nguvu kubwa kuficha ujinga?

Waziri ameua mchepuko kwenye ajali ikafichwafichwa, Kigwangala ametandika mtu nayo inafichwafichwa!!

Arusha kuna ufisadi wa mabilioni ya pesa lakini mkuu wa mkoa analindwa na serikali!
Kwann waliompiga risasi Tundu Lissu mpala leo hawajakamatwa?

Yupo wapi Anzory gwanda na Ben sanane?

Kwann MAKONDA/ BASHITE alivamia kituo cha habari sote tukiona na hajachukulia hatua yyte?

Kwann waliompiga risasi Akwilin hawajachukuliwa hatua yyte mpaka leo?

Kwann SAA BAYA aliwakata watu masikio taarifa zilifika kwa magufuli na aliachwa aendelee kutesa watu?

Haya mambo wewe uliyatetea na kuwatukana watu. Huu uchungu unaoupata leo unatoka wqpi? Wale waliouwawa enzi za magufuli hawakuwa watu?

Kaa kwa kutulia SUKUMA GANG KAMPIGA CHUMA SUKUMA GANG WEWE UNAUMIA? TUSEME AMEJIPIGA RISASI MWENYEWE
 
RPC Mtafungwa wa Mwanza amesema kijana Omary aliyedai alipigwa risasi mguuni na Dr Kigwangalla alipewa PF 3 na baada ya kufika hospital Uchunguzi wa kitabibu imeonesha hana jereha lolote na mfupa haujavunjika

Hivyo Omary anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani

Aidha Uchunguzi wa Kesi zote mbili bado unaendelea na Dr Kigwangalla yuko nje kwa dhamana, amesema Kamanda Mutafungwa

Source: Ayo tv
 
Sasa kama huyo Kigwangala hajamdhuru mlinzi wake, kwa nini na yeye anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika?
Police wanataka kulazimisha bao la Mkono! Huyo Mzee wanaharakati wa Mwanza wamsaidie apate haki yake,la sivyo kibao kitamgeukia maana na yeye tayari kesha kua mshitakiwa ghafla!! Rushwa ni adui wa haki siku zote!!
 
RPC Mtafungwa wa Mwanza amesema kijana Omary aliyedai alipigwa risasi mguuni na Dr Kigwangalla alipewa PF 3 na baada ya kufika hospital Uchunguzi wa kitabibu imeonesha hana jereha lolote na mfupa haujavunjika....
Hiyo RUSHWA aliyopokea RPC wa Mwanza kutoka kwa Kigwangalla itamtokea puani. Nakuonya RPC Mutafungwa kuwa UTAFUNGWA, be careful.

Wenzio hupokea Rushwa kwa akili sana lakini ya kwako umepokea kizembe
 
Back
Top Bottom