Ni jambo la kushangaza sana kwamba habari za matukio ya aina hii zimekuwa kama wimbo mwororo katika masikio ya wananchi wa Tanzania, hadi lini tutaendelea kusikia visa hivi vya kusikitisha vinavyofanywa na watu tuliowapa dhamana ya kuhakikisha usalama wetu, huku tukiwalipa kwa kodi zetu, ni lini mwisho wa kusikia hizi cold blood killings.,viongozi wa jeshi la polisi hajagundua tu kuwa ongezeko la matukio haya ni ishara kuwa kuna tatizo kubwa sana ndani ya jeshi hilo?.,yawezekana kwamba si polisi wote lakini miongoni mwao wapo ambao hawakustahili kuwa polisi.,hebu kina Said Mwema wafunguke macho jamani, kulea uovu ndani ya chombo nyeti kama hicho kuna siku yatatokea makubwa zaidi, ni bora kuziba ufa ili baadae usijejikuta unajenga ukuta mzima.