Kichwa Maji wewe RITZ, tafuta kalavat lakujifichawewe ni Jini?
Ningeshauri huyo prince Charles ahairishe hiyo ziara yake ya Arusha..Aende akatembee Kilombero Wakulima wa Miwa na Mpunga..
asante Regia
ha ha ha, hajui kilimo huyo Regia, amekulia katika jumba la dhahabu kila kona.Ningeshauri huyo prince Charles ahairishe hiyo ziara yake ya Arusha..Aende akatembee Kilombero Wakulima wa Miwa na Mpunga..
Jamani bado hali ni tete mkoani Arusha kuliko inavyodhaniwa na wengi.
Nimeweza kutumia uzoefu wangu na kuingia Police Central kuna ulinzi mkali polisi zaidi ya 70 wenye silaha na wengine wanaingia na kutoka.
Hali ni tete sana hakuna ruhusa mtu kuingia eneo la Police Central kwa namna yoyote ile hata kama una shida gani unazuiliwa getini na askari wenye silaha tayari kwa lolote na kama una shida ya kipolisi unaambiwa nenda kwenye vituo vingine vidogo utahudumiwa huko.
Nimeweza kupenya na kuongea na baadhi ya maofisa waandamizi akiwemo Zuberi mwenyewe ambaye alikuwa ameenea uwanjani akiwapanga mapolisi na kuonekana makini na kila kona kwa umakini na tahadhari kubwa kabisa.
Kwa hali ilivyo hapa kaunta hakuna kazi nyingi kama ilivyo kawaida bali
ni nyimbo za Taifa Shange nderemo na vifijo na vigelele vya wanawake walioko mahabusu huku wakimaliza nyimbo na kunza upya kwa kauli mbiu ya Peoples Power kiasi ambacho hata baadhi ya askari wanaonekana kujaribiwa ila majukumu yanawabana lakini wanaonekana kuhamasika na nyimbo hizo.
Nimetoka na kujaribu kutembea baadhi ya mitaa FFU wanazunguka na mapikipiki na wengine kwa miguu wakiingia kila uchochoro kuangalia kama kuna makundi ya vijana na kuyatawanya na inavyoonekana watu wamenyamaza lakini akili zao bado hazijatulia na watakuja na maamuzi mapya ambayo yanaweza kuigharimu serikali na Amani yetu kwa ujumla.
Mkuu Derimto.
Kadhia yote hii imesabishwa na mtu mmoja mpenda sifa za kitoto kibaya zaidi viongozi wake badala ya kutumia akili wakajiingiza kichwa kichwa.
Ningeshauri huyo prince Charles ahairishe hiyo ziara yake ya Arusha..Aende akatembee Kilombero Wakulima wa Miwa na Mpunga..
Siamini kama haya maneno yanatoka kwa mh. mbunge!Ningeshauri huyo prince Charles ahairishe hiyo ziara yake ya Arusha..Aende akatembee Kilombero Wakulima wa Miwa na Mpunga..
vipi?mbona nasikia baadhi ya viongozi wamekamatwa?