Polisi aliyekataa Rushwa ya milioni 10 na kupandishwa cheo apokonywa vyeo vyote, amlilia Rais Samia

Katika Hali ya kushangaza Askari polisi ,Meshack Laizer aliyepandishwa cheo Na IGP Simon Siro Disemba 22,2019 jiji Arusha Kwa kukataa Rushwa ya sh,milioni kumi ,amevuliwa vyeo vyote rasimi baada ya kukataa kwenda kusomea cheo hicho, CCP Moshi.


Meshack alipanda cheo kutoka sajenti Hadi staffsajenti Kutokana na jitihada zake za kupambana na Rushwa baada ya kukataa burungutu la sh, milioni 10.


Askari hiyo ambaye Kwa Sasa ni askari wa kawaida mwenye cheo Cha Koplo akiwa mkuu wa kituo kidogo Cha polisi Kijenge amethibitisha kuvuliwa vyeo vyote baada ya kupokea barua , desemba 12,2021 ikimtaarifu kwamba umevuliwa vyeovyote tangu novemba 26 mwaka huu.


Alisema katika utendaji wake wa kazi jijini Arusha,amewahi kukataa Rushwa ya sh, 250,000 kutoka kwa raia mmoja aliyemkuta akiendesha kiwanda bubu Cha kutengeneza vichwa vya majiko ya gesi, tukio lililotolewa Julai 3 mwaka 2020.


Pia askari huyo alidai kukaa Rushwa ya sh, 150,000 na sh,milioni 10 Kwa watu waliotaka kumhonga .


Alisema matukio hayo yalimpatia sifa ya utendaji Kazi uliotukuka ndani ya jeshi Hilo na kupelekea,polisi Arusha, Takukuru pamoja na IGP Siro kumwandikia barua za kumpongeza .


PC Meshack alipandishwa cheo na IGP Siro mwaka 2019 kupitia Kwa aliyekuwa RPC Arusha, Marehemu Jonathan Shana baada ya kukataa Rushwa ya sh, milioni 10 kutoka Kwa kampuni Moja ya mafuta baada ya kukamata gari la Kampuni hiyo likiuza mafuta mtaani bila kufuata utaratibu.


Askari huyo ambaye alipendeke zwa kupanda cheo mwaka huu ,kutoka staff sajenti na kuwa SM/RSM amejikuta akishushwa vyeo vyote na kuwa askari wa kawaida jambo ambalo amemwomba Rais Samia na waziri wa mambo ya ndani George Simbachawene kumsaidia .


Hata hivyo alidai kwamba licha ya kupandishwa cheo mwaka 2019 ,hakuwahi kuongezewa mshahara kwani malipo yake yalikuwa ni ya askari wa kawaida.
















View attachment 2053636
Alistahili kushushwa cheo. Kama hakutii mamlaka, alitegemea kupata nini hasa, kuweka rekodi nyingine?
 
Hapo ujue boss ndio amekula offer ya $5000 au zaidi.
Sasa kama haki inapindishwa na walio juu huku chini ufanye nini?

Kuna afisa uhamiaji akimkamata Mchina hana vibali , Mchina alimpa $5,000 wayamalize. Afisa akazikataa, alimuweka ndani. Kesho yake boss wake alimtoa Mchina. Sasa si kheri angejilia $5,000 zake.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Waziri2025 , kwanza asante kwa taarifa hii, itafika kunako, ila kwanza lets put the records clear.
Sii kweli kuwa amevuliwa vyeo vyote na kubaki askari wa kawaida, bali amevuliwa vyeo alivyopandishwa fasta na kubaki na rank aliyokuwa nayo kabla ya kupandishwa.
Askari wa kawaida ni yule asiye na cheo chochote, Coplo ni mbavu mbili, ni cheo!. Hivyo heading kuwa amevuliwa vyeo vyote sii taarifa sahihi, bali amevuliwa vyeo vya kupwa bure bure na kurejeshewa kile cheo chake cha zamani!.

Kwenye polisi, majeshi na askari wetu kuna vyeo vya aina 4.
  1. Junior NCO's,- private, la corplo na corploKoplo wa Polisi(cpl)Koplo Usu
    Konstebo wa Polisi(pc)
  2. Senior NCO's - Sergeant, Staff Sergeant na Warrant officer 1&2/Sir Major (kolokolo) Sajini Meja wa polisi(rsm), Stesheni Sajini wa Polisi(s/sgt) na Sajini wa Polisi(sgt)
  3. Junior COs- Maofisa wadogo Mrakibu Msaidizi wa Polisi(ASP), Mkaguzi wa Polisi(Insp)Mkaguzi Msaidizi wa Polisi(A/Insp)
  4. Senior Offices, Naibu Kamishina wa Polisi(DCP), Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP), Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Mrakibu Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SSP), Mrakibu wa Polisi(SP)
  5. Staff Officers- Kamishina wa Polisi(CP), Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi(DIGP), Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP)
Kwa vyeo vyote vya chini, ili askari kupanda cheo kimoja kwenda kingine ni lazima ahudhurie kozi. Hivi vyeo vya kupeana tuu, hufuatiwa na aliyepewa kuhudhuria kozi.
Vyeo vya staff officers sio vyeo vya merits ni vyeo vya hisani ya CinC.

Hivyo huyo askari, alipaswa baada ya kupata cheo kwa sadakalawe, he had to deserve kwa kwenda kozi, vinginevyo anapokonywa!.

Nimesoma mahali kuwa alikuwa Sajini, sasa ni koplo, huko ni kushushwa cheo, aseme vuzuri tuu, kuna kosa amefanya kustahili kushushwa cheo, hivyo awe muwazi tuu.
P

Mkuu uneeleza vema Kabisa...
Ila Mtoa mada kashasema jamaa alikataa Kwenda course then akashushwa cheo..
Its so simple..
Mi nimemuelewa mtoa mada hivyo...
Sasa kama alipandishwa then akaambiwa cheo hiki tunakupa Nafasi ya Kwenda Kukisomea halafu unagoma si unashushwa tuu.
 
Police bado wana mfumo mbovu sana,unasemaje umempandisha mtu cheo kwa utendaji wake alafu unamlazimisha akasomee hicho cheo la sivyo unamshusha.Ni bora wangesema wamempa nafasi ya kwenda kusomea cheo flani.
 
Huyu police kawahi nisaidia na ni mtu mwema, maana ma police wengi ni waovu, Simbachawene na Rais wamsaidie huyu police kupata haki yake aisee
 
naye mjinga tu....unapandishwa cheo na unapewa opportunity ya kwenda kusoma. Hakujua kuwa pengine akimaliza kusoma atapanda zaidi ya staff sajent?
Huyo jamaa kama ni memwelewa atakuwa ameonewa.
Huyo jamaa cheo alipandishwa kutokana na kuonyesha ujasiri huo wa kukataa rushwa sasa iweje akubali kwenda kozi na wenzake wa kawaida ambao hawajaonyesha maajabu yeyote hivyo ili waweze kupanda cheo ni lazima waende darasani.
Kwa uelewa wangu kwenye majeshi mtu akifanyajambo la ushujaa na ikaamriwa apandishwe cheo kutokana na ushujaa huo basi kama kuna wenzake waliokuwa depo moja anakuwa ameshawaacha, hao wenzake wenyewe kupata hicho cheo ni hadi waende kozi ,huyo jamaa aliyepandishwa cheo kwa ushujaa hatatakiwa kwenda hiyo kozi.
Huyo jamaa imekuwaje wamlazimishe kwenda kozi ya cheo ambacho ameshakipata.
Mimi ndivyo nilivyoelewa kesi ya huyo jamaa anyway labda kuna mambo mengine yaliyojificha.
Halafu nyie maaskari polisi utendaji wenu ni mbovu sana mnaonea sana wananchi kiasi kwamba hata mkileta malalamiko yenu huku kwwnye jamii kwamba mmeonewa na mabosi wenu wananchi hawasikitiki .
Achaneni na utendaji mbovu wa kuonea wananchi mnasababisha kuchukiwa sana na jamii
 
Kwa vyeo vyote vya chini, ili askari kupanda cheo kimoja kwenda kingine ni lazima ahudhurie kozi. Hivi vyeo vya kupeana tuu, hufuatiwa na aliyepewa kuhudhuria kozi.
Vyeo vya staff officers sio vyeo vya merits ni vyeo vya hisani ya CinC.

Hivyo huyo askari, alipaswa baada ya kupata cheo kwa sadakalawe, he had to deserve kwa kwenda kozi, vinginevyo

Huyo askari hajapewa cheo bure.
Kapewa cheo kutokana na kutenda kitendo cha ushujaa na sio sadakalawe kama unavyotaka kutuaminisha.
Huyo mtu atapelekwaje kozi na wenzake wa kawaida ambao hawajafanya jambo la ujasiri?
mfano mwanafunzi wa darasa fulani mf la 1 ameonekana very bright akarushwa darasa itambidi arudi kufanya mtihani na wale wenzake aliokwisha waacha?
 
Umeandika kisiasa sana
Angeeleza kwanini ameshushwa cheo maana taarifa ya kiofisi kwa mujibu wa PGO anayo.
Sasa kama alifanya utovu wa nidhamu kwann asiadhibiwe? Atoe sababu alizopewa
Sababu ni hii hapa chini. Sasa yeye alitaka apewe cheo huku amegoma kwenda chuoni?
amevuliwa vyeo vyote rasimi baada ya kukataa kwenda kusomea cheo hicho, CCP Moshi.
 
Huyu police kawahi nisaidia na ni mtu mwema, maana ma police wengi ni waovu, Simbachawene na Rais wamsaidie huyu police kupata haki yake aisee
Ila Arusha sijui kwanini? Kama pale central police yule Gwakisa sio mtenda haki. Yule na OCD wahamishwe. Kwa pamoja wanasaidia matajiri kipokonya haki za wananchi maskini. Huo ndio ukweli. Wahamishwe
 
Kwa waliyoyafanya Akina Kingai, Mahita, Goodluck, Swai na Jumanne kwenye kesi ya Mh. Mbowe na wenzake, basi siwezi kumuonea huruma Askari yoyote WA jeshi la police. We must draw our conclusion from particular to general.
 
Umeandika kisiasa sana
Angeeleza kwanini ameshushwa cheo maana taarifa ya kiofisi kwa mujibu wa PGO anayo.
Sasa kama alifanya utovu wa nidhamu kwann asiadhibiwe? Atoe sababu alizopewa
NI kweli lakini pia umeamua kukwepa kabisa kuizungumzia issue ya cheo chake since mwaka 2019 todate kwamba kilikua bila mshahara? Hiyo paragraphy hukuiona kabisa? Anywa, hi nchi ngumu sana, asikwambie mtu
 
Mara amevuliwa vyeo vyote, mara kabakia na ukoplo, kwani ukoplo hauna nembo ya cheo?
Kuhusu kutopanda mshahara hili lililetwa na Magufuli, liliathiri taasisi nyingi au karibu zote mpaka Samia alipotukumbuka kuanzia June 2021.
Kuhusu kukataa kwenda kusoma huo ni ujeuri , alipaswa kufukuzwa kazi kabisa.
Aliandila barua ngapi kudai stahiki zake kama ushahidi?, Nakala anazo?
 
Back
Top Bottom