Polisi aliyekataa Rushwa ya milioni 10 na kupandishwa cheo apokonywa vyeo vyote, amlilia Rais Samia

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Katika Hali ya kushangaza Askari polisi ,Meshack Laizer aliyepandishwa cheo Na IGP Simon Siro Disemba 22,2019 jiji Arusha Kwa kukataa Rushwa ya sh,milioni kumi ,amevuliwa vyeo vyote rasimi baada ya kukataa kwenda kusomea cheo hicho, CCP Moshi.

Meshack alipanda cheo kutoka sajenti Hadi staffsajenti Kutokana na jitihada zake za kupambana na Rushwa baada ya kukataa burungutu la sh, milioni 10.

Askari hiyo ambaye Kwa Sasa ni askari wa kawaida mwenye cheo Cha Koplo akiwa mkuu wa kituo kidogo Cha polisi Kijenge amethibitisha kuvuliwa vyeo vyote baada ya kupokea barua , desemba 12,2021 ikimtaarifu kwamba umevuliwa vyeovyote tangu novemba 26 mwaka huu.

Alisema katika utendaji wake wa kazi jijini Arusha,amewahi kukataa Rushwa ya sh, 250,000 kutoka kwa raia mmoja aliyemkuta akiendesha kiwanda bubu Cha kutengeneza vichwa vya majiko ya gesi, tukio lililotolewa Julai 3 mwaka 2020.

Pia askari huyo alidai kukaa Rushwa ya sh, 150,000 na sh,milioni 10 Kwa watu waliotaka kumhonga .

Alisema matukio hayo yalimpatia sifa ya utendaji Kazi uliotukuka ndani ya jeshi Hilo na kupelekea,polisi Arusha, Takukuru pamoja na IGP Siro kumwandikia barua za kumpongeza .

PC Meshack alipandishwa cheo na IGP Siro mwaka 2019 kupitia Kwa aliyekuwa RPC Arusha, Marehemu Jonathan Shana baada ya kukataa Rushwa ya sh, milioni 10 kutoka Kwa kampuni Moja ya mafuta baada ya kukamata gari la Kampuni hiyo likiuza mafuta mtaani bila kufuata utaratibu.

Askari huyo ambaye alipendeke zwa kupanda cheo mwaka huu ,kutoka staff sajenti na kuwa SM/RSM amejikuta akishushwa vyeo vyote na kuwa askari wa kawaida jambo ambalo amemwomba Rais Samia na waziri wa mambo ya ndani George Simbachawene kumsaidia .

Hata hivyo alidai kwamba licha ya kupandishwa cheo mwaka 2019 ,hakuwahi kuongezewa mshahara kwani malipo yake yalikuwa ni ya askari wa kawaida.

images%20(22).jpg
 
Sijui Ni Mimi TU?

Yaan Sijawai kabisa kujiskia kuwaonea huruma polisi wa nchi hii wanapopatwa na matatizo

ukiona unaonea wengine huruma halafu polisi huwaonei wakikutwa na majanga,ujue huna utu ila ni unafiki tu uko nao unaouita huruma.

iko hivi,kila binaadam ana sehemu yake ya udhaifu inayomtofautisha na viumbe wengine,ndio maana pamoja na kumchukia mende,kuna mazingira ukimkuta huwezi kumuua.
wewe huruma yako haina kipimo cha kusema huyu hapana,ukweli ni kwamba huna hiyo huruma ila unakosa sababu tu ya kuwawekea kisirani na wengine.

ndio maana mtu timamu wa afya ya akili hubaki kimya ,maana anajua polisi anafikwa na majanga kama binaadamu mwingine sio kwa sababu ya upolisi wake.
 
unawezakuta jamaa alichunguzwa akakutwa nje ya zile sifa zilizofanya apewe cheo,alikuwa na makamba kamba mengi sana.

ujue polisi ukiona kakataa hela basi jua kuna hela nyingine nyingi kachukua,
japo sijakataa malaika pia wapo PT na wanapaa kabisa kama kingai.
 
ukiona unaonea wengine huruma halafu polisi huwaonei wakikutwa na majanga,ujue huna utu ila ni unafiki tu uko nao unaouita huruma.

iko hivi,kila binaadam ana sehemu yake ya udhaifu inayomtofautisha na viumbe wengine,ndio maana pamoja na kumchukia mende,kuna mazingira ukimkuta huwezi kumuua.
wewe huruma yako haina kipimo cha kusema huyu hapana,ukweli ni kwamba huna hiyo huruma ila unakosa sababu tu ya kuwawekea kisirani na wengine.

ndio maana mtu timamu wa afya ya akili hubaki kimya ,maana anajua polisi anafikwa na majanga kama binaadamu mwingine sio kwa sababu ya upolisi wake.
Police wa Tanzania sio wa kuhurumia siku moja nmeshidudia wanamuonea binti mmoja bila kosa kisa mmoja wao alimtaka aka kataa wakamgezia kesi ya umalaya anajiuza
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom