Polisi akatwa mkono katika ugomvi wa kugombea mwanamke

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, linawashikilia watu wawili wakazi wa Mtaa wa Nkende mjini Tarime wakidaiwa kumkata mkono Mkaguzi wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana-River cha nchini Kenya, James Mnuve (50), wakati wakimgombania mwanamke.

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kukatwa mkono Mkaguzi huyo wa Polisi wa nchini Kenya.
Mwaibambe alidai kuwa tukio hilo lilitokea Julai 13 mchana katika mtaa wa Nkende mjini Tarime ambapo vijana hao walitenda kosa hilo.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Michael Omahe, anayedaiwa kumtorosha mwanamke huyo, Anne Njeri, kutoka Kenya na kumleta Tanzania kisha kuishi naye kinyumba huku akisaidiana na rafiki yake, Daniel Onchiri.

“Mwanamke huyo (Njeri) anadaiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi pia na askari James Mnuve na walikuwa wakiishi huko Tana River nchini Kenya, baada ya kuondoka, Julai 13 mchana askari huyo alimfuatilia kutoka Kenya hadi Mtaa wa Nkende, Tarime alipokuwa anaishi na kijana aliyemtorosha (Michael Omahe),” alisema Kamanda.

Akaongeza, “Alipofika Mtaa wa Nkende alimkuta Michael, pamoja na rafiki yake huyo wakiwa na mwanamke huyo na hapo ndipo ugomvi ulipoanza kwani askari James alitaka kuondoka na mwanamke huyo na zikazuka vurugu kubwa na kusababisha Mnuve kukatwa kwa kutumia panga.”

Aidha Kamanada huyo alisema kuwa, “Jeshi la Polisi tulifika kwenye eneo la tukio mapema na kuweza kuwakamata watuhumiwa wote watatu; Marandi, Ochiri na mwanamke huyo na kisha tukawahoji kabla ya kuwafikisha mahakamani huku majeruhi akiwa amepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa matibabu.”

Majeruhi James anadai kuwa yeye ni Inspekta wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana River nchini Kenya na mwanamke huyo, Njeri Wanjoi, ni mke wake.

Chanzo:
Mpekuzi
 
Hivi kwa nini polisi wetu mara kibao wanahusika na ugomvi wa wanawake hadi kuuana??
Mwaka huu tu nimesikia case kama hivi.
1.huko tanga polisi alipigana na mkewe akamuua kisa mapenzi. Na huyo polisi akatokomea.
2. Hata wiki haijaisha kuna mshkaji huko mwanza alimsaprise demu wake kumtembelea all the way from dsm, hatimaye suprise ikawa sapraiz. Wakapigana polisi akamuua mshkaji.
3. Hii tena ya huko rorya ni mupya...
Swali je:? Polisi nyie ndio mnazijua papuchi vizuriiii??????
 
Neno (nkende ) kwa kilugha chetu ni tusi kabisa, ila pole yake jamaa mke wa mtu anauma.
 
Back
Top Bottom