Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 16,018
- 23,357
Laghai za kitandani huwapumbaza watu na kujiona wanapendwa.Mkwepa Kodi,
Labda mimi na wewe tupo tofauti na wanaume wengine.
Mwanamke kama huyo, nikishajua yupo hai na ana mwanaume mwingine, siwezi kusumbua nafsi yangu kumtafuta.
Kumbe kuna sanaa za mapenzi hutumiwa kuwahadaa mabwege.
Unatenda hadi mtu anakulilia kabisa na unahakikisha anatoa chozi la maji unaridhika kwamba umemmudu.
Kumbe chozi lile lilikuwa ni kwa ajili ya raha ya kushiba ugali wa kulumangila, wewe ukiwa umegeuzwa picha ya samaki, unatumika na haupendwi.
Na katika kulialia kwake kule saazingine anaweza akamtaja kwa jina kabisa jamaa yake na ukiachwa kwenye ujinga wako wa kudhani midadi na maruweruwe ya kuiona jehanamu kwa kuvunja amri ya6.
Kwanini sasa akikutoroka, usimfuate huko alikotoroshewa na kuvuka mipaka bila pass na kuishia kulambwa mapanga?
Tatizo la mapenzi, tangia waasisi Adamu na Eva, hayajawahi 'kubalansi'. Ukiona mshirika wako unampenda sana, yaani ile sana kabisa, elewa yeye anakuona wa kawaida ama hakupendi na mnaishi naye jwa manufaa f'lan. Na ukiona mtu haumpendi lakini yeye anakufuatafuata, elewa anakupenda kwa dhati, vuta upendo wako kwake ili umpende. Maana huyo aweza kuwa sahihi kwako.
Kwa hiyo huyo PK kanaswa kwa kuona kwamba kanaswa kijinga, lakini kwa wataalamu wa saikolojia wanaweza wakaeleza vinginevyo.