Polepole: Nipo Namibia, kila mtu anamuulizia Magufuli

Sioni cha ajabu kumuulizia Magu mana ndio rais na boss wako kwa sasa. Ulitaka wamuulizie Kikwete?
 
View attachment 581718
Hii ni twitter ya "propagandist" wa CCM,anasema huko Namibia kila akipita watu wanamuulizia JPM,JPM yaani kila kona ni Magufuli tu.

Polepole anasema Magufuli karudisha heshima ya Taifa letu,sasa sijui anataka kusema hii heshima inayorudishwa na JPM ilipotezwa na kina nani?

Kwa watu wa "logic" watakubaliana kuwa Polepole anamaanisha Ma-Rais wengine waliotangulia kuanzia Mwinyi mpaka Jakaya waliipoteza heshima ya nchi hii,sasa huyu aliyepo anajitahidi kurudisha pale tulipovuliwa nguo kimataifa kama Taifa.

Anasahau kuwa hao waliopoteza heshima ya Taifa ni wa chama hichohicho ambacho amekuwa anasema kimeliletea Taifa heshima kwa miaka 50 toka Uhuru.Hawa wanasiasa huwa wanajichanganya sana
Mtu akikosea akajisahihisha anafaa kupongezwa, usiongee kwa lugha ya mvinyo uliochachwa .....vijana epukeni sana homa ya negative perception, (naysaysm) haimaanishi nakubaliana na osho juu ya positive philosophy kwa asilimia mia ila turuhusu bongo zetu zifanye kazi....je magufuli katika sekta ya umeme hujaona mabadiliko? Je nidhamu ya utumishi wa uma haujaiona? Watafute wote wale wa kangamoja ndembendembe laki si pesa waambie waongee hayo maneno ndio utajua alichofanya magufuli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni rahisi kusifia rangi ya nyoka kama hajakuuma, tunaojua maumivu ya mtu wenu mnayempamba kila uchao wala siyo mafisadi maana wengi nawajua na wanaendelea na maisha ya anasa tena wakiwa ndani ya CCM, lakini tunaoumia ni sisi nyasi (Watanzania wa hali ya chini) tunaokosa dawa hospitali huku mkinunua ndege za maonyesho, tusiopandishiwa mishahara kwa miaka 3 huku mkihubiri kuondoa mishahara hewa na watumishi hewa ambao hatuoni impact yake.

Tunaoumia ni sisi ambao watoto wetu wanakosa mikopo ya elimu ya juu na kuishia kulandalanda mitaani tukiomba misaada ya wasamaria, tunaoumia ni sisi tuliosoma kwa mikopo wakati wa JK tukiahidiwa makato madogo tutakapopata ajira lakini Leo kwa tunakatwa asilimia 15 kwa ubabe hadi take home inabaki 48,000/- kinyume cha kanuni za utumishi. Msitake tuongee mengi jamani, ni maumivu kila mahali!!

ACHA nikae KIMYA...!
Pole Bila bila, i feel you.
 
Kiuchumi Namibia wameizidi Tanzania?????naomba jibu

sent from my iPhone 7 nimeinunua SAPNA pale Posta mtaa SAMORA
 
Kila akipita watu wanamuulizia magufuli......wamejuaje kama huyu ndio polepole

sent from my iPhone 7 nimeinunua SAPNA pale Posta mtaa SAMORA
 
Haiwezekani ukakutana na kila mtu, haiwezekani zaidi kila mtu aulize swali moja, inawezekana umekutana na mmoja au wawili uliowafanya wakufahamu kwamba wewe ni katibu Mwenezi hivyo wakakuulizia kuhusu mwenyekiti wako.... Pengine angekuwepo Roma wangemuuliza kuhusu Diamond

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijuavyo mimi, ukifanya kosa na ukajirekebisha matokeo ni kujijengea heshima. Ukisubiri polisi, mahakama na jela utajiletea majina ya hovyo na kujipotezea heshima yako. Vivyo hivyo Dokta hajasubiri makosa ya CCM yarekebishwe na chama kingine. Na huo ndio uungwana, ukinya pembeni hata kama una kinyaa cha first class, we safisha tu. Usisubiri wakaanza kutaka jua nani alikuwa wa mwisho.

Nionavyo mimi: Sasa hata chama kingine kikashika dola ni sawa tu maana Dokta kwa sehemu kubwa ameset the minimum expected level of performance. Na hii inawachanganya wengi sana. In short wamekaa!

Sent from my VFD 600 using JamiiForums mobile app
 
Mh Magufuli ni Raisi bora kupata kutokea ktk taifa hili tunaweza mchukulia simple tu kwa vile tupo nae interior apa , Lakini ktk rank ya Maraisi bora apa Africa huwezi kumtoa kwenye top 10 within 54 countries
 
Polepole anaturingishia kwamba kapanda ndege ya bure mpaka Namibia. Hongera kwa kupanda ndege dogo
 
Mh Magufuli ni Raisi bora kupata kutokea ktk taifa hili tunaweza mchukulia simple tu kwa vile tupo nae interior apa , Lakini ktk rank ya Maraisi bora apa Africa huwezi kumtoa kwenye top 10 within 54 countries
Kwalipi au mbwembwe za majukwaani
Yani watu kama nyie nazani hata elimu kichwan akuna nyau ww

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli mnamdharau nyie tu ila katika africa akigombea urais kwa asilimia 50 ya nchi za africa atashinda kwa kishindo. Wenye dharau ni wale waliokatiwa mirija na nyumbu, tena baadhi sio wote.

Udhaifu wa rais wangu ni mdogo sana na hauna madhara makubwa kwa vile bado anajifunza polepole kuwa mwanasiasa, hapo kale hakuijua siasa yeye ni mtu wa kazi tu habari za taarabu majukwaani hana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pushapu jee?
 
Umenena vema mkuu. Marais wengine waliomtangulia waliipotezea sifa nchi hii. Mbona hata Mwinyi alikiri hili?

JPM anarudisha heshima ya nchi hii.
Anachosema Polepole ni kweli kabisa. Nilienda South Africa pia kwenye meeting ambayo washiriki walitoka mataifa mbalimbali ya Africa. Unapojitambulisha unatoka Tanzania wengi wanapenda kumzungumzia Magufuli. Wengi huomba tubadilishane watupe Rais wao na kwamba tuwaazime Magufuli japo kwa mwaka mmoja.
This is very true! Kwa wote wanaotoka nje ya nchi watakwambia.


Hizi ni propaganda za kitoto. Ukienda kwenye ziara ya kinchi ni kawaida sana kusikia wakimsifu rais wenu hata kinafiki. Cga muhimu huyo rais asifiwe asisifiwe tunataka ubora wa maisha. Kama hakuna ubora wa maisha hata aje Trump hapa kumsifia Magufuli ni bure tu.
 
Kwan namibia ina Jumla ya watu wangapi,kila mtu aliongea na Mr.Slow slow?

Philips X2560
 
Back
Top Bottom