Kama Taifa hatupaswi kujutia kumpata mtu aina ya Hayati Magufuli

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Naendelea kuja hapa kivingine

Kabla ya kuendelea na declare kwamba Mi ni Mwana CCM nilofanya kazi ngazi zote za chama na kila awamu isipokuwa ya Mwalimu Nyerere,

Kila binadamu Ana mapungufu yake na ndo maana Mazuri ya JPM yapo na Mabaya yapo Pia ,

Niendelee kutumia frusa hii kuwa kumbusha kwamba Tanzania ni yetu sote na hakuna mtanzania zaidi ya mwingine,

Kuna ka kikundi uwa kanajiona wao ndo watanzania kuliko wengine ila kuna kengine nako kanaona ndo kanapaswa kupewa attention.

Faida kuu za Magufuli kuongoza Tanzania
1. Si kila kibaya ni kibaya mengine uletwa liwe funzo, funzo ni kwamba Tanzania haitakuja Tena kucheza na Nafasi ya Juu kumpa yeyote kisa ama kumkomoa mwingine au kisa kuhofia Fulani akitawala inakula kwa Fulani

2. Vetting kwenye kuwapitisha wagombea isiangalie utendaji wa kazi tu maana Magufuli mengine unaweza sema ila ukisema alikuwa mzembe ntabishana na wewe usiku kucha! Ila kupiga kazi si kigezo pekee cha kumpa mtu uongozi..na Yule aloficha faili namba 0332 la hospitali yetu ile kuu alipaswa kujua Taifa litakuja kuingia mkenge.

3. Imetuonesha aina ya wanasiasa hasa CCM tulio nao ni vigeugeu ukianzia na kigwangala ukaenda kwa kina Gambo wana switch kulingana na mdundo, wakati wa Magufuli walikuwa na msimamo fulan baada ya Magu kulala mbele wakageuka hii ni Hatari kwa uso wa dunia na nchini

4. Somo jingine ni kwamba wakati wa Kutafta Makamu wa Rais tuwe makini wenda ndo mnakuwa pia mmechagua Rais ajaye bila kujua, kuna chama fulan cha Upinzani kimewai pitisha mgombea mwenza kichekesho, kwa kuamini kwamba Rais anapaswa asiwe na vice threat wanasahau Katiba hii hata Dr Mpango japo Mungu aepushe mbali unaweza amka ukakuta ye ndo Rais wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba

5.Somo kwa Machawa wa Marais wamepata Somo kwamba usimdharau makamu wake akiondoka Rais Huyo Makamu ndo boss cc Polepole na Sabaya! Heshimu watu wote

6. Imetufundisha kwamba Taasisi nyingi za Tanzania hazina meno wanasikilizia Mungu mtu magogoni atasema nini wao wanafuata Mkumbo kwa kinachompendeza Mkuu wao wala si maslahi ya nchi ..

7. Imeleta funzo kwa watanzania miaka 6 wakiwa kifungoni bila kujua, hawakuwa huru

Nawaambia jambo moja Mwaka mmoja nilikutana na Marehemu Magufuli mlimani city kwenye sherehe za wakadiriaji majenzi, akawa anamwambia katibu wao tukiwa sehemu tunapata soda kwamba “hawa wanakusumbua kisa umewapa uhuru wa kutoa Mawazo Yao sana akasisitiza ukitaka uongoze vizuri wanyime uhuru Huo na pia hawatakuyumbisha nikasoma kitu hapo akiwa waziri

Soma Pia

NGAZI ZOTE UMEWAHI KUWA MWENYEKITI WA CHAMA TAIFA? WEWE NA MAGUFULI NI WAPUMBAV..
 
Magufuli hakustahili kuwa rais kabisa wa nchi hii. Hakuwa na sifa za kuwa rais, bali alipata kutokana na CCM kuzidiwa ushawishi katika jamii. Na huu mchezo wa hilo genge linalojiita system kutuchagulia kiongozi kwa mitazamo yao inabidi ifike mwisho.
 
Siku moja nilikuwa Kahama. Magufuli akiwa Waziri. Tukawa tunajadili nani anafaa kuwa Rais.

Kwa kuangalia ule utendaji kazi wa Magufuli, mimi nikalitaja jina la Magufuli. Mzee mmoja ambaye alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, akamaka, akasema, ' tema mate chini, balaa hilo lisitokee'. Alielezea sana, na ilionekana anamfahamu sana, kuliko wote tuliokuwepo pale.

Alipoteuliwa tu kuwa mgombea, niliyakumbuka maneno ya yule mjumbe wa NEC. Nikiwa Dar, tayari Magu akiwa ameteuliwa na kuzindua kampeni, mzee mmoja aliyekuwa ofisi ya Waziri
Mkuu, akasema, 'sijui, yaani John awe Rais, hii nchi itawaka moto. Magonjwa ya akili huwa hayaponi moja kwa moja'.

Nikayaweka maneno ya hawa wawili moyoni. Magufuli alivyoanza uongozi, hakika nikakubali kuwa wale watu wawili walikuwa wanamfahamu vizuri. Walikuwa sahihi sana.

Lakini kwa vyovyote, wanaostahili kulaumiwa sana ni Kamati Kuu ya CCM. Wao walikuwa wanamfahamu vizuri kuliko sisi sote. Nadhani alistahili kuishia kwenye utendaji na siyo kuwa kiongozi mkuu, nafasi inayohitaji mchanganyiko wa karama, na zaidi hekima.
 
Hivi huo ugonjwa wa akili wa Magufuli ni fact, au hisia tu?

Kuna mwenye ushahidi wapi aliwahi kulazwa/tibiwa?
 
Bila kisahau ametupa somo la kuchukia watu wakisema mabaya yako. Ikiwezekana hakikisha wasiojulikana wanaenda kuhakikisha wao hawajulikani wako wapi.
 
JPM kasaidia sana kuwakumbusha watu nguvu ya Rais

Heshma waliyonayo Chadema kwa Mama wangekuwa nayo wakati wa Mkwere mengi sana yangewezekana sema enzi zile walijiona wana nguvu sana kiasi kwamba waliamini hawawezi kushughulikiwa
 
Naendelea kuja hapa kivingine

Kabla ya kuendelea na declare kwamba Mi ni Mwana CCM nilofanya kazi ngazi zote za chama na kila awamu isipokuwa ya Mwalimu Nyerere,

Kila binadamu Ana mapungufu yake na ndo maana Mazuri ya JPM yapo na Mabaya yapo Pia ,

Niendelee kutumia frusa hii kuwa kumbusha kwamba Tanzania ni yetu sote na hakuna mtanzania zaidi ya mwingine,

Kuna ka kikundi uwa kanajiona wao ndo watanzania kuliko wengine ila kuna kengine nako kanaona ndo kanapaswa kupewa attention.

Faida kuu za Magufuli kuongoza Tanzania
1. Si kila kibaya ni kibaya mengine uletwa liwe funzo, funzo ni kwamba Tanzania haitakuja Tena kucheza na Nafasi ya Juu kumpa yeyote kisa ama kumkomoa mwingine au kisa kuhofia Fulani akitawala inakula kwa Fulani

2. Vetting kwenye kuwapitisha wagombea isiangalie utendaji wa kazi tu maana Magufuli mengine unaweza sema ila ukisema alikuwa mzembe ntabishana na wewe usiku kucha! Ila kupiga kazi si kigezo pekee cha kumpa mtu uongozi..na Yule aloficha faili namba 0332 la hospitali yetu ile kuu alipaswa kujua Taifa litakuja kuingia mkenge.

3. Imetuonesha aina ya wanasiasa hasa CCM tulio nao ni vigeugeu ukianzia na kigwangala ukaenda kwa kina Gambo wana switch kulingana na mdundo, wakati wa Magufuli walikuwa na msimamo fulan baada ya Magu kulala mbele wakageuka hii ni Hatari kwa uso wa dunia na nchini

4. Somo jingine ni kwamba wakati wa Kutafta Makamu wa Rais tuwe makini wenda ndo mnakuwa pia mmechagua Rais ajaye bila kujua, kuna chama fulan cha Upinzani kimewai pitisha mgombea mwenza kichekesho, kwa kuamini kwamba Rais anapaswa asiwe na vice threat wanasahau Katiba hii hata Dr Mpango japo Mungu aepushe mbali unaweza amka ukakuta ye ndo Rais wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba

5.Somo kwa Machawa wa Marais wamepata Somo kwamba usimdharau makamu wake akiondoka Rais Huyo Makamu ndo boss cc Polepole na Sabaya! Heshimu watu wote

6. Imetufundisha kwamba Taasisi nyingi za Tanzania hazina meno wanasikilizia Mungu mtu magogoni atasema nini wao wanafuata Mkumbo kwa kinachompendeza Mkuu wao wala si maslahi ya nchi ..

7. Imeleta funzo kwa watanzania miaka 6 wakiwa kifungoni bila kujua, hawakuwa huru

Nawaambia jambo moja Mwaka mmoja nilikutana na Marehemu Magufuli mlimani city kwenye sherehe za wakadiriaji majenzi, akawa anamwambia katibu wao tukiwa sehemu tunapata soda kwamba “hawa wanakusumbua kisa umewapa uhuru wa kutoa Mawazo Yao sana akasisitiza ukitaka uongoze vizuri wanyime uhuru Huo na pia hawatakuyumbisha nikasoma kitu hapo akiwa waziri

Soma Pia

Kwa Muhtasari wako huu hapo juu inatupa funzo kuwa ni LAZIMA NCHI IPATE KATIBA MPYA.
Kama taifa haliwezi likaongozwa na kauli na matashi ya Mtu MMOJA.
Nyerere aliwahi kutahadharisha kuwa Katiba hii jinsi ilivyo mbaya Akitokea Dikteta anaweza kuitumia na kuhujumu taifa.
Funzo tumelipata kwa Magu hatuna budi kuchukuwa Hatua kabla hajatokea DIKTETA mbaya zaidi tukabaki tuna jilaumu.
Ikiwa CCM watadhani haliwahusu wao kwa vile wako madarakani, wakawaulize akina KABUDI, LUKUVI, MAKONDA, SPIKA NDUBGAI NA WENZAKE. Katiba na Nguvu ya RAISI imewangoa madarakani.
 
Hivi huo ugonjwa wa akili wa Magufuli ni fact, au hisia tu?

Kuna mwenye ushahidi wapi aliwahi kulazwa/tibiwa?

Hizi propaganda utaweza kuzijibu zote mkuu?

Mgonjwa wa akili katatua adha ya foleni Dar ndani ya miaka mitano (fly overs)

Mgonjwa wa akili amelazimisha bwawa la umeme wa kutosha na ziada

Mgonjwa wa akili amefanikisha utaratibu wa malipo ya Serikali kwa mtandao!

Na mengine mengi mazuri yanayorithiwa kimya kimya.

Pamoja na madhaifu yake ya kibinadamu, mgonjwa huyu wa akili anafaa ama hafai?
 
Kwa Muhtasari wako huu hapo juu inatupa funzo kuwa ni LAZIMA NCHI IPATE KATIBA MPYA.
Kama taifa haliwezi likaongozwa na kauli na matashi ya Mtu MMOJA.
Nyerere aliwahi kutahadharisha kuwa Katiba hii jinsi ilivyo mbaya Akitokea Dikteta anaweza kuitumia na kuhujumu taifa.
Funzo tumelipata kwa Magu hatuna budi kuchukuwa Hatua kabla hajatokea DIKTETA mbaya zaidi tukabaki tuna jilaumu.
Ikiwa CCM watadhani haliwahusu wao kwa vile wako madarakani, wakawaulize akina KABUDI, LUKUVI, MAKONDA, SPIKA NDUBGAI NA WENZAKE. Katiba na Nguvu ya RAISI imewangoa madarakani.
Yawezekana
 
Back
Top Bottom