Udhaifu wa Wabunge na Viongozi wa Chadema ndio unaowapa kiburi hao akina Polepole kuendelea kuwatukana.
Kwa nini Chadema hawajifunzi kutoka Polisi?
Kila wanapotaja jina la Magufuli, nje ya kumsifia, wanakamatwa na Polisi na kupelekwa Mahakamani.
Kwa nini ninyi Chadema mnashindwa kumfungulia kesi ya udhalilishaji Polepole?
Kwa nini mmekubali kuwa Mahakama zetu ni mahali pa ninyi kushitakiwa tu, lakini ninyi hamuendi kufungua mashitaka?
Kazi yenu imekuwa kulialia tu!
Angalieni tangia Bernard Membe ampeleke Mahakamani Cyprian Musiba, mmesikia au mmeona huyo Musiba akiropoka tena juu ya Membe?
Polisi wanawanyima vibali vya mikutano, au wanawazuia kufanya mikutano ya ndani, KINYUME CHA SHERIA, badala ya kumfungulia kesi huyo OCD "in his/her personal capacity, for his/her unlawful performance of duty', kwa kuvunja Sheria za nchi, kazi yenu ni kulalamika tu!
Hata Waziri George Mkuchika anapowaeleza kuwa msikubali kukamatwa ovyo ovyo, na ikitokea, muwafungulie mashtaka hao wanaowaweka mahabusu " unlawfully", mimi naona hamuelewi hata kidogo!
Binafsi, mnanishangaza sana.
Mawakili wenu kazi yao ni kuwatetea tu, kuwafungulia mawashitaka hao akina Polepole na Jeshi la Polisi hawawezi?
What is wrong with you?
I really miss Hon. Tundu Antipas Lissu.
I'm sorry for loosing my temper, but Chadema has to be proactive, not always reactive!