Polepole na CCM yake wapuuzwe, ni wapuuzi

Polepole na CCM yake wapuuzwe, ni wapuuzi

Nimemsikiliza jana kijana mwenzangu ndugu Humphrey Polepole akizungumza kwa niaba ya ccm juu ya mambo kadhaa aliyoyaita makubwa nchini, mambo hayo ni mauaji ya Kibiti na Ripoti ya Makanikia.

Nimelazimika kulichambua hili kwa mtindo wa makala kwa nia ya kumkanya na kumwambia Polepole awe na adabu na heshima kwa Watanzania, sisi sio wajinga kama anavyotupimia kipimo alichonacho ambacho ni wanachama wenzake ndani ya ccm.

Nimesikitika kuona kijana huyu anawaita Watanzania ni wapuuza wale tunaounga mkono juhudi za rais huku tukihoji kwamba wizi wote huu katika raslimali umefanywa na Chama cha Mapinduzi, hivyo tukitaka makada wa chama hicho wasimvuruge Rais anapojaribu kupambana na hali hii.

Natataka nimrejeshe nyuma kijana huyu kwa lengo la kumfunza ama kumkumbusha na kisha kumkanya awe na adabu mbele ya umma hasa linapokuja suala la maslahi mapana ya nchi itikadi na mihemko yake iishie viunga vya Lumumba.

Mwaka 1998 wakati makampuni makubwa ya uchimbaji madini ya ASHANTI yalipoingia mikataba na serikali ya Tanzania iliyokuwa chini ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania Benjamin William Mkapa, chama cha mapinduzi kililiridhia kwa kauli moja, serikali yake kuingia mikataba hiyo na kikahubiri hadharani kwamba taifa sasa linanufaika, Hivyo tunapohoji ushiriki na uratibu na unufaika wa ccm katika raslimali za nchi yetu, Polepole anapata wapi kibri chakutuita sisi wapuu?

Kwamfano Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega. Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni, Muulizeni Polepole kama anafahamu kampuni hii ililipa mrahaba wa shingapi mpaka madini yalipoisha? Haya yote yamefanyika chini ya ccm

Lakini sivyo tu, rejea hansadi za Bunge juu ya hotuba za Upinzani zote tangu bunge la kwanza la vyama vingi, upinzani wamekuwa wakipiga kelele uwazi wa mikataba hii ambayo yote husainiwa Ikulu ya Tanzani, yani wizi wote mkubwa katika nchi hii huratibiwa Ikulu tangu Mwalimu Nyerere alipotutoka tu. Polepole anaweza kuwa hajui kwakuwa ameingia juzi kwenye siasa ya nchi hii anafikiri kuongoza ccm ni kuongoza zile NGOs zake za pale Mwenge za utetezi wa haki za mashoga.

Suala lingine alilozungumza Polepole na kujinasibu ni kiongozi wa chama cha watu ni suala la Mauaji ya Kibiti huku akimtisha Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP katika taarifa yake. Na zaidi akajikita kutuhumu vyama vya siasa kwamba vimekaa kimya. Nataka nimkumbushe, vyama vya siasa havijakaa kimya, vyama vya siasa vina platform yake ya kutolea kauli za kitaifa na njia hii havipangiwi na chama kingine yaani chama cha kihalifu ccm,

Mauaji ya Kibiti ni uhalifu mkubwa, una kila elements za kubashiri aina zake, mauaji haya hayahitaji kukurupuka kisiasa, kwakuwa kwakufanya hivyo waweza kujikuta yanageuzwa kuwa matukio ya kisiasa au ya kidini kws vyovyote yanavyoweza kuchukuliwa, Yanahitaji vyombo vya kiuchunguzi ndivyo vishughulike nayo, na sio matamko ya kisiasa kama polepole anavyotaka iwe, wala hayahitaji matamko ya kidini labda katika muundo utakao kutanisha imani zote pawe na sauti moja, nje ya hapo yatajengwa mazingira na kuitwa mauaji ya kidini. Polepole kwa mambo haya ni mchanga, walionyamaza na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi anawaona wapuuzi ile yeye ndiye mjanja na mzalendo,

Nataka nimkumbushe tu katika utawala wake ccm, Anafahamu kwamba Ben Saanane maarufu kama Ben-Rabiu Wa Saanane ni mwezi wa sita huu amepotea/ametekwa? Ipo wapi kauli ya chama chake katika hili?

Anafahamu kwamba Bagamoyo miili saba iliokotwa kwenye viroba ikazikwa pembeni ya mto mithiri ya mbwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Anafahamu kwamba Lugumi imekiuka mkataba wa makubaliano na wizara ya mapolisi juu ya ufungaji ya mitambo ya kielekroniki vituo vya polisi na kampuni hiyo ilishalipws pesa zote kufunga vituo zaidi ya 200 lakini mpaka dakika hii ni vituo vinne tu ndivyo vimefungwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Mnafiki mkubwa huyu..

Manunuzi ya Ndege, ujenzi wa barabara za Mwenge > Moroko, Mwanza Airport nk zimeidhinishwa cha Bunge lipi nchini? Ipo wapi kauli ya chama katika hili yeye akiwa ni msemaji?

Namsihi sana Polepole awe na adabu mbele za Watanzania, Chama cha Mapinduzi katiks suala la madini na mengineyo yote, kabla ya kusimama hadharani na kujitia kuwatusi watanzania kwamba wapuuzi kinatakiwa kutuomba radhi watanzania kwa uhalifu mkubwa na uhujumu uchumi wa nchi yetu tangu 1997 mpaka leo hii...

Polepole alitakiwa jana kuitumia nafasi ile kuliomba radhi taifa kwa chama chake kutubaka bila ridhaa yetu kwa miaka 18 mpaks leo katika raslimali zetu, lakini kwakuwa kijana keshakunywa madaraka ya kulevya basi kaishia kututukana tu huku akijiita ccm mpya.

Na Yericko Nyerere
wewe ndio wa kupuuzwa kwa sababu wewe ni mpuuzi siku zote.
 
Hivi Yericko Nyerere si mioto wa Kanda ya Ziwa?(Royal Faimly) mbona anachatuka hivi. Anatakiwa awe kama Paskali Msukum!.
 
Ni lazima mkubali dude lenu limeoza siku nyingi, sasa linaendelea kuwanukia watanzania wote...
Naona hata huelewi nini nimekiandika ila ndiyo hali tuliyonayo kwasasa wache Mkapa atuite wapumbafu maana ndiyo kipaji chetu watanzania.
 
Mamilioni ya watanzania tayari wamesha wapuuza ccm
kaka tulisema hivyo hivyo baada ya list of shame lakini watanzania wakatuletea Magufuli. Angalia sana ulimi wako mkuu huzungumzii watanzania wote unazungumzia washabiki wa kisiasa waliojaa mitandaoni hata hapa JF
 
Umekuwa ukijaribu kwa miaka mingi duh, upo pale paleeeee eeeeh

Hadi sasa unazidi kutoa mapovu.

Kichwa cha uzi wako kimenitosha kuandika haya.
 
Kila nikiona au kusikia jina la Hamphrey Polepole najisikia vibaya sana,ila sitaki kuwasemea watanzania wengine.huyu kijana mwenzetu tangu alipokua kwenye mchakato wa katiba mpya hadi kuandikwa kwa rasimu ya katiba mpya nilikua namuuliza Mungu kama kuna akina Polepole wengine 10 tu amwongezee huyu kijana nguvu tupate katiba mpya.Kwa ujumla michango yake hasa ktk kuonyesha udhaifu na ukandamizaji wa chama tawala ktk swala Zima la maendeleo ya nchi hii yalinipa tumaini mkubwa sana kwa kijana huyu.Zilipoanza kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 nikua namfuatilia tu lkn zilipo kolea,nikaanza kuona mchele mchele.
Lakini matumaini yaliisha pale niliposhudia huyu kijana mwenzetu,alipokuali kuonyesha rangi zake halisi kwa kkujisaliti,kujikataa na hata kuwasaliti watanzania wenzake kwa kupokea kijiti cha ukatibu uenezi na itikadi kutoka kwa Nape huku akijuwa wazi kasha nasa kwenye mtego wa milele wa kuzima nyota yake iliyong'aa ghafla ktk kudai na kuwatetea watanzania kupata katiba mpya itakayojibu aswali na kutatua matatizo mengi ya watz.Namhakikishia hakuna siku atakayo kuja kung'aa tena kama Enzi za mchakato wa katiba mpya.Nadhani he is in the wrong track kama hatojali kupoteza maslahi binafsi basi angalie pale alipo jikwaa!
Mimi binafsi hamna jema jipya analoweza kuzumngumzia kwa sasa kuhusu alipo nikamwelewa maana hata yeye mwenyewe anajua anaigiza tu siku iingie.
Kuhusu hili la madini na rasilimali yetu kwa ujumla,kama ni mzalendo kweli na ni msisi emu mpya basi yeye na wenzake waamue kumweleza mh rais ukweli wote mchungu kuhusu chama chake ili ktk vita hii ajipange vizuri akijua anapambana na makaburu wa nje na wa ndani ya nyumbani kwake.
 
kaka tulisema hivyo hivyo baada ya list of shame lakini watanzania wakatuletea Magufuli. Angalia sana ulimi wako mkuu huzungumzii watanzania wote unazungumzia washabiki wa kisiasa waliojaa mitandaoni hata hapa JF
Watanzania
 
mimi Gang mo nilishawapuuza ccm na vibarka wao kabla hata sijazaliwa
 
Ccm wote hua hawana akili mpaka wakitumbuliwa ndiyo wanapata akili
 
Wenye akili tulimpuuza hata kabla hajatoa hicho kijitamko chake.
Mi nilishampuuza tangu alipokubali kuwa mkuu wa wilaya as if si yeye aliyekuwa akihubiri ITV wakati wa mchakato wa katiba mpya juu ya mamlaka ya rais na msururu wa viongozi wasio na kazi. Mnafiki sana kakaangu huyu
 
Wakati tunaungana, ni vema pia tukajuwa kuwa aliyetufikisha hapo ni CCM na serikali yake.Na kwa kweli ili haya yasijirudie tena huko mbele njia pekee ni kuitoa CCM na serikali yake madarakani kwa namna yoyote kupitia sanduku la kura, ikishindikana hats kwa maombi tujaribu.
Mmmmh.hyo kesi nyingine mkuu.
 
Nimemsikiliza jana kijana mwenzangu ndugu Humphrey Polepole akizungumza kwa niaba ya ccm juu ya mambo kadhaa aliyoyaita makubwa nchini, mambo hayo ni mauaji ya Kibiti na Ripoti ya Makanikia.

Nimelazimika kulichambua hili kwa mtindo wa makala kwa nia ya kumkanya na kumwambia Polepole awe na adabu na heshima kwa Watanzania, sisi sio wajinga kama anavyotupimia kipimo alichonacho ambacho ni wanachama wenzake ndani ya ccm.

Nimesikitika kuona kijana huyu anawaita Watanzania ni wapuuza wale tunaounga mkono juhudi za rais huku tukihoji kwamba wizi wote huu katika raslimali umefanywa na Chama cha Mapinduzi, hivyo tukitaka makada wa chama hicho wasimvuruge Rais anapojaribu kupambana na hali hii.

Natataka nimrejeshe nyuma kijana huyu kwa lengo la kumfunza ama kumkumbusha na kisha kumkanya awe na adabu mbele ya umma hasa linapokuja suala la maslahi mapana ya nchi itikadi na mihemko yake iishie viunga vya Lumumba.

Mwaka 1998 wakati makampuni makubwa ya uchimbaji madini ya ASHANTI yalipoingia mikataba na serikali ya Tanzania iliyokuwa chini ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania Benjamin William Mkapa, chama cha mapinduzi kililiridhia kwa kauli moja, serikali yake kuingia mikataba hiyo na kikahubiri hadharani kwamba taifa sasa linanufaika, Hivyo tunapohoji ushiriki na uratibu na unufaika wa ccm katika raslimali za nchi yetu, Polepole anapata wapi kibri chakutuita sisi wapuu?

Kwamfano Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega. Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni, Muulizeni Polepole kama anafahamu kampuni hii ililipa mrahaba wa shingapi mpaka madini yalipoisha? Haya yote yamefanyika chini ya ccm

Lakini sivyo tu, rejea hansadi za Bunge juu ya hotuba za Upinzani zote tangu bunge la kwanza la vyama vingi, upinzani wamekuwa wakipiga kelele uwazi wa mikataba hii ambayo yote husainiwa Ikulu ya Tanzani, yani wizi wote mkubwa katika nchi hii huratibiwa Ikulu tangu Mwalimu Nyerere alipotutoka tu. Polepole anaweza kuwa hajui kwakuwa ameingia juzi kwenye siasa ya nchi hii anafikiri kuongoza ccm ni kuongoza zile NGOs zake za pale Mwenge za utetezi wa haki za mashoga.

Suala lingine alilozungumza Polepole na kujinasibu ni kiongozi wa chama cha watu ni suala la Mauaji ya Kibiti huku akimtisha Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP katika taarifa yake. Na zaidi akajikita kutuhumu vyama vya siasa kwamba vimekaa kimya. Nataka nimkumbushe, vyama vya siasa havijakaa kimya, vyama vya siasa vina platform yake ya kutolea kauli za kitaifa na njia hii havipangiwi na chama kingine yaani chama cha kihalifu ccm,

Mauaji ya Kibiti ni uhalifu mkubwa, una kila elements za kubashiri aina zake, mauaji haya hayahitaji kukurupuka kisiasa, kwakuwa kwakufanya hivyo waweza kujikuta yanageuzwa kuwa matukio ya kisiasa au ya kidini kws vyovyote yanavyoweza kuchukuliwa, Yanahitaji vyombo vya kiuchunguzi ndivyo vishughulike nayo, na sio matamko ya kisiasa kama polepole anavyotaka iwe, wala hayahitaji matamko ya kidini labda katika muundo utakao kutanisha imani zote pawe na sauti moja, nje ya hapo yatajengwa mazingira na kuitwa mauaji ya kidini. Polepole kwa mambo haya ni mchanga, walionyamaza na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi anawaona wapuuzi ile yeye ndiye mjanja na mzalendo,

Nataka nimkumbushe tu katika utawala wake ccm, Anafahamu kwamba Ben Saanane maarufu kama Ben-Rabiu Wa Saanane ni mwezi wa sita huu amepotea/ametekwa? Ipo wapi kauli ya chama chake katika hili?

Anafahamu kwamba Bagamoyo miili saba iliokotwa kwenye viroba ikazikwa pembeni ya mto mithiri ya mbwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Anafahamu kwamba Lugumi imekiuka mkataba wa makubaliano na wizara ya mapolisi juu ya ufungaji ya mitambo ya kielekroniki vituo vya polisi na kampuni hiyo ilishalipws pesa zote kufunga vituo zaidi ya 200 lakini mpaka dakika hii ni vituo vinne tu ndivyo vimefungwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Mnafiki mkubwa huyu..

Manunuzi ya Ndege, ujenzi wa barabara za Mwenge > Moroko, Mwanza Airport nk zimeidhinishwa cha Bunge lipi nchini? Ipo wapi kauli ya chama katika hili yeye akiwa ni msemaji?

Namsihi sana Polepole awe na adabu mbele za Watanzania, Chama cha Mapinduzi katiks suala la madini na mengineyo yote, kabla ya kusimama hadharani na kujitia kuwatusi watanzania kwamba wapuuzi kinatakiwa kutuomba radhi watanzania kwa uhalifu mkubwa na uhujumu uchumi wa nchi yetu tangu 1997 mpaka leo hii...

Polepole alitakiwa jana kuitumia nafasi ile kuliomba radhi taifa kwa chama chake kutubaka bila ridhaa yetu kwa miaka 18 mpaks leo katika raslimali zetu, lakini kwakuwa kijana keshakunywa madaraka ya kulevya basi kaishia kututukana tu huku akijiita ccm mpya.

Na Yericko Nyerere
Tumuunge mkono Mhe.Rais kwa kupigania rasilimali za nchi zisipotee lakini tuzuie wajinga wachache wanaotaka kubeba jambo hili kisiasa. Nimemsikia Polepole akiwalaumu watanzania na viongozi wa dini eti wamekaa kimya wakati rasilimali za nchi zikiibiwa.

Ndugu Polepole hajawatendea haki watanzania wala viongozi wa dini, anapaswa awaombe radhi. Hivi waliotuingiza kwenye mikataba mibovu ni viongozi wa dini? Polepole anasahau kuwa mikataba yote ya hovyo inayoliangamiza taifa hili imepitishwa na serikali ya CCM na kuungwa mkono kwa kura nyingi za NDIYO kutoka kwa wabunge wa CCM?

Kimsingi Polepole hana "moral authority" ya kujadili suala hili maana CCM yake na wabunge wake ndio waliotuingiza kwenye matatizo yote haya. Kikubwa anachoweza kufanya Polepole ni kuomba radhi kwa niaba ya chama chake, kwa serikali yake kuliingiza taifa kwenye hasara kubwa. Na sio kuwalaumu viongozi wa dini.

Viongozi wa dini hawatungi sera, hawapitishi sheria, hawana nguvu ya dola. Sasa wanalaumiwa kwa lipi? Yani uache kulaumu wabunge wa CCM waliopitisha sheria mbovu za madini, uje kulaumu wachungaji, mapadri na masheikh? Upuuzi gani huu?

Serikali ya Rais Mkapa ndiyo iliyopitisha sheria inayoruhusu mchanga kusafirishwa nje ya nchi. Kwahiyo kama ni kuibiwa tumeibiwa tangu wakati wa Mkapa. Lakini Mkapa hakuwa TLP wala TADEA. Alikua CCM. Na wabunge wa CCM ndio waliopitosha sheria hiyo kwa wingi wao.

Leo watu walewale waliopitisha utaratibu huo kwa makofi ya shangwe, ndio haohao wanaompigia makofi aliyetengua utaratibu huo. Unafiki.!!

Wabunge wa upinzani walipokataa kupitisha sheria ya madini kwa dharura walifukuzwa bungeni. Walipohoji kwanini sheria nyeti inayolinda rasilimali zetu ipitishwe kwa dharura wabunge wa CCM walizomea.

Waziri Muhongo akasimama na kuwadhihaki wanasheria wa madini kuwa hawajui kiingereza. Spika akawafukuza wabunge wa upinzani, wale wa CCM wakabaki ndani na kupitisha sheria hiyo kwa kura ya NDIYO. Leo watu walewale, wa chama kilekile kilichotuingiza kwenye matatizo badala ya kuomba radhi, wanaibuka na kuwalaumu viongozi wa dini. Huu ni wendawazimu.!

Serikali ya CCM na wabunge wake wametuingiza kwenye matatizo makubwa sana kama taifa. Rais anapochukua hatua tunapaswa tumuunge mkono kwa umoja wetu kama taifa. Rais anafanya kazi ya nchi, sio kazi ya CCM. Kama mnataka afanye kazi ya CCM jengeeni matawi aje kuzindua.

Viongozi wengi wa upinzani walipohoji mambo haya waliitwa wachochezi. Leo Rais anafanya yaleyale ambayo wapinzani walihoji then viongozi wachache wa CCM wanataka kujivika ushujaa. Ujinga wa kiwango cha lami.

Na hili la madini ni moja tu kati ya mengi ambayo serikali ya CCM imetuingiza kwenye matatizo. Huko kwenye utalii, maliasili, uvuvi, uwekezaji etc kuna mengi mazito kuliko haya. Kwa mfano Loliondo kuna mwekezaji amepewa kibali cha uwindaji lakini amegeuza eneo hilo kuwa sehemu ya nchi yake. Ukiingia ktk himaya yake network ya simu ya mitandao ya ndani inapotea na inasoma United Arabs Emirates.

Mwarabu huyo anadaiwa kuwafukuza wakazi wa eneo hilo ambao ni wamasai na kuwachomea nyumba zao na kuchoma mifugo yao. Pia amejenga uwanja mkubwa ambapo ndege hutua moja kwa moja huko mbugani na kubeba wanyama kwenda uarabuni bila kukaguliwa na mamlaka yoyote ya ndani.

Jambo hili limepigiwa kelele na wapinzani kwa muda mrefu lakini wakaitwa wachochezi. Lakini siku Rais Magufuli akiamua kumfukuza huyu mwekezaji, viongozi wa CCM watakua mstari wa mbele kumpongeza Rais, wakati CCM hiyohiyo na wabunge wake wamemlinda Mwekezaji huyo kwa muda wote huu.

Tuache unafiki kwenye masuala ya kitaifa. Polepole aache kuwalaumu viongozi wa dini, instaed akilaumu chama chake na wabunge wake wa CCM kwa kupitisha mikataba ya hovyo inayoligharimu taifa. Rasilimali za nchi hii sio za CCM, sio za CHADEMA sio za ACT. Ni za watanzania wote. Yoyote anayezitetea tutamuunga mkono bila kujali tofauti zetu za itikadi za vyama.!

Malisa GJ
 
Yerico Nyerere!eti anataka ccm wapuuzwe?watu walio madarakani utawapuuza vipi.Hata chadema wenyewe mnawafuatilia ccm na kuwa makini nao ndio maana mnawasikiliza na kutoa ushauri elekezi kila siku
 
Back
Top Bottom