Polepole na CCM yake wapuuzwe, ni wapuuzi

Nimemsikiliza jana kijana mwenzangu ndugu Humphrey Polepole akizungumza kwa niaba ya ccm juu ya mambo kadhaa aliyoyaita makubwa nchini, mambo hayo ni mauaji ya Kibiti na Ripoti ya Makanikia.

Nimelazimika kulichambua hili kwa mtindo wa makala kwa nia ya kumkanya na kumwambia Polepole awe na adabu na heshima kwa Watanzania, sisi sio wajinga kama anavyotupimia kipimo alichonacho ambacho ni wanachama wenzake ndani ya ccm.

Nimesikitika kuona kijana huyu anawaita Watanzania ni wapuuza wale tunaounga mkono juhudi za rais huku tukihoji kwamba wizi wote huu katika raslimali umefanywa na Chama cha Mapinduzi, hivyo tukitaka makada wa chama hicho wasimvuruge Rais anapojaribu kupambana na hali hii.

Natataka nimrejeshe nyuma kijana huyu kwa lengo la kumfunza ama kumkumbusha na kisha kumkanya awe na adabu mbele ya umma hasa linapokuja suala la maslahi mapana ya nchi itikadi na mihemko yake iishie viunga vya Lumumba.

Mwaka 1998 wakati makampuni makubwa ya uchimbaji madini ya ASHANTI yalipoingia mikataba na serikali ya Tanzania iliyokuwa chini ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania Benjamin William Mkapa, chama cha mapinduzi kililiridhia kwa kauli moja, serikali yake kuingia mikataba hiyo na kikahubiri hadharani kwamba taifa sasa linanufaika, Hivyo tunapohoji ushiriki na uratibu na unufaika wa ccm katika raslimali za nchi yetu, Polepole anapata wapi kibri chakutuita sisi wapuu?

Kwamfano Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega. Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni, Muulizeni Polepole kama anafahamu kampuni hii ililipa mrahaba wa shingapi mpaka madini yalipoisha? Haya yote yamefanyika chini ya ccm

Lakini sivyo tu, rejea hansadi za Bunge juu ya hotuba za Upinzani zote tangu bunge la kwanza la vyama vingi, upinzani wamekuwa wakipiga kelele uwazi wa mikataba hii ambayo yote husainiwa Ikulu ya Tanzani, yani wizi wote mkubwa katika nchi hii huratibiwa Ikulu tangu Mwalimu Nyerere alipotutoka tu. Polepole anaweza kuwa hajui kwakuwa ameingia juzi kwenye siasa ya nchi hii anafikiri kuongoza ccm ni kuongoza zile NGOs zake za pale Mwenge za utetezi wa haki za mashoga.

Suala lingine alilozungumza Polepole na kujinasibu ni kiongozi wa chama cha watu ni suala la Mauaji ya Kibiti huku akimtisha Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP katika taarifa yake. Na zaidi akajikita kutuhumu vyama vya siasa kwamba vimekaa kimya. Nataka nimkumbushe, vyama vya siasa havijakaa kimya, vyama vya siasa vina platform yake ya kutolea kauli za kitaifa na njia hii havipangiwi na chama kingine yaani chama cha kihalifu ccm,

Mauaji ya Kibiti ni uhalifu mkubwa, una kila elements za kubashiri aina zake, mauaji haya hayahitaji kukurupuka kisiasa, kwakuwa kwakufanya hivyo waweza kujikuta yanageuzwa kuwa matukio ya kisiasa au ya kidini kws vyovyote yanavyoweza kuchukuliwa, Yanahitaji vyombo vya kiuchunguzi ndivyo vishughulike nayo, na sio matamko ya kisiasa kama polepole anavyotaka iwe, wala hayahitaji matamko ya kidini labda katika muundo utakao kutanisha imani zote pawe na sauti moja, nje ya hapo yatajengwa mazingira na kuitwa mauaji ya kidini. Polepole kwa mambo haya ni mchanga, walionyamaza na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi anawaona wapuuzi ile yeye ndiye mjanja na mzalendo,

Nataka nimkumbushe tu katika utawala wake ccm, Anafahamu kwamba Ben Saanane maarufu kama Ben-Rabiu Wa Saanane ni mwezi wa sita huu amepotea/ametekwa? Ipo wapi kauli ya chama chake katika hili?

Anafahamu kwamba Bagamoyo miili saba iliokotwa kwenye viroba ikazikwa pembeni ya mto mithiri ya mbwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Anafahamu kwamba Lugumi imekiuka mkataba wa makubaliano na wizara ya mapolisi juu ya ufungaji ya mitambo ya kielekroniki vituo vya polisi na kampuni hiyo ilishalipws pesa zote kufunga vituo zaidi ya 200 lakini mpaka dakika hii ni vituo vinne tu ndivyo vimefungwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Mnafiki mkubwa huyu..

Manunuzi ya Ndege, ujenzi wa barabara za Mwenge > Moroko, Mwanza Airport nk zimeidhinishwa cha Bunge lipi nchini? Ipo wapi kauli ya chama katika hili yeye akiwa ni msemaji?

Namsihi sana Polepole awe na adabu mbele za Watanzania, Chama cha Mapinduzi katiks suala la madini na mengineyo yote, kabla ya kusimama hadharani na kujitia kuwatusi watanzania kwamba wapuuzi kinatakiwa kutuomba radhi watanzania kwa uhalifu mkubwa na uhujumu uchumi wa nchi yetu tangu 1997 mpaka leo hii...

Polepole alitakiwa jana kuitumia nafasi ile kuliomba radhi taifa kwa chama chake kutubaka bila ridhaa yetu kwa miaka 18 mpaks leo katika raslimali zetu, lakini kwakuwa kijana keshakunywa madaraka ya kulevya basi kaishia kututukana tu huku akijiita ccm mpya.

Na Yericko Nyerere

Huyu anayeitwa POLEPOLE nadhani ameshaanza kuwa KASIKASI maana anachokihubiri hakipo na nadhani Dozi ya Madaraka ya Kulevya imeanza Kumlevya.
 
Kungekuwa na sistimu ya mtu ukiumbuka unakufa Tanzania yangu kuanzia juzi tunge flahi Sana maana hakuna ccm ambae ange salia
 
I see ur point, ila mi naongea kama Mtanzania na sio UKawa wala Upinzani. Sijawahi weka imani kwa mwanadamu kwa sababu ya lable za kisiasa, CCM, CHADEMA - Mtanzania ni yule yule.
Ni vizuri kama wewe unaongea kama mtanzania lakini nilivyoona maoni yako yamenikwaza na kukuweka katika kundi moja na Yericko, lakini tuache mambo ya siasa maana wewe na mimi si wanasiasa tunachotakiwa kuacha siasa katika masuala kama haya. Maana ukianza kusema alikua wapi kufanya mwanzoni ama na yeye ni CCM basi utakua unasema aache mambo yaendelee kama siku zote na hilo ni kosa kubwa.

Mikataba ilishafanywa na wahuni hivyo baada ya kumtafuta mchawi anachotakiwa kukifanya ni kuanzia hapa tulipo maana akiingia huko nyuma kuna mahala atakwama. Aige mfano wa Rais wa Nigeria makaburi ni magumu sana kuyafukua...Me just say
 
Nimemsikiliza jana kijana mwenzangu ndugu Humphrey Polepole akizungumza kwa niaba ya ccm juu ya mambo kadhaa aliyoyaita makubwa nchini, mambo hayo ni mauaji ya Kibiti na Ripoti ya Makanikia.

Nimelazimika kulichambua hili kwa mtindo wa makala kwa nia ya kumkanya na kumwambia Polepole awe na adabu na heshima kwa Watanzania, sisi sio wajinga kama anavyotupimia kipimo alichonacho ambacho ni wanachama wenzake ndani ya ccm.

Nimesikitika kuona kijana huyu anawaita Watanzania ni wapuuza wale tunaounga mkono juhudi za rais huku tukihoji kwamba wizi wote huu katika raslimali umefanywa na Chama cha Mapinduzi, hivyo tukitaka makada wa chama hicho wasimvuruge Rais anapojaribu kupambana na hali hii.

Natataka nimrejeshe nyuma kijana huyu kwa lengo la kumfunza ama kumkumbusha na kisha kumkanya awe na adabu mbele ya umma hasa linapokuja suala la maslahi mapana ya nchi itikadi na mihemko yake iishie viunga vya Lumumba.

Mwaka 1998 wakati makampuni makubwa ya uchimbaji madini ya ASHANTI yalipoingia mikataba na serikali ya Tanzania iliyokuwa chini ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania Benjamin William Mkapa, chama cha mapinduzi kililiridhia kwa kauli moja, serikali yake kuingia mikataba hiyo na kikahubiri hadharani kwamba taifa sasa linanufaika, Hivyo tunapohoji ushiriki na uratibu na unufaika wa ccm katika raslimali za nchi yetu, Polepole anapata wapi kibri chakutuita sisi wapuu?

Kwamfano Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega. Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni, Muulizeni Polepole kama anafahamu kampuni hii ililipa mrahaba wa shingapi mpaka madini yalipoisha? Haya yote yamefanyika chini ya ccm

Lakini sivyo tu, rejea hansadi za Bunge juu ya hotuba za Upinzani zote tangu bunge la kwanza la vyama vingi, upinzani wamekuwa wakipiga kelele uwazi wa mikataba hii ambayo yote husainiwa Ikulu ya Tanzani, yani wizi wote mkubwa katika nchi hii huratibiwa Ikulu tangu Mwalimu Nyerere alipotutoka tu. Polepole anaweza kuwa hajui kwakuwa ameingia juzi kwenye siasa ya nchi hii anafikiri kuongoza ccm ni kuongoza zile NGOs zake za pale Mwenge za utetezi wa haki za mashoga.

Suala lingine alilozungumza Polepole na kujinasibu ni kiongozi wa chama cha watu ni suala la Mauaji ya Kibiti huku akimtisha Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP katika taarifa yake. Na zaidi akajikita kutuhumu vyama vya siasa kwamba vimekaa kimya. Nataka nimkumbushe, vyama vya siasa havijakaa kimya, vyama vya siasa vina platform yake ya kutolea kauli za kitaifa na njia hii havipangiwi na chama kingine yaani chama cha kihalifu ccm,

Mauaji ya Kibiti ni uhalifu mkubwa, una kila elements za kubashiri aina zake, mauaji haya hayahitaji kukurupuka kisiasa, kwakuwa kwakufanya hivyo waweza kujikuta yanageuzwa kuwa matukio ya kisiasa au ya kidini kws vyovyote yanavyoweza kuchukuliwa, Yanahitaji vyombo vya kiuchunguzi ndivyo vishughulike nayo, na sio matamko ya kisiasa kama polepole anavyotaka iwe, wala hayahitaji matamko ya kidini labda katika muundo utakao kutanisha imani zote pawe na sauti moja, nje ya hapo yatajengwa mazingira na kuitwa mauaji ya kidini. Polepole kwa mambo haya ni mchanga, walionyamaza na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi anawaona wapuuzi ile yeye ndiye mjanja na mzalendo,

Nataka nimkumbushe tu katika utawala wake ccm, Anafahamu kwamba Ben Saanane maarufu kama Ben-Rabiu Wa Saanane ni mwezi wa sita huu amepotea/ametekwa? Ipo wapi kauli ya chama chake katika hili?

Anafahamu kwamba Bagamoyo miili saba iliokotwa kwenye viroba ikazikwa pembeni ya mto mithiri ya mbwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Anafahamu kwamba Lugumi imekiuka mkataba wa makubaliano na wizara ya mapolisi juu ya ufungaji ya mitambo ya kielekroniki vituo vya polisi na kampuni hiyo ilishalipws pesa zote kufunga vituo zaidi ya 200 lakini mpaka dakika hii ni vituo vinne tu ndivyo vimefungwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Mnafiki mkubwa huyu..

Manunuzi ya Ndege, ujenzi wa barabara za Mwenge > Moroko, Mwanza Airport nk zimeidhinishwa cha Bunge lipi nchini? Ipo wapi kauli ya chama katika hili yeye akiwa ni msemaji?

Namsihi sana Polepole awe na adabu mbele za Watanzania, Chama cha Mapinduzi katiks suala la madini na mengineyo yote, kabla ya kusimama hadharani na kujitia kuwatusi watanzania kwamba wapuuzi kinatakiwa kutuomba radhi watanzania kwa uhalifu mkubwa na uhujumu uchumi wa nchi yetu tangu 1997 mpaka leo hii...

Polepole alitakiwa jana kuitumia nafasi ile kuliomba radhi taifa kwa chama chake kutubaka bila ridhaa yetu kwa miaka 18 mpaks leo katika raslimali zetu, lakini kwakuwa kijana keshakunywa madaraka ya kulevya basi kaishia kututukana tu huku akijiita ccm mpya.

Na Yericko Nyerere
Hakuna mtu mwenye akili wa kumsikiliza huyo chumia tumbo
 
Hahahaha tatizo la ccm ni akili ndogo sana wanapiga sarakasi huku wamevaa misuri matokeo yake mambo yote hadharani, ccm mwenye akili yake timamu ni Bashe tu labda na hawa mawaziri wanaotumbuliwa ndio huwa akili zinawaijia baada ya maslahi yao kukanyagwa
Umenena mkuu
 
kanitoa hamu huyu slowslow, ati kuwa wapinzani hawaumii, hajawahi wasikia wapinzani wakitoa pole au kukaa pa1 na kujadiliana hicho kitu, wakati wapinzani wakitaka kufanya mikutano yao wajadili hayo mambo mnawanyima vibali, mbaya zaidi mtu anasimama bungeni na kutamka hili jambo lizungumzwe kwa dharula mjengoni wao wanasema nchi ipo salama na wakakataa, yaani sikutaka kumsikiliza mpaka mwisho niliendelea na kazi zangu
 
TUACHE UCCM NA UCHADEMA.
MADINI SIO YA MAGUFULI WALA CCM.
NI YA WATANZANIA,
KWA HILI TUUNGANE
TUSIJE KUCHEKWA NA WAJUKUU ZETU.
Wakati tunaungana, ni vema pia tukajuwa kuwa aliyetufikisha hapo ni CCM na serikali yake.Na kwa kweli ili haya yasijirudie tena huko mbele njia pekee ni kuitoa CCM na serikali yake madarakani kwa namna yoyote kupitia sanduku la kura, ikishindikana hats kwa maombi tujaribu.
 
Polepole anatapatapa. Anatafuta namna ya kisikika, sasa ameamua kupayuka. Kila linalomjia kichwani basi anavaa shati ya kijani kisha anaongea na vyombo vya habari.

Ingekuwa Tanzania ni kama China kwa ukali wa sheria, robo tatu ya wanaccm wangekuwa wamenyongwa akiwemo rais Magufuli.
Nimecheka sana
 
Kwa bongo ilipofika inabidi tusameheane tu na kuungana kutetea maslahi ya taifa,ukisema kufukua makaburi,hakuna mwanasiasa atakayetoka salama,si upinzani wala watawala!
Ccm imetufikisha pahala pabaya sana
 
Nakumbuka wakati mikataba ya madini inaingiwa sana harakati na wapinzani wengi walilalama sana kupinga mikataba mibovu ya madini ambayo ilionekana dhahili kwamba madini hayo hayatatunufaisha madini yatachimbwa na yataisha na tutaachiwa mahandaki tu sasa hali hii imeanza kujionyesha hadharani kwanza mgodi Wa nzega wameshafungwa tumeachiwa mahandaki na hakuna manufaa tukiyoambulia na mda si mrefu mgodi Wa buzwagi nao utafungwa Kwa mrahaba 4%!na kuna mda wakati mikataba inaingiwa kuna MTU mmoja Kwa wakati ile nilikuwa Simjui anaitwa tundu lissu akiwa Mwanasheria Wa mazingira aliwahi kumkuta kwenye kituo kimoja cha luninga alipotoa malalamiko ya makampuni ya madini na askari polisi kufanya unyama huko bulyankuru Kwa kufukia Kwa makatapila wachimbaji wadogo katika migodi hiyo lakini serikali ilipinga Kwa nguvu zote ,na akaelezea azma yake ya kuwahi mkutano Wa washika dau Wa madini uliokuwa ukifanyika Canada lakini kabla alizungumzia kauli hiyo ya washika dau wakiwa marekani kuwa kampuni ya barrick ilikuwa imenunua eneo LA ardhi lenye ukubwa Wa theruthi moja Tanzania!hivyo Tanzania hii inafikia kuwa nchi ya Shamba LA bibi kwani lawama kubwa ziiendee chama chapinduzi (ccm)Kwa wizi mkubwa unaofanyika na uliofanyika nasema ccm kwani ndo chama kinachoongoza nchi na binge lake kwani binge kinashindwa kufanya kazi zake kinafanya kazi ya kusifia raid wao na chama wanaacha kabisa masilahi ya taifa na jambo lingine watawala kudharau wadau wengine kwani wao ndo wao!Mimi rais wangu namjua kinadharia utendaji wake tatizo LA huu ufisadi ni katiba mbovu tuliyonayo inatakiwa rais ambaye anamadaraka makubwa panatakiwa pawepo chombo cha kumdhibiti pindi ikitokea anakiuka miiko ya uongozi na Mimi nilitarajia kwa rais wetu Wa sasa pindi alipoingia madarakani kwa sababu chama chake kina nguvu kuliko rais angefanya kama alivyofanya rais wa Malawi Wa kipindi mile sijui alikuwa mbingu wamthalika (nimesahau kidogo)yeye kwa kuwa alikuwa anakijua chama chake kwa ufisadi na roho mbaya yeye baada ya kuapishwa na kuchukua madaraka akaamua kuhama chama na kuanzisha cha kwake ndo akaanza kusafisha chama kwani huwezi kusafisha chama ukiwa ndani ya chama!
 
Na pia kuhusu mauaji mbona hashangai polisi kuua waislam kisa wana ndevu tu....
Kuhusu mikataba ..mbona hasemi mkataba wa kujenga bomba la mafuta Kutoka kwa Museveni? Mbona huo mkataba wa siri ? Museveni ni fisadi wa kutupwa kuna nini huu mkataba ? Kwa taarifa tu kupitisha mafuta kwa bomba basi transit fee ndogo kabisa ni $10 kwa barel moja na uganda itapitisha mapipa 600,000 kwa siku ..mkataba uko wapi ? Au museveni kaahidi kuzile ccm ? Mnataka akiondoka magu yuje tena kujadili huu mkataba...kama hakuna ufisadi basi wekeni wazi ujulikane taifa litapata kiasi gani kama transit fees. Msituhadae na idadi ya ajira za manamba za muda.....we need to know transit fees ni kiasi gani...sudan wanapata $1,200,000 kwa siku kupitasha mafuta ya Juba....
Nakuunga mkono kwa 100%
 
Back
Top Bottom