Polepole na CCM yake wapuuzwe, ni wapuuzi

Polepole na CCM yake wapuuzwe, ni wapuuzi

Polepole anajua kukariri ibara za katiba tu lakin mambo ya uchanganuzi au kujenga hoja ni zero (uwezo mdogo) hapa CCM inabidi ifanye kazi ya ziada kumtafutia mtu wa kumsaidia katika hili kwa kuwa kambi ya upinzani bunge ilisema lijadiliwe kama hoja maalum wao kwa wingi wao walikataa hotuba ya Lema liyozungumzi hili jambo walipinga na kuzomea ushauri polisi isifanye kazi za Kisiasa itafanikiwa au tuwalete Scotland yard
 
Hakuna haki wala maendeleo ndani yahili taifa bila kuuondoa ccm madalakani. Kamaunabisha basi hayaja kukuta au hazikutoshi kchwani. narudia tena tutaendelea Kuwa hivihuvi mpaka wajukuu zetu watakapo jtambua.hakuna cha mtetezi wawa nyonge wala nini hapa.kila kitu siasa navisasi nakuonea watu ovyo
 
Ni vizuri kama wewe unaongea kama mtanzania lakini nilivyoona maoni yako yamenikwaza na kukuweka katika kundi moja na Yericko, lakini tuache mambo ya siasa maana wewe na mimi si wanasiasa tunachotakiwa kuacha siasa katika masuala kama haya. Maana ukianza kusema alikua wapi kufanya mwanzoni ama na yeye ni CCM basi utakua unasema aache mambo yaendelee kama siku zote na hilo ni kosa kubwa.

Mikataba ilishafanywa na wahuni hivyo baada ya kumtafuta mchawi anachotakiwa kukifanya ni kuanzia hapa tulipo maana akiingia huko nyuma kuna mahala atakwama. Aige mfano wa Rais wa Nigeria makaburi ni magumu sana kuyafukua...Me just say

Na akianzania hapa natakiwa awaunganishe wanasiasa wote, wachumi, wanasheria bila kuangalia itikadi kusaidiana kwa pamoja kutatua, ila tusipoangalia ataendelea na mtazamo wa watu wa kijani tu.
 
Ni kweli kabisa,hasa wale waliokuwa viongozi kama Sumaye,lowasa and co.
Rudisheni rambirambi za wafiwa wacha kujitoa akili
979992cbc9bd78f817d4ed2b97be1164.jpg
 
Alidharaulika tangu alipokubali kuyala matapishi yake
Exactly, mchumia tumbo, mjinga kabisa! Vijitu vidovidogo usiviamini. Kwetu wamama waliokuwa wanazalisha wajawazito enzi hizo walikuwa wanaviua during parturition! visilete mbegu mbaya kwenye ukoo! They were able to locate then at birth! (linaweza lisiwe andiko zuri, lakini ilikuwa inafanyika hivyo believing kuwa ukiwa mdogo mdogo na akili ni ndogo)
 
Nimemsikiliza jana kijana mwenzangu ndugu Humphrey Polepole akizungumza kwa niaba ya ccm juu ya mambo kadhaa aliyoyaita makubwa nchini, mambo hayo ni mauaji ya Kibiti na Ripoti ya Makanikia.

Nimelazimika kulichambua hili kwa mtindo wa makala kwa nia ya kumkanya na kumwambia Polepole awe na adabu na heshima kwa Watanzania, sisi sio wajinga kama anavyotupimia kipimo alichonacho ambacho ni wanachama wenzake ndani ya ccm.

Nimesikitika kuona kijana huyu anawaita Watanzania ni wapuuza wale tunaounga mkono juhudi za rais huku tukihoji kwamba wizi wote huu katika raslimali umefanywa na Chama cha Mapinduzi, hivyo tukitaka makada wa chama hicho wasimvuruge Rais anapojaribu kupambana na hali hii.

Natataka nimrejeshe nyuma kijana huyu kwa lengo la kumfunza ama kumkumbusha na kisha kumkanya awe na adabu mbele ya umma hasa linapokuja suala la maslahi mapana ya nchi itikadi na mihemko yake iishie viunga vya Lumumba.

Mwaka 1998 wakati makampuni makubwa ya uchimbaji madini ya ASHANTI yalipoingia mikataba na serikali ya Tanzania iliyokuwa chini ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania Benjamin William Mkapa, chama cha mapinduzi kililiridhia kwa kauli moja, serikali yake kuingia mikataba hiyo na kikahubiri hadharani kwamba taifa sasa linanufaika, Hivyo tunapohoji ushiriki na uratibu na unufaika wa ccm katika raslimali za nchi yetu, Polepole anapata wapi kibri chakutuita sisi wapuu?

Kwamfano Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega. Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni, Muulizeni Polepole kama anafahamu kampuni hii ililipa mrahaba wa shingapi mpaka madini yalipoisha? Haya yote yamefanyika chini ya ccm

Lakini sivyo tu, rejea hansadi za Bunge juu ya hotuba za Upinzani zote tangu bunge la kwanza la vyama vingi, upinzani wamekuwa wakipiga kelele uwazi wa mikataba hii ambayo yote husainiwa Ikulu ya Tanzani, yani wizi wote mkubwa katika nchi hii huratibiwa Ikulu tangu Mwalimu Nyerere alipotutoka tu. Polepole anaweza kuwa hajui kwakuwa ameingia juzi kwenye siasa ya nchi hii anafikiri kuongoza ccm ni kuongoza zile NGOs zake za pale Mwenge za utetezi wa haki za mashoga.

Suala lingine alilozungumza Polepole na kujinasibu ni kiongozi wa chama cha watu ni suala la Mauaji ya Kibiti huku akimtisha Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP katika taarifa yake. Na zaidi akajikita kutuhumu vyama vya siasa kwamba vimekaa kimya. Nataka nimkumbushe, vyama vya siasa havijakaa kimya, vyama vya siasa vina platform yake ya kutolea kauli za kitaifa na njia hii havipangiwi na chama kingine yaani chama cha kihalifu ccm,

Mauaji ya Kibiti ni uhalifu mkubwa, una kila elements za kubashiri aina zake, mauaji haya hayahitaji kukurupuka kisiasa, kwakuwa kwakufanya hivyo waweza kujikuta yanageuzwa kuwa matukio ya kisiasa au ya kidini kws vyovyote yanavyoweza kuchukuliwa, Yanahitaji vyombo vya kiuchunguzi ndivyo vishughulike nayo, na sio matamko ya kisiasa kama polepole anavyotaka iwe, wala hayahitaji matamko ya kidini labda katika muundo utakao kutanisha imani zote pawe na sauti moja, nje ya hapo yatajengwa mazingira na kuitwa mauaji ya kidini. Polepole kwa mambo haya ni mchanga, walionyamaza na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi anawaona wapuuzi ile yeye ndiye mjanja na mzalendo,

Nataka nimkumbushe tu katika utawala wake ccm, Anafahamu kwamba Ben Saanane maarufu kama Ben-Rabiu Wa Saanane ni mwezi wa sita huu amepotea/ametekwa? Ipo wapi kauli ya chama chake katika hili?

Anafahamu kwamba Bagamoyo miili saba iliokotwa kwenye viroba ikazikwa pembeni ya mto mithiri ya mbwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Anafahamu kwamba Lugumi imekiuka mkataba wa makubaliano na wizara ya mapolisi juu ya ufungaji ya mitambo ya kielekroniki vituo vya polisi na kampuni hiyo ilishalipws pesa zote kufunga vituo zaidi ya 200 lakini mpaka dakika hii ni vituo vinne tu ndivyo vimefungwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Mnafiki mkubwa huyu..

Manunuzi ya Ndege, ujenzi wa barabara za Mwenge > Moroko, Mwanza Airport nk zimeidhinishwa cha Bunge lipi nchini? Ipo wapi kauli ya chama katika hili yeye akiwa ni msemaji?

Namsihi sana Polepole awe na adabu mbele za Watanzania, Chama cha Mapinduzi katiks suala la madini na mengineyo yote, kabla ya kusimama hadharani na kujitia kuwatusi watanzania kwamba wapuuzi kinatakiwa kutuomba radhi watanzania kwa uhalifu mkubwa na uhujumu uchumi wa nchi yetu tangu 1997 mpaka leo hii...

Polepole alitakiwa jana kuitumia nafasi ile kuliomba radhi taifa kwa chama chake kutubaka bila ridhaa yetu kwa miaka 18 mpaks leo katika raslimali zetu, lakini kwakuwa kijana keshakunywa madaraka ya kulevya basi kaishia kututukana tu huku akijiita ccm mpya.

Na Yericko Nyerere
Kwanza hustahili kutumia jina la Nyerere kwa hulka uliyonayo,chama chako kinapenda sana kudandia mambo yasiyo na mshiko na huwa mbele kutoa matamshi,lakini kwenye mambo ya msingi na muhimu kwa nchi yetu chama chako kinaota matende,kwenye mambo ya kipuuzi Chadema hakihitaji platform lakini kwenye mambo muhimu kinahitaji platform.Chadema na wewe mwenyewe ni bure kabisa.Kwanza huaminiki na hata hao wenzako wanakuona kama mpiga domo tu.Humfikii hata robo kijana mwenzako Polepole,wee endelea kubwabwaja tu.
 
Polepole anatapatapa. Anatafuta namna ya kisikika, sasa ameamua kupayuka. Kila linalomjia kichwani basi anavaa shati ya kijani kisha anaongea na vyombo vya habari.

Ingekuwa Tanzania ni kama China kwa ukali wa sheria, robo tatu ya wanaccm wangekuwa wamenyongwa akiwemo rais Magufuli.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji2] [emoji7] [emoji43]
 
Mikataba yote ilisainiwa kwenye selikali ya Awamu ya tatu, hivyo ukitaka kuuona upuuzi wa Polepole fukuza kwanza wale mawaziri wastaafu kwenye chama cha bwana Yericko Nyerere.
 
Ccm mmetutesa sana jamani! Msituone matutusa! Mnatia hasira. Eti ccm mpya wakati watu ni walewale. Hata Magu naye slikuwepo wakati haya maovu yakifanya na hskuwahi kuonekana hata siku moja akiyapinga. Naye alishiriki kupiga dili. Kula ten percent kwenye barabara, vivuko vibovu n.k. Leo anajifanya mtakatifu!
 
Back
Top Bottom