Polepole na CCM yake wapuuzwe, ni wapuuzi

TUACHE UCCM NA UCHADEMA.
MADINI SIO YA MAGUFULI WALA CCM.
NI YA WATANZANIA,
KWA HILI TUUNGANE
TUSIJE KUCHEKWA NA WAJUKUU ZETU.
 
Bila kumsahau na Marehemu Alphonce Mawazo aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Geita wa chadema aliyeuwawa saa tano mchana,ccm walitoa tamko gani kulaani,tofauti na kutumia polisi kuzuia asiagwe,ccm ni ukimwi wa taifa ili.
 
Pole pole yuko mezani anakula... Tumuache labda kuna siku atashiba na kurudi huku tulipo!
 
Wameshajitoa ufahamu siku nyingi hata ukiwaambia ukweli jibu lao ni unajua unajua hawana ubavu kujibu hoja
 
Kwangu mimi bora hao wazungu waibe tu,hata hizo hela tukipata ccm watanunua magari ya kifahari na kusahau maendeleo ya watu,list ya magari Yao ya kifahari

Rais Benz
WAZIRI MKUU Benz
makamu Benz
waziri vx
@n,waziri vx
@makatibu vx
@rc vx
@dc vx
RPC vx
Magereza vx
igp vx
@majaji vx
@wabunge vx
spika vx
@mashirika ya vx(((((( ni bora hata Acacia waibe na kuongezea wafanyakazi mshahara kuliko hawa wakoloni ccm,wanakula wenyewe,wanajambiana wenyewe
 
Muulize Polepole ni muumini wa katiba hipi mpaka sasa
 
Shida ya CCM wanafikiri wao tu ndo wana akili na sie ni wajing wote!
Tatizo ni moja Watanzania hawaangalii nini Yericko na wewe mnasema katika mitandao wanachokiona ni kwamba CCM na genge lake la matapeli linaanza kushughulikiwa na hivyo Watanzania watawasamehe kwa hilo na UKAWA wanakosea sana kubeza hii kitu maana ndiyo silaha ya CCM kuwaua tena mwaka 2020 kama mlivyokosea mwaka 2015 kumweka mtu mliyemtukana miaka 7....Me just say
 
Watakuwa wanauelewa ukweli, ila wanachukulia uelewa mdogo wa watz wengi na uoga wetu kutimiza azma yao.
Wapinzani mnasubiri nini kuidai katiba mpya ya rasimu ya Warioba? Vinginevyo nothing will gonna change.
 
Inawezekana alikuwa na lengo jema la kufikisha ujumbe lkn kuna mambo hakusema kwa kinywa chenye kunena ya haki mfano swala la madini,nijuavyo hao ambao tunawaita wezi hawakujiweka migodini,wamefuata sheria zote.Tujiulize CHADEMA,CUF,TLPau NCCR ndio walitunga hizo sheria kwakutumia wingi wa wabunge wao bungeni tena nasikia kwa hati ya DHARURA?Mauaji ya Kibiti,kuna mbunge anaitwa Selasini(kama sikosei),sijui ni wa chama gani aliwahi kuliomba binge lijadili hali ya usalama wa nchi(kama sikosei) sijui kama alikubaliwa!Kuleta siasa wakati damu za watu zikimwagika hiyo HAPANA si Tanzania tuitakayo.
 
Nimemsikiliza jana kijana mwenzangu ndugu Humphrey Polepole akizungumza kwa niaba ya ccm juu ya mambo kadhaa aliyoyaita makubwa nchini, mambo hayo ni mauaji ya Kibiti na Ripoti ya Makanikia.

Nimelazimika kulichambua hili kwa mtindo wa makala kwa nia ya kumkanya na kumwambia Polepole awe na adabu na heshima kwa Watanzania, sisi sio wajinga kama anavyotupimia kipimo alichonacho ambacho ni wanachama wenzake ndani ya ccm.

Nimesikitika kuona kijana huyu anawaita Watanzania ni wapuuza wale tunaounga mkono juhudi za rais huku tukihoji kwamba wizi wote huu katika raslimali umefanywa na Chama cha Mapinduzi, hivyo tukitaka makada wa chama hicho wasimvuruge Rais anapojaribu kupambana na hali hii.

Natataka nimrejeshe nyuma kijana huyu kwa lengo la kumfunza ama kumkumbusha na kisha kumkanya awe na adabu mbele ya umma hasa linapokuja suala la maslahi mapana ya nchi itikadi na mihemko yake iishie viunga vya Lumumba.

Mwaka 1998 wakati makampuni makubwa ya uchimbaji madini ya ASHANTI yalipoingia mikataba na serikali ya Tanzania iliyokuwa chini ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania Benjamin William Mkapa, chama cha mapinduzi kililiridhia kwa kauli moja, serikali yake kuingia mikataba hiyo na kikahubiri hadharani kwamba taifa sasa linanufaika, Hivyo tunapohoji ushiriki na uratibu na unufaika wa ccm katika raslimali za nchi yetu, Polepole anapata wapi kibri chakutuita sisi wapuu?

Kwamfano Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega. Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni, Muulizeni Polepole kama anafahamu kampuni hii ililipa mrahaba wa shingapi mpaka madini yalipoisha? Haya yote yamefanyika chini ya ccm

Lakini sivyo tu, rejea hansadi za Bunge juu ya hotuba za Upinzani zote tangu bunge la kwanza la vyama vingi, upinzani wamekuwa wakipiga kelele uwazi wa mikataba hii ambayo yote husainiwa Ikulu ya Tanzani, yani wizi wote mkubwa katika nchi hii huratibiwa Ikulu tangu Mwalimu Nyerere alipotutoka tu. Polepole anaweza kuwa hajui kwakuwa ameingia juzi kwenye siasa ya nchi hii anafikiri kuongoza ccm ni kuongoza zile NGOs zake za pale Mwenge za utetezi wa haki za mashoga.

Suala lingine alilozungumza Polepole na kujinasibu ni kiongozi wa chama cha watu ni suala la Mauaji ya Kibiti huku akimtisha Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP katika taarifa yake. Na zaidi akajikita kutuhumu vyama vya siasa kwamba vimekaa kimya. Nataka nimkumbushe, vyama vya siasa havijakaa kimya, vyama vya siasa vina platform yake ya kutolea kauli za kitaifa na njia hii havipangiwi na chama kingine yaani chama cha kihalifu ccm,

Mauaji ya Kibiti ni uhalifu mkubwa, una kila elements za kubashiri aina zake, mauaji haya hayahitaji kukurupuka kisiasa, kwakuwa kwakufanya hivyo waweza kujikuta yanageuzwa kuwa matukio ya kisiasa au ya kidini kws vyovyote yanavyoweza kuchukuliwa, Yanahitaji vyombo vya kiuchunguzi ndivyo vishughulike nayo, na sio matamko ya kisiasa kama polepole anavyotaka iwe, wala hayahitaji matamko ya kidini labda katika muundo utakao kutanisha imani zote pawe na sauti moja, nje ya hapo yatajengwa mazingira na kuitwa mauaji ya kidini. Polepole kwa mambo haya ni mchanga, walionyamaza na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi anawaona wapuuzi ile yeye ndiye mjanja na mzalendo,

Nataka nimkumbushe tu katika utawala wake ccm, Anafahamu kwamba Ben Saanane maarufu kama Ben-Rabiu Wa Saanane ni mwezi wa sita huu amepotea/ametekwa? Ipo wapi kauli ya chama chake katika hili?

Anafahamu kwamba Bagamoyo miili saba iliokotwa kwenye viroba ikazikwa pembeni ya mto mithiri ya mbwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Anafahamu kwamba Lugumi imekiuka mkataba wa makubaliano na wizara ya mapolisi juu ya ufungaji ya mitambo ya kielekroniki vituo vya polisi na kampuni hiyo ilishalipws pesa zote kufunga vituo zaidi ya 200 lakini mpaka dakika hii ni vituo vinne tu ndivyo vimefungwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Mnafiki mkubwa huyu..

Manunuzi ya Ndege, ujenzi wa barabara za Mwenge > Moroko, Mwanza Airport nk zimeidhinishwa cha Bunge lipi nchini? Ipo wapi kauli ya chama katika hili yeye akiwa ni msemaji?

Namsihi sana Polepole awe na adabu mbele za Watanzania, Chama cha Mapinduzi katiks suala la madini na mengineyo yote, kabla ya kusimama hadharani na kujitia kuwatusi watanzania kwamba wapuuzi kinatakiwa kutuomba radhi watanzania kwa uhalifu mkubwa na uhujumu uchumi wa nchi yetu tangu 1997 mpaka leo hii...

Polepole alitakiwa jana kuitumia nafasi ile kuliomba radhi taifa kwa chama chake kutubaka bila ridhaa yetu kwa miaka 18 mpaks leo katika raslimali zetu, lakini kwakuwa kijana keshakunywa madaraka ya kulevya basi kaishia kututukana tu huku akijiita ccm mpya.

Na Yericko Nyerere

Yericko lini wewe na wenzako mtajifunza kuwa watanzania siyo wajinga kama mnavyodhani? CCM ni kweli limejaa genge la wezi lakini hilo genge limeanza kusafishwa na kosa mnalolifanya ninyi UKAWA ni lilelie lilowanyima madaraka mwaka 2015 lakini kwa ubongo wenu mdogo mnadhani CCM iliiba kura.

Kama unaandika mpaka vitabu ninadhani umesoma kwa kiwango Fulani lakini nashaurika kusema kwamba huutumii usomi wako vizuri, ni lini mtajifunza kuwa mkiaanza kupinga mambo mlioyapigia kelele miaka karibu 15 na kuyapinga leo wenzenu mnaowaita genge la wezi CCM watatumia mwanya huo????

Wewe, Lissu na Zitto mnadhani mnaiua CCM lakini wanajua hilo ni kweli watu waliojitoa ufahamu kuanzia mwaka 2015 July lakini kwa watanzania wengi nina imani sana hawapo upande wenu. Nilidhani mnaelewa kutumia siasa za matukio kwa manufaa yenu lakini ni bado wepesi. Kilichotakiwa sasa si kuwalaumu CCM mnatakiwa kutuonyesha watanzania kama mpo tayari kuchukua madaraka ya hii nchi kwa kutuambia nini mtafanya katika hili suala badala ya kujaza server kama mlivyofanya miaka 7 iliyopita.....Me just say
 
Nnja na Uroho wa madaraka ndivyo vinavyo mpelekapeleka Polepole.
 
Anadhani kuongoza ccm ni sawa na kuongoza NGO zake pale mwenge
 
Watakuwa wanauelewa ukweli, ila wanachukulia uelewa mdogo wa watz wengi na uoga wetu kutimiza azma yao.
Wapinzani mnasubiri nini kuidai katiba mpya ya rasimu ya Warioba? Vinginevyo nothing will gonna change.

Mi si mpinzani, ni Mtanzania. Sijawahi kuweka imani kwa mtu Mimi kwa sababu ya lable za vyama. Watanzania ni wale wale.
 
Tatizo ni moja Watanzania hawaangalii nini Yericko na wewe mnasema katika mitandao wanachokiona ni kwamba CCM na genge lake la matapeli linaanza kushughulikiwa na hivyo Watanzania watawasamehe kwa hilo na UKAWA wanakosea sana kubeza hii kitu maana ndiyo silaha ya CCM kuwaua tena mwaka 2020 kama mlivyokosea mwaka 2015 kumweka mtu mliyemtukana miaka 7....Me just say

I see ur point, ila mi naongea kama Mtanzania na sio UKawa wala Upinzani. Sijawahi weka imani kwa mwanadamu kwa sababu ya lable za kisiasa, CCM, CHADEMA - Mtanzania ni yule yule.
 
Umejaza hii server ukimsema Lowassa na kutaka watu wamkatae, leo hii unalamba sahani yake. Kama ni kuomba msamaha wewe unatakiwa uwe wa kwanza kuwaomba msamaha Watanzania kwa kuwaamisha unapinga ufisadi kumbe ulikuwa uneweka 'seat' ili ujaze tumbo.

Na pia nikukumbe, CCM ina makosa, tena makosa makubwa, leo dawa haiwezi kuwa chama cha walamba matipishi. Wewe na genge lako mmeonesha kiini cha ugonjwa unalisumbua hili taifa, kwamba watu wanaongea wasichokiamini. Miaka nenda mmelia ufisadi na kuibiwa na makampuni ya madini, leo hii katokeza mtu kuchukua hatua ya kupambana na mafisadi, wewe unakazana kubadilisha 'goal' post na kudeki ili 'wawekezaji' wa kisiasa wamapte maficho.
Magufuli anapambana na 'ufisadi', siyo? Sasa huyo Lowassa bado anafanya nini mtaani? Anapaswa kuwa gerezani sasa, au siyo?
 
Nimemsikiliza jana kijana mwenzangu ndugu Humphrey Polepole akizungumza kwa niaba ya ccm juu ya mambo kadhaa aliyoyaita makubwa nchini, mambo hayo ni mauaji ya Kibiti na Ripoti ya Makanikia.

Nimelazimika kulichambua hili kwa mtindo wa makala kwa nia ya kumkanya na kumwambia Polepole awe na adabu na heshima kwa Watanzania, sisi sio wajinga kama anavyotupimia kipimo alichonacho ambacho ni wanachama wenzake ndani ya ccm.

Nimesikitika kuona kijana huyu anawaita Watanzania ni wapuuza wale tunaounga mkono juhudi za rais huku tukihoji kwamba wizi wote huu katika raslimali umefanywa na Chama cha Mapinduzi, hivyo tukitaka makada wa chama hicho wasimvuruge Rais anapojaribu kupambana na hali hii.

Natataka nimrejeshe nyuma kijana huyu kwa lengo la kumfunza ama kumkumbusha na kisha kumkanya awe na adabu mbele ya umma hasa linapokuja suala la maslahi mapana ya nchi itikadi na mihemko yake iishie viunga vya Lumumba.

Mwaka 1998 wakati makampuni makubwa ya uchimbaji madini ya ASHANTI yalipoingia mikataba na serikali ya Tanzania iliyokuwa chini ya mwenyekiti wa ccm na rais wa Tanzania Benjamin William Mkapa, chama cha mapinduzi kililiridhia kwa kauli moja, serikali yake kuingia mikataba hiyo na kikahubiri hadharani kwamba taifa sasa linanufaika, Hivyo tunapohoji ushiriki na uratibu na unufaika wa ccm katika raslimali za nchi yetu, Polepole anapata wapi kibri chakutuita sisi wapuu?

Kwamfano Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu yote tani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega. Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza dola 370 milioni kuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June 1997). Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, Kampuni hii imeuza dhahabu ya thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni, Muulizeni Polepole kama anafahamu kampuni hii ililipa mrahaba wa shingapi mpaka madini yalipoisha? Haya yote yamefanyika chini ya ccm

Lakini sivyo tu, rejea hansadi za Bunge juu ya hotuba za Upinzani zote tangu bunge la kwanza la vyama vingi, upinzani wamekuwa wakipiga kelele uwazi wa mikataba hii ambayo yote husainiwa Ikulu ya Tanzani, yani wizi wote mkubwa katika nchi hii huratibiwa Ikulu tangu Mwalimu Nyerere alipotutoka tu. Polepole anaweza kuwa hajui kwakuwa ameingia juzi kwenye siasa ya nchi hii anafikiri kuongoza ccm ni kuongoza zile NGOs zake za pale Mwenge za utetezi wa haki za mashoga.

Suala lingine alilozungumza Polepole na kujinasibu ni kiongozi wa chama cha watu ni suala la Mauaji ya Kibiti huku akimtisha Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP katika taarifa yake. Na zaidi akajikita kutuhumu vyama vya siasa kwamba vimekaa kimya. Nataka nimkumbushe, vyama vya siasa havijakaa kimya, vyama vya siasa vina platform yake ya kutolea kauli za kitaifa na njia hii havipangiwi na chama kingine yaani chama cha kihalifu ccm,

Mauaji ya Kibiti ni uhalifu mkubwa, una kila elements za kubashiri aina zake, mauaji haya hayahitaji kukurupuka kisiasa, kwakuwa kwakufanya hivyo waweza kujikuta yanageuzwa kuwa matukio ya kisiasa au ya kidini kws vyovyote yanavyoweza kuchukuliwa, Yanahitaji vyombo vya kiuchunguzi ndivyo vishughulike nayo, na sio matamko ya kisiasa kama polepole anavyotaka iwe, wala hayahitaji matamko ya kidini labda katika muundo utakao kutanisha imani zote pawe na sauti moja, nje ya hapo yatajengwa mazingira na kuitwa mauaji ya kidini. Polepole kwa mambo haya ni mchanga, walionyamaza na kuacha vyombo vya dola vifanye kazi anawaona wapuuzi ile yeye ndiye mjanja na mzalendo,

Nataka nimkumbushe tu katika utawala wake ccm, Anafahamu kwamba Ben Saanane maarufu kama Ben-Rabiu Wa Saanane ni mwezi wa sita huu amepotea/ametekwa? Ipo wapi kauli ya chama chake katika hili?

Anafahamu kwamba Bagamoyo miili saba iliokotwa kwenye viroba ikazikwa pembeni ya mto mithiri ya mbwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Anafahamu kwamba Lugumi imekiuka mkataba wa makubaliano na wizara ya mapolisi juu ya ufungaji ya mitambo ya kielekroniki vituo vya polisi na kampuni hiyo ilishalipws pesa zote kufunga vituo zaidi ya 200 lakini mpaka dakika hii ni vituo vinne tu ndivyo vimefungwa? Ipo wapi kauli ya chama yeye akiwa msemaji? Mnafiki mkubwa huyu..

Manunuzi ya Ndege, ujenzi wa barabara za Mwenge > Moroko, Mwanza Airport nk zimeidhinishwa cha Bunge lipi nchini? Ipo wapi kauli ya chama katika hili yeye akiwa ni msemaji?

Namsihi sana Polepole awe na adabu mbele za Watanzania, Chama cha Mapinduzi katiks suala la madini na mengineyo yote, kabla ya kusimama hadharani na kujitia kuwatusi watanzania kwamba wapuuzi kinatakiwa kutuomba radhi watanzania kwa uhalifu mkubwa na uhujumu uchumi wa nchi yetu tangu 1997 mpaka leo hii...

Polepole alitakiwa jana kuitumia nafasi ile kuliomba radhi taifa kwa chama chake kutubaka bila ridhaa yetu kwa miaka 18 mpaks leo katika raslimali zetu, lakini kwakuwa kijana keshakunywa madaraka ya kulevya basi kaishia kututukana tu huku akijiita ccm mpya.

Na Yericko Nyerere
ACHA KUPOTOSHA UMMA KWA KUROPOKA KAMA KASUKU ASUBUHI
CCM NI CHAMA IMARA CHA KIKOMBOZI TANZANIA UNAPOANZA KUONGEA POROJO ZAKO URUDI NYUMA NA KUANGALIA HISTORIA YA NCHI YETU KWANZA

CCM IMETUTOA MBALI TUACHE AKILI ZA KITOTO KUBEZA KILA LINALOFANYWA NA CHAMA CHA KIKOMBOZI CCM
 
Back
Top Bottom