GE2025 Polepole: Kuna watu wanaodhani wao ni wana-CCM zaidi ya Mwl. Nyerere, wajiangalie sana

GE2025 Polepole: Kuna watu wanaodhani wao ni wana-CCM zaidi ya Mwl. Nyerere, wajiangalie sana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, amesema ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakuna utamaduni wa kuvuana nguo hadharani, bali kuna utamaduni wa kukosoana kwa lengo la kujenga chama.

"Tunakosoana kwenye vikao" haipaswi kutumiwa kuzuia wengine kutoa maoni yao waziwazi, kwani si wote wanashiriki vikao hivyo. Ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa CCM, mfano bora wa kukosoa ulikuwa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Mzee Karume, ambao waliwahi kutoa maoni yao hadharani hata walipoona mambo hayaendi vizuri ndani ya chama.

Polepole amesema haileti maana mtu kujiona ni mwana CCM zaidi ya Mwalimu Nyerere, ambaye mwenyewe aliwahi kukosoa hadharani kwa nia ya kujenga.

Hivi kwanini wanaccm hawatekwi,kuwekwa jela ..kwani huwa hawakosei?
 
Screenshot_20250714-185856~2.png
 
Inashangaza kama watu kama huyu na wengi wengine ndani ya CCM bado hawajui kilichotokea ndani ya chama chao hadi wakati huu!
Anawaambia watekaji wa chama chao, kuhusu 'icon' wa chama? Watu ambao wanadharau na kumkana kabisa huyo 'icon' anayemtambua yeye?

Huku ni kujitia usingizi mwenyewe, ili usiamini kinachoendelea, au ni kujidanganya maksudi tu mwenyewe?

CCM sasa hivi iko mikononi mwa watu ambao hawakukubaliana na Mwalimu Nyerere kwa lolote lile. Walikaa kimya ndani ya chama wakisubiri wakati wao wa kukichukua chama na kukitumia.

Samia sasa yupo kileleni, akiwa sambamba na Kikwete kustawisha dhamira ile ile ya wazee wao.

Ajabu, ni hawa akina Polepole, hilo bado hawalijui? Ni vigumu kuliamini hili.
 
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, amesema ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakuna utamaduni wa kuvuana nguo hadharani, bali kuna utamaduni wa kukosoana kwa lengo la kujenga chama.

"Tunakosoana kwenye vikao" haipaswi kutumiwa kuzuia wengine kutoa maoni yao waziwazi, kwani si wote wanashiriki vikao hivyo. Ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa CCM, mfano bora wa kukosoa ulikuwa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Mzee Karume, ambao waliwahi kutoa maoni yao hadharani hata walipoona mambo hayaendi vizuri ndani ya chama.

Polepole amesema haileti maana mtu kujiona ni mwana CCM zaidi ya Mwalimu Nyerere, ambaye mwenyewe aliwahi kukosoa hadharani kwa nia ya kujenga.

Msoga gang hao
 
Back
Top Bottom