Polepole ashitakiwe kwa uhalifu huu, kama anachosema ni kweli

Polepole ashitakiwe kwa uhalifu huu, kama anachosema ni kweli

Kwa hiyo huo mfumo upo mpaka sasa?

Upo wapi?

Amesema mwenyewe tukathibitishe kama NIDA+INEC+CCM ziko zimeungwa pamoja.

Jiulize wangapi pale CCM na serikalini na tume na NIDA wanajua kuhusu bomu hilo?

KILL THE MESSENGER???

You're joking 😜 obviously!

Mkuu ni wazi unatetea usichokijua.

Wenyewe wakisikia ulichosema wanafumba macho kwa aibu.
Yeye kasema yeye ndiye amehusika kuutengeneza mfumo huo. Kwanini asikamatwe kama mhalifu na kusaidia kufichua wahusika wote?
 
Polepole amesema mwenyewe kuwa yeye na wenzake aliowataja walitengeneza mfumo pale CCM na tume ya uchaguzi unaounganisha tume, CCM na NIDA ili kumsadia Magufuli kushinda uchaguzi 2020 kwa njia nyepesi, na mfumo huo ungetumika pia kama mgombea wake ndiye angeteuliwa kuwania Urais.

Kama kweli hili ni kweli Polepole lazima ashitakiwe kwa uhalifu huu mkubwa kiasi hiki.
Uzuri kaomba msamaha na kaonesha tobo wanalokimbilia panya kujificha..tutalifix
 
Mama Kaburu mkoloni toka Zanzibar alikuwa makamu wa Rais kama wewe ni mpenda kesi kama ccm basi washitaki wote waliokuwa madarakani kwenye utawala wa magufuli
Inawezekana wagombea walikuwa hawajui wanachaguliwaje. Tumlete Polepole kwenye tukio aseme nani alikuwa nani. Kwanza aje athibitishe pasipo shaka kuwa ilikuwa hivyo kweli na aonyeshe mfumo ulipo. Kama ni kweli ana hatia na kama ni uongo ana hatia pia.
 
Samia pia ashtakiwe sababu alishiriki kikamilifu Katika hujuma hizo akiwa mgombea mwenza.

Alinuukuliwa akisema: Hata msipotupigia kura, tutaounda serikali.

Na hapo ndio hasa Msingi ulipo wa kutaka muafaka wa kitaifa kwa kujisahihisha.

Tushuke kumwaga oil.
 
Polepole amesema mwenyewe kuwa yeye na wenzake aliowataja walitengeneza mfumo pale CCM na tume ya uchaguzi unaounganisha tume, CCM na NIDA ili kumsadia Magufuli kushinda uchaguzi 2020 kwa njia nyepesi, na mfumo huo ungetumika pia kama mgombea wake ndiye angeteuliwa kuwania Urais.

Kama kweli hili ni kweli Polepole lazima ashitakiwe kwa uhalifu huu mkubwa kiasi hiki.

Ashitakiwe na nani?

Ukiona wapo kimya ujue ni kweli. Wanajua wakimshitaki wataibua na mengine ambayo hakuyasema.
 
Polepole amesema mwenyewe kuwa yeye na wenzake aliowataja walitengeneza mfumo pale CCM na tume ya uchaguzi unaounganisha tume, CCM na NIDA ili kumsadia Magufuli kushinda uchaguzi 2020 kwa njia nyepesi, na mfumo huo ungetumika pia kama mgombea wake ndiye angeteuliwa kuwania Urais.

Kama kweli hili ni kweli Polepole lazima ashitakiwe kwa uhalifu huu mkubwa kiasi hiki.
Acha kututoa kwenye reli,dhamira ya kufanyq hivyo ikikuwa njema ila maharamia wameigeuza dhamira njema kuwa uharamia.No reform no election.Hatuchomoki kwenye reli,na hatudandanyiki,mwisho wa wizi umewadia.
 
Ndiyo silaha ya mwisho mliyobakiwa nayo! Kufungulia wenye Haki mashitaka ya Uongo! Ambayo mkiambiwa mashahidi ni Samia,Mpango na Majaliwa mnapanic.
Hapa Polepole kasema mwenyewe bila kushurutishwa, na amemtaja Kailima
 
Hyo case haitakubalika, Maana itaichafua vibaya sana SSM, kwa sababu mashahidi lazima waitwe Mwenyekiti wa chams, Katibu wa chama, Mwenyekiti wa Tume na mkurugenzi wa Daftari
 
Nadhani Polepole au wajuzi watoe details ya jinsi mfumo unganishi unavyotumika kuiba kura.
 
Uzuri kaomba msamaha na kaonesha tobo wanalokimbilia panya kujificha..tutalifix
Adhabu ya kutengeneza mfumo haramu na kuutumia sio kuomba msamaha tu bro. Mahakama ndiyo unajua adhabu sahihi kwa kosa hili . Hii kesi haitachukua muda mrefu kwakuwa Polepole kasema mwenyewe kuwa alihusika na mfumo huo.
 
Je kuhusika kwake kunawaondolea hatia watumiaji na wanufaika wa mfumo huo hatari?

Na hii inatuambia nini kuhusu uhalali wa uchaguzi 2025?
Uchaguzi wa 2025 haujatumia mifumo hiyo bado, labda kama bado ipo na wanatarajia kuitumia pia.
 
Polepole amesema mwenyewe kuwa yeye na wenzake aliowataja walitengeneza mfumo pale CCM na tume ya uchaguzi unaounganisha tume, CCM na NIDA ili kumsadia Magufuli kushinda uchaguzi 2020 kwa njia nyepesi, na mfumo huo ungetumika pia kama mgombea wake ndiye angeteuliwa kuwania Urais.

Kama kweli hili ni kweli Polepole lazima ashitakiwe kwa uhalifu huu mkubwa kiasi hiki.
Labda mahakama za kimataifa
 

Wizi wa kura (Vote rigging)​

Wizi wa kura ni udanganyifu wa uchaguzi unaofanywa kwa makusudi ili kubadilisha matokeo. Njia hutofautiana kulingana na iwapo kura zinapigwa kwa karatasi au kwa mfumo wa kielektroniki.

1. Udanganyifu kabla ya kupiga kura​

  • Kuwanyima watu haki ya kupiga kura – kuondoa majina ya wapiga kura fulani kwenye orodha.
  • Vitisho au rushwa – kuwatisha au kuwapa wapiga kura pesa, chakula, au zawadi ili wapige kura fulani.
  • Usajili bandia wa wapiga kura – kuandikisha majina ya watu wasio na uhalisia au waliokufa.

2. Udanganyifu wakati wa kupiga kura​

  • Kujaza kura (ballot stuffing) – kuingiza karatasi za kura za ziada kwenye boksi.
  • Kupiga kura mara nyingi – mtu mmoja kupiga kura mara zaidi ya moja kwa majina tofauti.
  • Kura za posta/absentee ballot bandia – kuiba, kughushi, au kutumia vibaya kura za posta.
  • Kura za kulazimishwa – wapiga kura kulazimishwa kuonyesha wanachochagua au kupiga kura kwa pamoja.

3. Udanganyifu baada ya kupiga kura​

  • Kuharibu au kubadilisha kura wakati wa kuhesabu.
  • Matokeo ya uongo – kutangaza hesabu ambazo haziendani na kura halisi.
  • Vituo hewa – kutangaza kura kutoka maeneo ambayo hayakupiga kura.
  • Udanganyifu wa kielektroniki – kudukua mashine za kupigia kura au kubadilisha takwimu za kidijitali.

4. Udanganyifu wa kimfumo (structural)​

  • Mgawanyo wa majimbo kwa upendeleo (gerrymandering) – kubadilisha mipaka ya majimbo ili upande fulani ufaidike.
  • Udhibiti wa vyombo vya habari – kueneza propaganda za upande mmoja huku ukinyamazisha wapinzani.
  • Matumizi mabaya ya rasilimali za serikali – kutumia pesa, magari, au usalama wa taifa kwa kampeni.
  • Upendeleo wa tume ya uchaguzi – chombo kinachosimamia uchaguzi kupendelea upande mmoja.
 
CCM ndiyo wa kushitakiwa kwa uhaini, kupindua matokeo ya uchaguzi ni kitendo cha uhaini kwa 100%.
Ni lazima Polepole aje athibitishe kwanza kauli yake au uchunguzi ufanywe kuthibitisha hayo. Njia rahisi nini yeye kuthibitisha kauli yake, inawezekana anaropoka tu katika kipindi hiki cha uropokaji na waropokaji. Kuna wakati tuliwahi kuonyeshwa picha za majenerali huko Iran ambao ni ndugu zake Salim Ahmed Salim eti kama akiwa Rais hapa majenerali hao wataiteka nchi
 
Back
Top Bottom