Polepole analipwa mshahara kama Balozi, lakini mpaka leo yuko Dodoma. Watanzania Malawi wanateseka

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,002
20,660
Hivi ni nani anahudumia watanzania kwa huduma za ubalozi? Nani anafanya kazi za Tanzania huko Malawi? Polepole anazunguka tu humu nchini wakati hapo Malawi hata kwa basi la Sauli au Super Feo anafika

Screenshot_20220519-200613.jpg
 
CCM hamuachagi fitna na kusagiana kunguni, labda anafanya harakati apate jimbo kunako 2025. Ukishazoea kulamba asali huwezi kukubali kupelekwa matopeni.

Sisi pangu pakavu ndio tunaona labda huo ubalozi wa malawi ni deal, kwa zile bajeti hamna kitu pale.

Mtu aliyefikia level ya uenezi wa taifa chamani kwenye asali na maziwa! Kule wamempeleka wakamuue kwa stress.
 
Namkumbuka Hayati Mwamba alivyomtingisha Balozi Simba alieteuliwa kuwakilisha Zambia akaanza kuzurura


alikuwa Naibu Katibu mkuu Mambo ya ndani

akateuliwa kuwa Balozi Zambia na Nafasi yake pale ya Naibu KK akapewa Kailima akaanza kila ofisi kuingia kuaga mara znz, mara kwa VP, mara kwa PM…nadhan baada ya Mwamba kuunguruma nadhani alisafiri na magari ya IT
 
Mleta mada ni mpumbavu sana!

Leta ushahidi kwamba hiyo twit ni ya leo
Hata kama ni ya sekunde hii, lazima tukubali kuwa watu humu waache ujuaji na haswa kwa vitu wasivyokuwa na uelewa navyo. Ubalozi ni tofauti na appointment zingine, ubalozi lazima ipelekwe nyaraka ya appointee nchi husika, kisha nchi husika baada ya kujiridhisha iseme sawa aje au asije. Sasa huko kujiridhisha inachukua muda, na watu waelewe nchi anapoenda wanaweza mkataa kutokana sababu kadha wa kadha.
 
Mtoa Uzi ungefanya kwanza utafiti wa taratibu za kidiplomasia zilivyo.
Hawezi kwenda tu kienyeji..lazima apitie mafunzo au kozi fupi ya masuala ya Diplomasia na Itifaki kwa muda wa miezi mitatu au zaidi..vile vile kule anakoenda ni lazima waridhie.
Mengine wataongezea wengine.
 
Watanzania kila siku nasema ni watu wa hovyo sana... vichwa maji...

nazani kama mmemsikia waziri wa ulinzi kuhusu mkakati wanao andaa kumaliza tatizo lililopo kati ya tanzania na malawi ungeelewa zaidi

kwanini usiweke taarifa za mpaka wa tanzania na malawi kuwa tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, kwanini usiulize kuhusu ziwa nyasa kuitwa ziwa malawi hivi sasa?

sasa serikali ina sema wapo katika kulitatua haya kidiplomasia... swala kwa nini yupo dodoma au tanzania lina kuchanganya...

lakini juzi balozi possi alikuwepo hapa tanzania, na dr. slaa alikuwa ana kuja mara kwa mara na alikuwa ana alikwa ktk vyombo vya habari, haya hayakuwa na maana sababu hamuelewi au hatuelewi mabalozi shughuli zao na uwajibikaji wao... na mengine mengi
 
Back
Top Bottom