Humphrey Polepole kuwa Balozi ni promotion, lakini...

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
POLEPOLE KUWA BALOZI NI PROMOTION LAKINI........

Na Elius Ndabila
0768239284

Leo Mhe Rais amemteua Mhe Humphrey Polepole kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Ikumbukwe kuwa Mhe Polepole Kwa siku za hivi karibuni alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya awamu ya sita Kwa alichokiita shule ya uongozi.

Baada ya uteuzi wake kuna mijada inakuja kuwa je Mhe Polepole amepata Demotion au Promotion? Jibu ni Promotion.

Hadhi ya Ubalozi ni kubwa kuliko Ubunge. Ubalozi ni nchi ndani ya nchi nyingine. Hivyo unapokuwa Balozi ni sawa na kuwa wewe ni Mkuu wa nchi kwenye nchi nyingine. Kuwa Balozi kunakupa immunity/ Kinga nyingi kuliko Ubunge. Balozi hata begi lake tu haliruhusiwi kuguswa na mtu yeyote. Kwa tafsiri isiyo rasmi Polepole anaenda kuwa Rais wa Tanzania ndani ya Malawi. Maswala yote yanayohusiana na Diplomasia nchini Malawi yeye ndiye atakuwa kilanja mkuu.

Lakini.......Mhe Polepole amezoea kuongea. Kama atafika Malawi atajisahau akaanza kuongea aliyokuwa anaongea huku basi nafasi yake inaweza kuwa DEMOTION. Inaweza kuwa demotion Kwa kuwa anaweza kuondolewa. Lakini kama atakuwa mtiifu basi hii ni Promotion.

Tafakari
 
Imeniudhi sana, kwa kawaida huwa sipendi mnafiki......atamharibia tu kwa makusudi
 
POLEPOLE KUWA BALOZI NI PROMOTION LAKINI........

Na Elius Ndabila
0768239284

Leo Mhe Rais amemteua Mhe Humphrey Polepole kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Ikumbukwe kuwa Mhe Polepole Kwa siku za hivi karibuni alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya awamu ya sita Kwa alichokiita shule ya uongozi...
Bujibuji nakosa hadi ubalozi wa kadi za X mas.... Yerewuii
 
POLEPOLE KUWA BALOZI NI PROMOTION LAKINI........

Na Elius Ndabila
0768239284

Leo Mhe Rais amemteua Mhe Humphrey Polepole kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Ikumbukwe kuwa Mhe Polepole Kwa siku za hivi karibuni alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya awamu ya sita Kwa alichokiita shule ya uongozi...
Kwanza yeye kakataa kuchanjwa,na Malawi huingii bila kuchanjwa,je atafanyaje?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
huu ni udhaifu wa kiongozi kumfuta siasa kijanja it means slow alikuwa anachoma ushujaaa kauonesha ndani ya chama haijalishi anaenda kufutika au laa.

n sawa na askari anaekufa akiwa vitani.
 
Huko sasa apige kimya,kazi afaidi mema ya nchi.

Nashkuru Mungu kwasasa kazi yangu najiamulia,singoji teuzi wala kutumbuliwa.
 
POLEPOLE KUWA BALOZI NI PROMOTION LAKINI

Na Elius Ndabila
0768239284

Leo Mhe Rais amemteua Mhe Humphrey Polepole kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Ikumbukwe kuwa Mhe Polepole Kwa siku za hivi karibuni alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya awamu ya sita Kwa alichokiita shule ya uongozi...
Diplomasia ya Tanzania na Malawi ni ya kawaida sana, hata ushirikiano wa nchi hizi mbili kiuchumi ni mdogo sana ukilinganisha na nchi nyingine kama Uganda na Kenya. Hivyo Polepole asijidanganye, aendeleee na maisha yake kama awali Mama ndio amesha msogeza kando hivyo, ni muda tu.
 
Atamaliza mkataba baada ya 2025 na hataweza kwa muda huo kumsumbua nmama sawa na Ernest Nchimbi alivyo nyamazishwa
 
Back
Top Bottom