Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,996
- 146,321
Tuna tatizo kubwa sana la kumsikiliza na kumjadili mtu badala ya hoja.POLEPOLE ANAHITAJI MSAADA WA MATIBABU KULIKO KUMSHANGAA
Hivi sasa idadi kubwa ya Watu wameamua kumpuuza polepole kwa kile anachokisema na kukirusha kwenye mitandao kila siku,Sababu ya Wananchi kumpuuza ni kutokana na historia yake wakati wa serikali ya Magufuli
Kwanini Polepole hakumshauri Magufuli asivifungie vyama vya siasa kufanya kazi zao za kikatiba?
Kwanini polepole hakumshauri Magufuli awatafute wahuni waliokua wanabambikia watu kesi na kupora mali zao,wahuni waliokua wanateka,anatesa na kuuwa watu?
Kwanini polepole hakumshauri Magufuli awashughulikie wahuni walipora fedha kwenye mifuko ya hifadhi za jamii na kupelekea wastaafu kukosa fedha zai kwa wakati?
Leo polepole anajikasimisha majukumu mazito ya kujifanya kuitetea CCM na Tanzania bila kutaja jukumi hilo amepewa na nani,kiufupi yani yeye anakijua chama kuliko wajumbe wote wa CCM na ana uchungu na Tanzania kuliko watanzania wenyewe walioamua kumuunga mkono Dkt Samia?
Polepole huyu huyu alikaa kimya alipowasikia wahuni waliojitokeza hadharani kutaka kubadilisha katiba ya Nchi ili kuongeza mda wa ukomo wa Urais Madarakani.Hii inaonyesha wazi walikaa kimya ili kutaka kupima upepo wa Nje ili mda wao waliopanga ukifika watekeleze adhima yao ya kuendelea kubaki madarakani mpaka mda waliokua wamepanga.
Polepole ni mtu wa kupuuzwa hapaswi kusikilizwa hata kidogo na tunajua hawezi kuwa peke yake ni lazima kuna kundi liko nyuma linalompa nguvu na kumficha,Lakini tunasema wakati wa Mungu utafika mda sio mrefu na hukumu ya Mungu itafanya kazi yake.
Kwanza kabisa nataka kukuunga mkono kwamba Polepole ana unafiki mwingi sana, hajanyooka. Ana contradictions nyingi sana zinazomfanya aonekane kuwa mtu anayegombea madaraka zaidi ya mtu anayetaka mapinduzi.
Kwa hiyo nataka kuanza kwa kuonesha kuwa naelewa hilo.
Lakini, hata baada ya kuelewa hilo, hilo halimaanishi Polepole apuuzwe kwenye kila kitu anachosema.
Ukishaelewa hilo, na kusema huyu mnafiki tu anatafuta madaraka, hivyo usiingie kwenye mtego wa kumpa madaraka, unaweza kuchuja hoja zake nyingine ukazikubali (kama hoja, si kama maneno ya Polepole) na ukazitumia.
Kwa nfano, Polepole anaongelea matatizo ya ufisadi, matatizo ya uongozi mbovu, matatizo ya siasa za kuendeshwa na matajiri wachache, hizi zote ni points valid bila kujali anayesema ni nani.
Kwenye mantiki tunatakiwa tuangalie point, si aliyesema point, even a broken clock can be right twice a day. Ukikataa jambo kwa sababu kalisema Polepole unafanya logical fallacy, ad hominem fallacy.
Tuchambue hoja, tusimkubali au kumkataa mtu yeyote kwa style ya "all or nothing at all".
Baada ya kusema hivyo, unaweza kupanga points hapa na kusema katika hili na hili na hili sikubaliani na Polepole kwa sababu hii na hii, lakini katika hili na hili na hili nakubaliana na Polepole kwa sababu hii na hii.
Unaweza hata kukubaliana na hitimisho laPolepole wakati hukubaliani na sababu zilizomfikisha Polepole kwenye hitimisho hilo.
Kwa nfano, mimi nakubaliana na Polepole kuwa Samia kashindwa uongozi na anatakiw akuachia wengine, lakini si kwa sababu za Polepole za kumwaga oil kila miaka kumi, utamaduni ambao haujaandikwa kwenye katiba wala kanuni yoyote. Mimi naona Samia ka hijack mchakato na kaharibu mambo mengi hivyo kakosa sifa za uongozi tu.