Polepole amkimbia Msigwa Azam tv!!

Polepole amkimbia Msigwa Azam tv!!

Olmost

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
340
Reaction score
448
Katika hali ya kushangaza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amegoma kuingia katika kipindi kwenye Televisheni ya AZAM ambapo ilipaswa yeye pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa wajadili kuhusu hali ya uchaguzi ujao wa marudio pamoja na masuala mbalimbali yanayohusiana na Tume ya Uchaguzi.

AZAM TV iliwaalika viongozi hawa wawili leo jumamosi tarehe 14 julai muda wa saa 3.00 asubuhi katika studio zao kwa lengo la kujadili hali ya maandalizi ya uchaguzi wa marudio wa Jimbo la Bunyungu pamoja na kata mbalimbali na pia mjadala ulilenga kujadili suala la Tume ya Uchaguzi pamoja na utendaji wake.

Ambapo Viongozi wote wawili walifika katika studio hizo mapema kabla ya muda na katika hali ya kushangaza ghafla Polepole alipomuona Msigwa akakataa kushiriki katika kipindi hicho kwa madai ya kwamba akujiandaa na pia yeye ahusiki na suala la uchaguzi huo na sio msemaji wa mambo ya Tume ya uchaguzi na hivyo akakataa kushiriki kipindi hicho licha ya jitihada zilizofanywa na wawakilishi wa AZAM za kumshawishi ashiriki kipindi hicho lakini ziligonga ukuta.

Baadaye baada ya mgeni mmoja kukataa kushiriki ndipo Mch. Msigwa akatoa wazo la kushiriki mwenyewe ili aweze kuelezea kwa ujumla kuhusiana na mada hiyo lakini AZAM Tv wakamwambia wataandaa siku nyingine sababu mpangilio wa kipindi cha leo ulikuwa ni pande zote mbili za waalikwa hao ziweze kutoa maelezo na mitazamo mbalimbali kuhusiana na mada hiyo hali iliyopelekea Mbunge Msigwa naye kutopata Nafasi ya kujadili katika kipindi hicho ambacho kiliahirishwa.
 
Escape from sobibor.
Kipindi kikianza utaona haya wakati utataka kuomba madesa wala ruhusa ya kwenda uani.
 
Polepole inapendeza aandaliwe kipindi cha peke yake,maana hana uwezo wa kufanya debate na Msigwa.
Na kadiri siku zinavyokwenda uwezo wake wa kureson mambo unapungua kwa kasi!
 
Tunaomba hata video alivyokiwa akibisha huyo ndugu
 
Sera zake ni za uropokaji ila sio za kujenga hoja sasa kaona ataenda kuaibika amezoea kuita waandishi Lumumba na kuropoka kama mlevi
 
kuishi uongo ni kazi sana, unaweza kuvumilia kuidanganya nafsi yako kwa kipindi fulani tu ila kuna siku uvumilivu utakushinda!!! polepole ukweli utakuweka huru.
 
Nini kimeikumba Azam TWO. Siku ya nne dssa taarifa ya habari ya saa mbili usiku imeota mbawa. Kuna mgomo au wamefungiwa? Any rumours?
 
Pole pole hawezi kukaa na msigwa,alimpa makavu live channel 10 mpaka akaona nyota.
 
Back
Top Bottom