Polepole amkimbia Msigwa Azam tv!!

Polepole amkimbia Msigwa Azam tv!!

*POLEPOLE AMGWAYA MSIGWA AZAM TV*

Katika hali ya kushangaza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amegoma kuingia katika kipindi kwenye Televisheni ya AZAM ambapo ilipaswa yeye pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa wajadili kuhusu hali ya uchaguzi ujao wa marudio pamoja na masuala mbalimbali yanayohusiana na Tume ya Uchaguzi.

AZAM TV iliwaalika viongozi hawa wawili leo jumamosi tarehe 14 julai muda wa saa 3.00 asubuhi katika studio zao kwa lengo la kujadili hali ya maandalizi ya uchaguzi wa marudio wa Jimbo la Bunyungu pamoja na kata mbalimbali na pia mjadala ulilenga kujadili suala la Tume ya Uchaguzi pamoja na utendaji wake.

Ambapo Viongozi wote wawili walifika katika studio hizo mapema kabla ya muda na katika hali ya kushangaza ghafla Polepole alipomuona Msigwa akakataa kushiriki katika kipindi hicho kwa madai ya kwamba akujiandaa na pia yeye ahusiki na suala la uchaguzi huo na sio msemaji wa mambo ya Tume ya uchaguzi na hivyo akakataa kushiriki kipindi hicho licha ya jitihada zilizofanywa na wawakilishi wa AZAM za kumshawishi ashiriki kipindi hicho lakini ziligonga ukuta.

Baadaye baada ya mgeni mmoja kukataa kushiriki ndipo Mch. Msigwa akatoa wazo la kushiriki mwenyewe ili aweze kuelezea kwa ujumla kuhusiana na mada hiyo lakini AZAM Tv wakamwambia wataandaa siku nyingine sababu mpangilio wa kipindi cha leo ulikuwa ni pande zote mbili za waalikwa hao ziweze kutoa maelezo na mitazamo mbalimbali kuhusiana na mada hiyo hali iliyopelekea Mbunge Msigwa naye kutopata Nafasi ya kujadili katika kipindi hicho ambacho kiliahirishwa.
Source; FB
 
Huyu mwandishi anajifunza uandishi wa propaganda ila hajui. yaan unatufanya watu wote humu tuna mawazo ya kiwango cha chini. taarifa haijabalance 5W hata kidogo, SIKU NYINGINE UKIONA KITU FB KIACHE USIPELEKE HUMU JF,
 
Wameeanza kutimua mbio mapemaa hivi...... Msigwaa alikua kaja na upako..😀😀😀😀. Polepole anatunza sahani yake. Ya ubwabwa. Lolote laweza tokea
 
Huyu mwandishi anajifunza uandishi wa propaganda ila hajui. yaan unatufanya watu wote humu tuna mawazo ya kiwango cha chini. taarifa haijabalance 5W hata kidogo, SIKU NYINGINE UKIONA KITU FB KIACHE USIPELEKE HUMU JF,
Pokea hvyo hvyo hiyo taarifa!
 
Huyu mwandishi anajifunza uandishi wa propaganda ila hajui. yaan unatufanya watu wote humu tuna mawazo ya kiwango cha chini. taarifa haijabalance 5W hata kidogo, SIKU NYINGINE UKIONA KITU FB KIACHE USIPELEKE HUMU JF,
Pokea hvyo hvyo hiyo taarifa!
 
Wewe subiri kichapo Jimboni Bunyungu...na kata zote halafu tutakutana hapo hapo Azam
 
Aisee! Huenda siku hizi anafikiri polepole kama lilivyo jina lake, otherwise sioni sababu ya kukimbia...
 
Hiyo ni taarifa ndugu,mbona umepanic hivi?Muulize Polepole kama ni kweli aligoma kushiriki kipindi
hapana mkuu sijapanic, i have to correct where i see problem, mantiki yangu kuonyesha upungufu tu kwamba habari yako imekosa kitu kinaitwa 5W, 5W ni taaluma katika uandishi ambayo ndio hutoa uahalali wa habari yoyote unayoiona au kuskia.
 
Polepole sio mtu wa kumkimbia mchungaji Msigwa labda yuko bize.
 
Back
Top Bottom