mfumo ndo unanipelekea nifanye hivyo, kama mapenzi yasingekuwa ya kidigitali hata nisingethubutu, ningesubiri nioe mama, lakini tatizo ndoa za siku hizi ni majanga, natamani ningewahi kuzaliwa enzi zenu ili nifahidi yale mapenzi ya kweli, mapenzi yaliyokuwa yakijali utu, vigezo vilikuwa ni uchapakazi tu, enzi ambazo wapendanao walikuwa na malengo ya dhati na mahusiano yao, tofauti na saa hizi ambapo mabinti saa nyingine hulazimisha ndoa kisa rafiki zake wameolewa, siku hizi mama mabinti hawawataki vijana wenzao wanataka wazee kisa wanawapa pesa, vijana bado tuantafuta na wao hawatutaki wanasema si wababaishaji hatuwezi kuwanunulia magali, yaani tena ukija na hii kitu inaitwa haki sawa wanavyoichukulia ndivyo sivyo ndo inafanya mahusiano yawe magumu zaidi maana mafahari wawili hawakai zizi moja mama.