Najua na nimelisema hilo kuwa hakuna kitendo ambacho kinahalalisha alichofanya huyo dada.lakini tatizo latu mara nyingi tunaangalia tulipoangukia na sio tulipojikwaa,inawezekana kabisa huyu dada kilichomfanya akafanya haya ni matokeo ya mateso,yes inawezekana alitakiwa kuondoka tu,je unajua kama hata njia ya kwao anaijua?
Kuna wadada wengine wanachukuliwa huko na kuja kupatiwa makazi kama haya na wanakuwa kama wapo kisiwani tu na hawana cha kufanya,lakini pia hata kama kingekuwepo cha kufanya kwa maana ya kuondoka,yule dada ni binadamu kama wengine,ukifanyiwa ubaya na ukatili kunakuwa na hali ya kutamani kisasi,hiyo ni kawaida kwa binadamu,mara nyingi huyu dada aaliona hawezi kuwaadhibu waajiri wake [kama walimfanyia ubaya] na aliona mnyonge wake ni huyu mtoto masikini ya Mungu]
Huyu mtoto anakuja kuwajibika kwa makosa ya waajiri wake,binti akaamua kumfanya alivyofanya,lengo langu sio kumuondoa huyu binti hatiani bali kujaribu kuangalia wengine ambao walisababisha hili tukio kwa namna moja au nyingine nao kuwajibika na sio kumfanya huyu binti mbuzi wa kafara na kumfanya ndio shetani kuliko shetani mwingine ambae anazunguka tu kwa raha zake na ndio aliyesababisha kwa hakika tukio hili!