NIMPENDENANI
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 6,114
- 5,397
Yani kwa hapo huyo bint amekosea ange deal na wazazi sio mtoto,na hakulazimishwa kazi ukiona sehemu kuna mateso unaondoka atakua ana mamtatizo ya akili sio bure.....
Mkuu hii kitu inaniuma sana
Binadamu tumefikia kiwango cha hatari sana cha kuona kama sisi ni binadamu lakini wengine asio binadamu .....
Aaaaaaahhhhh ......!!
"mabosi" wengi huwa ni wakatili kuliko tunavyodhani. Hawa hawa wanaolaani kitendo cha huyu dada kumfanyia unyama malaika huyu, wengi ni wakatili tena kupitiliza kwa wasaidizi wao majumbani huku wakiwalipa as low as 20,000tsh kwa mwezi, huku wakifanyishwa kazi kuliko punda. Hayo nimewahi kuyashihudia.
chochote kile haki-justify kitendo alichofanya yule dada.....kama aliona mateso yamezidi angeondoka,wapo madada wengi tu wanateswa mwisho wanatoroka au wanaomba kuondoka.....kitendo alichofanya ni cha kinyama na anastahili adhabu kali.
chochote kile haki-justify kitendo alichofanya yule dada.....kama aliona mateso yamezidi angeondoka,wapo madada wengi tu wanateswa mwisho wanatoroka au wanaomba kuondoka.....kitendo alichofanya ni cha kinyama na anastahili adhabu kali.
Sawa .....Kulaani kitendo alichofanyiwa innocent victim ni reaction ya kibinadamu.
Tatizo la kwanza linaonekana hapa,sijabase kokote ila nataka kila mmoja alione tatizo kwa mapana yakekujiuliza how na why inakuja baadaye sana. Na kama wewe ambavyo umeamua kubase upande wa msichana wa kazi mimi na wengine wengi tumeamua kujikita kwanza kwa innocent victim.
Kutokuwepo kwa mtu ambae asingekuwa mnyama hakuhalalishi unyama alioufanya huyo mwajiri wake na inawezekana tatizo limeanzia kwake ...Tunazo facts mezani ambazo ni mtoto kateswa kwa vipigo ambavyo ni vya kuua. Na pia reaction ya mzazi baada ya kukutana na hiyo fact, kweli mzazi aligeuka mnyama pia lkn nani asingegeuka mnyama kwa hali ilivyokuwa?
Sio njia sahihi na ndio maana nimesema kuwa sheria ichukue mkondo wake,lakini ni kwanini hamjadili kama aliteswa huyo mtesaji nae achukuliwe hatua?speculation ni kuwa binti ameteswa sana na kuamua kumalizia hasira zake kwa mnyonge (innocent victim ). Je ni njia sahihi kufanya aliyoyafanya?
Swali hili muulize huyo mwajiri wake kuwa baada ya kuona hilo tukio ni kwanini asingeenda polisi na akaamua kujichukulia sheria mkononi?wanaokutwa na hali kama hiyo hufanya nini? Kwanini asiondoke au asiende police?
Sawa lakini pia waliolianzisha nao wachukuliwe hatua ...Suala la kumalizia hasira waliodhaifu kuliko wewev sio jema kabisa. Nakumbuka mama alishanipiga sana kisa ameudhiwa na mama mkwe wake na wifi zake, of recent nilimkumbushaa au umeudhiwa kazini unakuja mpiga mkeo sio fair.
Sawa .......!!Anger management inahitajika kwa watu wengi. Yes binadamu anaweza kuwa shetani inahitaji trigger ndogo tu. So yule binti jwa wakati ule alikuwa shetani, na baba mtoto alikuwa shetani pia.
No one is trying to justify it, at least not Eiyer.
But at the same time it would be remiss to ignore the fact that most of those maids are maltreated by their bosses.
So if we are going to condemn the cruelty of the maids let's also condemn in equal measure, the cruelty of the bosses.
It's only fair.
THATS A NO-BRAINER....but what about those maids who are not mistreated but still end up abusing toddlers???
Pamoja na haya uliyosema bado unamuweka mwajiri kwenye hatia,mwenye jukumu la kukagua ni mtu wa aina gani anamuajiri ni mwajiri na sio mwajiriwa,kama utaajiri kichaa wewe iliemuajiri ndio unapaswa kuanza kupatiwa kibano kabla ya huyo kichaa uliemuajiriumemtazama dada kwa jicho ulilomtazama yule aliyekupa kisa chake. Pole anatakiwa kupewa mtoto na si kuhalalisha ukatili kwa mtoto, ila si vibaya kutoa angalizo kwa namna tunavyowafanya wafanyakazi wa ndani. Dada wa kazi anaweza kuwa na ugonjwa wa akili ukalipuka siku isiyojulikana. Wapo wadada wa kazi wanaoteswa lakini hawawakatili watoto. Wapo ambao hawateswi na waajiri ila wana visirani vinavyotokana na sababu nyingi zikiwamo za kimapenzi - kaachwa na bwana basi hasira kwa mtoto. Wengine wanafanya hizi kazi kwa sababu hawana namna, wamefungashwa na wazazi kuja mjini. Hata uwape nini bado wananuna tu na kazi wanafanya wanavyotaka. Unabembeleza housegirl mpaka unajishtukia. Nimeshakutana nao. Kwa hiyo sababu za ukatili wa wadada wa kazi nyingi.
Kesi hii ni kesi ambayo nayo ina historia yake,kuishi vizuri na hawa wadada sio kuwapa chakula na malazi tu,unatakiwa uwe rafiki yake na ujaribu kuwa kama mama,dada au hata rafiki yake wa karibu sana ili uweze kuzungumza nae na aweze kukuambia shida zake nyingiNimewahi kuwa na housegirl mkatili kwa mtoto. Hakuwahi kuonyesha kuwa na roho mbaya. kwa miezi mitatu aliyokaa nilijitahidi kumpa mahitaji yote muhimu. Anakula ninachokula mimi jioni, mchana anakula anachotaka yeye maana sipo. Analala kwenye chumba chake mwenyewe na malazi ni masafi. Jumapili anaenda anakojua yeye kwa mapunziko. Jumapili moja akanirudia saa 5 usiku. Nikauliza kulikoni nikadanganywa nilivyodanganywa maisha yakaendelea.
Mtoto wangu wakati huo akiwa na mwaka na miezi 3 alikuwa mbishi wa kula na kulala. Yule dada akawa ananiambia wewe anakusumbua sana. Mimi wala hanisumbui. Nikachukulia watoto wote hudeka wakiwa na mama zao. Kuna kipindi nikawa nikirudi home mtoto anaenda jikoni ananiletea kiboko usawa wa rula hivi. Wakati huo hawezi kuongea vizuri. Ananionyesha kile kiboko lakini nilivyokuwa mpuuzi hata sikufikiria kama kilikuwa kinamhusu. Siku moja nikiwa namnyonyesha akawa anapeleka sana mkono makalioni. Wakati nambadilisha diaper nakuta kuna mstari umevimba. Nikashangaa, nikamwita dada kumuonyesha akaniambia labda mdudu. Nikajiuliza huyu mdudu gani anapita kama rula. Kwa umri wa mtoto na upole wa dada sikuwaza habari ya kuchapwa. Siku ya siku jirani akaniita na kunipa habari kuwa mtoto wangu anachapwa sana na msichana wa kazi. Sikuwa na sababu ya kubisha maana dalili nilishaziona nikapuuza. Nikarudi nyumbani nikamtimua yule binti.
Kutokana na huo uzoefu wangu siwezi kusema moja kwa moja kuwa mayaya wanakatili watoto kwa sababu nao wakakatiliwa na waajiri. Mwajiri anaweza kumlamba miguu yaya na bado yaya akafanya vituko. Ukatili hutokana na "frustration" inayotokana na mtu kutofikia malengo yake fulani. Tuliangalie hili swala kwa upana zaidi. Ila kama mnataka tuangalie sababu moja ya waajiri, sawa.
Najua na nimelisema hilo kuwa hakuna kitendo ambacho kinahalalisha alichofanya huyo dada.lakini tatizo latu mara nyingi tunaangalia tulipoangukia na sio tulipojikwaa,inawezekana kabisa huyu dada kilichomfanya akafanya haya ni matokeo ya mateso,yes inawezekana alitakiwa kuondoka tu,je unajua kama hata njia ya kwao anaijua?
Kuna wadada wengine wanachukuliwa huko na kuja kupatiwa makazi kama haya na wanakuwa kama wapo kisiwani tu na hawana cha kufanya,lakini pia hata kama kingekuwepo cha kufanya kwa maana ya kuondoka,yule dada ni binadamu kama wengine,ukifanyiwa ubaya na ukatili kunakuwa na hali ya kutamani kisasi,hiyo ni kawaida kwa binadamu,mara nyingi huyu dada aaliona hawezi kuwaadhibu waajiri wake [kama walimfanyia ubaya] na aliona mnyonge wake ni huyu mtoto masikini ya Mungu]
Huyu mtoto anakuja kuwajibika kwa makosa ya waajiri wake,binti akaamua kumfanya alivyofanya,lengo langu sio kumuondoa huyu binti hatiani bali kujaribu kuangalia wengine ambao walisababisha hili tukio kwa namna moja au nyingine nao kuwajibika na sio kumfanya huyu binti mbuzi wa kafara na kumfanya ndio shetani kuliko shetani mwingine ambae anazunguka tu kwa raha zake na ndio aliyesababisha kwa hakika tukio hili!
Binti awajibike kwa tatizo lake na kama hao waajiri wa huyo binti wana matatizo yao na kimsingi kama yapo ndio yatakuwa chanzo basi nao wawajibike kama binti anavyowajibika kwa kupakwa matope na kuonekana kama sio binadamu
Sio njia sahihi na ndio maana nimesema kuwa sheria ichukue mkondo wake,lakini ni kwanini hamjadili kama aliteswa huyo mtesaji nae achukuliwe hatua?
Swali hili muulize huyo mwajiri wake kuwa baada ya kuona hilo tukio ni kwanini asingeenda polisi .!!
Yani kwa hapo huyo bint amekosea ange deal na wazazi sio mtoto,na hakulazimishwa kazi ukiona sehemu kuna mateso unaondoka atakua ana mamtatizo ya akili sio bure.....
Then they are what they are, period, end of sentence.
I'm all about fairness.
*Please, instead of toddlers let's use (young) children*
Umenena Eiyer! Nilipo ona hile video kwa Mara ya kwanza nilisikitika sana na ni video ambayo siwezi kurudi kuangalia maana inasukitisha sana mtoto kufanyiwa vile!
Lakini baadae nilianza kujenga picha juu ya hili tukio!
Kwanza ningekuwa Mimi cha kwanza ninge hitaji apimwe akili yule binti Maana nilijenga picha ya mtu mwenye tatizo la akili!
Pili nilijenga picha ya binti wa kazi anaye teswa sana na wenye nyumba hivyo analipiza kisasi kwa mtoto wa wanao mtesa na kumnyanyasa!
Pia nilijenga picha yakuwa huyu binti huteswa sana na Mama mwenye nyumba kiasi kwamba amepata tatizo la kisaikolojia na la kiakili maana tumezoea ni kawaida Wamama walio wengi kuwanyanyasa wafanyakazi!
Kwakweli nilikosa jibu nilipo pata taarifa kuwa huyu mtoto alikuwa anaishi na baba yake pamoja na housegirl tuu!
Bado niliendelea kujiuliza ni lini Mama mwenye nyumba aliachana na Mumewe kama walishawai kuishi pamoja?
Mama mwenye nyumba hakuwai kuishi na huyu binti wa kazi kabla ya kuondoka?
Nini hufanyiwa huyu mfanyakazi na Baba mwenye nyumba na wana maahusiano gani na mfanyakazi?
Nilijiuliza hayo Maswali kwakuwa asilimia 99% ya mateso ya wadada wa kazi huyapata kwa wa Mama wenye nyumba!
Na kuhakikishia kabisa kati ya wanawake 100 ni wanawake 3 wanaweza ishi na wafanyakazi wa ndani kama watu muhimu kwao!
Katika hili ni wazi kabisa kuna sababu za msingi kabisa yule mfanyakazi kufanya yale kama itathibitika hana tatizo la kisaikolojia au la kiakili! Wafanyakazi wandani wananyanyaswa sana tena uzuri Mimi nimeshuhudia sana hili lakini ukisema unaonekana una interest!
Yani unakuta hawapewi muda wa kupumzika na mshahara bado mdogo na wengine wana kopwa kabisa hadi mshahara!
Wafanyakazi hawa wanateswa sana na wanao watesa ndio hao hao huwa wakwanza kusema wana uchungu sana na huruma sana kumbe ni unafiki tuu!
Kwakweli kitendo alicho mfanyia mtoto hakikubaliki lakini kwa upande mwingine hawa watu nao hupata mateso sana kwa sisi wenyewe tunao laani kitendo chake!
Yani kwa hapo huyo bint amekosea ange deal na wazazi sio mtoto,na hakulazimishwa kazi ukiona sehemu kuna mateso unaondoka atakua ana mamtatizo ya akili sio bure.....