Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,801
- 43,177
Hakika....hata mimi nliongea hivyo. Mtu hawezi kuwa na roho mbaya kiasi kile from nowhere. Ipo namna tu sio bure
Habari za asubuhi.
Tukio lililotokea siku sio nyingi huko Uganda na kusambaa kutokana na maendeleo ya mawasiliano limewastua wengi hasa wanawake kwakuwa ni wazazi,lakini hata wanaume nao limewastua sana na kupelekea kuanza kuwa na hofu kuhusu usalama wa watoto wao ambao wanalelewa na hawa ma housegirl.
Tukio hili kwa bahati mbaya sana watu wamelitazama kwa upande mmoja tu na hii inasababishwa na tabia ya kibinadamu ya umimi,nasema hivyo kwasababu kwa sasa najua kuna namba kubwa sana ya watu ambayo in amuona yule dada kama mnyama na hastahili kabisa kuishi na wengine wanatamani hata angekuwa tayari ameshauwawa kwasababu ya kitendo ambacho amemfan yia yule mtoto,huu ni unafiki.
Nasema ni unafiki kwasababu kwenye tukio hili na matukio mengine binadamu tumejipachika utakatifu na kujiondoa kwenye madhambi pengine makubwa zaidi kuliko hata alilofanya huyu dada,lakini kikubwa zaidi dada yule ameonekana kama yeye tu ndio mwenye tatizo.
Kimsingi binadamu ambae amekamilika kiakili hawezi kufanya jambo kama lile na kama atafanya ni lazima kutakuwa na sababu nyuma ya alichokifanya.leo hii ni vigumu kukutana na mtu ambae hajui kabisa madhila ambayo wanakutana nayo hawa wadada wa kazi huko kwenye majumba wanamoishi,kuna dada mmoja ambae niliwahi kukutana nae na kuniambia maswahibu ambayo anakutana nayo huko anakofanya kazi hadi nililengwa na machozi.
Dada huyu anasema hajawahi kununuliwa nguo bali zile nguo ambazo zinachakaa za watoto wa mwajiri wake ndio anapewa kuvaa,zile ambazo zinawabana watoto hao na zinakuwa bado ni nzuri hapewi na hutafutwa namna nyingine ya kufanywa na hata wakati mwingine kupelekwa kwa watoto wa ndugu zao,binti huyu anasema kuwa hajawahi kukaa mezani kula pamoja na mwajiri wake na kila siku yeye huwa wa mwisho kula na wakati mwingine hulazimika kula makombo kwani kuna wakati chakula huisha na kwakuwa haruhusiwi kula pamoja na wanafamilia na c hakula kinapokuwa ni kidogo hulazimika kula makombo ya mabosi wake.
Dada huyu anasema kuwa pamoja na wakati mwingine kutokula chakula ambacho anakinunua mwenyewe na kukipika anasema siku akichelewesha chakula basi huambulia kufokewa na wakati mwingine ananyimwa chakula na kuna wakati hata hulala nje ya nyumba kwani mama mwenye nyumba humfungia nyumba kwa sababu ya kosa fulani tu.Dada huyu akaniambia kuwa kuna siku aliunguzwa mkono wake kwasababu tu alipoteza sh 500 ambayo alirudishiwa sokoni baada ya kyhemea vitu vya nyumbani.
Hayo ni kwa ufupi tu,yapo makubwa zaidi ya hayo na wengine hufikia kudhalilishwa kabisa na waajiri wao,kwasababu hawa watu wanaishi kwenye majumba na hakuna ambae wanaweza kumuambia angalau kupu nguza hasira ambazo wanakuwa nazo wameishia kutukutia ndani kwa ndani na kilichotokea Uganda ni mfano wa hili.Hakuna mtu ambae nimemsikia akijaribu kutazama upande wa pili wa shilingi ili kuona hasa tatizo limeanzia wapi.
Siungi mkono kile ambacho dada yule amekifanya na kinahitaji adhabu,lakini kumuona dada yule kama shetani wakati kuna shetani mwingine anadunda tu na ndie huenda amesababisha yote hayo sio jambo na kibinadamu.Kama nilivyosema hapo juu, ni vigumu sana kwa binadamu ambae yuko timamu kabisa kufanya kitendo kama kile lakini kama akifanya ni lazima kunakuwa na sababu nyuma ya hilo,kwanini hatuangalii kile ambacho kinaweza kluwa kimemsababisha huyu binti kufanya alichokifanya?
Binti yule sio kichaa,nasema hivyo kwasababu kama angekuwa na tatizo hilo sidhani kama hao waajiri wake wangekuwa wameishi nae kwamuda wote ambao wameishi nae,kwasababu hiyo sasa huyu binti ni mzima kabisa kiakili,sasa je ni kwasababu gani amefanya vile? Hili ni swali ambalo mtu yoyote yule mwenye utimamu wa akili na ubinadamu anatakiwa ajiulize lakini kwasababu sisi ni wanafiki hatujiulizi kwasababu tunayaogopa majibu ambayo yatakuja na kutuumbua.
Hivi ni nani anajua kama huyu binti amekuwa akipata mateso maku bwa sana hapo kwenye hiyo nyumba? Sisemi kuwa kama alipata mateso bali ni halali kwake kufanya hivyo lakini kujua hili angalau tunaweza kuona kuwa mwenye kuonwa ni shetani sio huyu binti pekee bali kuna mwingine au wengine.
Mateso ambayo wamekuwa wakikumbana nayo hawa wadada wa kazi ni ya kutisha na kama tunavyojua kuwa binadamu anapoteswa hutafuta namna ya kulipiza kisasi na pale ambapo anakuja kuona kuwa mhusika anaemtesa hawezi kumlipizia kisasi kwasababu huenda akawa ni tajiri basi mhusika hutafuta wanyonge wake ambao mara nyingi kwa hawa wadada wa kazi huwa ni wale wanaowalea na haya yaliyotokea ni matokeo ya haya.
Huyu dada hajapewa kabisa nafasi ya kujitetea na sidhani kama atapata,hili nalisema kwakuwa nasikia kwanza amepewa kipigo kikali sana na mwajiri wake na polisi walipokuja kumkamata huyu mwajiri aliwaonesha video na walimuachia,tatizo ambalo hata hawa mapolisi wa Uganda nao walishiondwa kufikiri kwa namna ya kibinadamu [kama kweli walimkamata na kumuachia] na wao waliona huyu mwajiri ana haki ya kumuadhibu huyu dada kwa kitendo kile,kitu ambacho sio sahihi kabisa.
Ifikie mahali tuwe na utu hata angalau kidogo,watu kama huyu dada hawana mtu wa kuwaambia madhila wanayokutana nayo na hiyo imewasababisha kufanya mambo ya ajabu kama haya,kwa wenzetu kuna vitengo vya kufatilia matukio kama haya na inafikia mahali uchunguzi hufanyika na hatimae kila mtu kubeba adhabu stahiki,kama mwajiri wake anahusika na kumnyanyasa huyo dada na kuna wakati hufikia hawa wadada kubakwa na waajiri wao,ni nani atawawajibisha hawa waajiri wa huyo dada wakati hawampi nafasi hata ya kujitetea?
Kama huyu dada ni shetani,hawa waajiri ambao wanawanyanyasa hawa wasaidizi wao wa ndani hadi wanawaathiri kisaikolojia watakuwa nani? Nani anawapa kipaza sauti hawa wadada na kuwapa nafasi ya kusema kile ambacho wanakutana na cho huko majumbani mwetu?
Binadamu tuna safari ndefu sana hadi kufikia kujitambua na kuacha unafiki huu,najua huyo dada yupo kwenye wakati mguu sana sasa,lakini naamini Mungu atam saidia,kitendo alichomfanyia yule mtoto hakikubaliki na sheria ichukue mkondo wake lakini kama hawa waajiri wake ambao naamini watakuwa wamehusika na madhila yaliyompata mtoto wao nao wana chao cha kujibu mbele ya sheria,haiwezekani tukio hili liachwe hivi hivi tu na mnyonge aadhibiwe peke yake
Haikubaliki
Hujaeleweka .....!!
To who?
well said.umemtazama dada kwa jicho ulilomtazama yule aliyekupa kisa chake. Pole anatakiwa kupewa mtoto na si kuhalalisha ukatili kwa mtoto, ila si vibaya kutoa angalizo kwa namna tunavyowafanya wafanyakazi wa ndani. Dada wa kazi anaweza kuwa na ugonjwa wa akili ukalipuka siku isiyojulikana. Wapo wadada wa kazi wanaoteswa lakini hawawakatili watoto. Wapo ambao hawateswi na waajiri ila wana visirani vinavyotokana na sababu nyingi zikiwamo za kimapenzi - kaachwa na bwana basi hasira kwa mtoto. Wengine wanafanya hizi kazi kwa sababu hawana namna, wamefungashwa na wazazi kuja mjini. Hata uwape nini bado wananuna tu na kazi wanafanya wanavyotaka. Unabembeleza housegirl mpaka unajishtukia. Nimeshakutana nao. Kwa hiyo sababu za ukatili wa wadada wa kazi nyingi.
Nimewahi kuwa na housegirl mkatili kwa mtoto. Hakuwahi kuonyesha kuwa na roho mbaya. kwa miezi mitatu aliyokaa nilijitahidi kumpa mahitaji yote muhimu. Anakula ninachokula mimi jioni, mchana anakula anachotaka yeye maana sipo. Analala kwenye chumba chake mwenyewe na malazi ni masafi. Jumapili anaenda anakojua yeye kwa mapunziko. Jumapili moja akanirudia saa 5 usiku. Nikauliza kulikoni nikadanganywa nilivyodanganywa maisha yakaendelea.
Mtoto wangu wakati huo akiwa na mwaka na miezi 3 alikuwa mbishi wa kula na kulala. Yule dada akawa ananiambia wewe anakusumbua sana. Mimi wala hanisumbui. Nikachukulia watoto wote hudeka wakiwa na mama zao. Kuna kipindi nikawa nikirudi home mtoto anaenda jikoni ananiletea kiboko usawa wa rula hivi. Wakati huo hawezi kuongea vizuri. Ananionyesha kile kiboko lakini nilivyokuwa mpuuzi hata sikufikiria kama kilikuwa kinamhusu. Siku moja nikiwa namnyonyesha akawa anapeleka sana mkono makalioni. Wakati nambadilisha diaper nakuta kuna mstari umevimba. Nikashangaa, nikamwita dada kumuonyesha akaniambia labda mdudu. Nikajiuliza huyu mdudu gani anapita kama rula. Kwa umri wa mtoto na upole wa dada sikuwaza habari ya kuchapwa. Siku ya siku jirani akaniita na kunipa habari kuwa mtoto wangu anachapwa sana na msichana wa kazi. Sikuwa na sababu ya kubisha maana dalili nilishaziona nikapuuza. Nikarudi nyumbani nikamtimua yule binti.
Kutokana na huo uzoefu wangu siwezi kusema moja kwa moja kuwa mayaya wanakatili watoto kwa sababu nao wakakatiliwa na waajiri. Mwajiri anaweza kumlamba miguu yaya na bado yaya akafanya vituko. Ukatili hutokana na "frustration" inayotokana na mtu kutofikia malengo yake fulani. Tuliangalie hili swala kwa upana zaidi. Ila kama mnataka tuangalie sababu moja ya waajiri, sawa.
Una uwezo wa kujua kile ambacho mwingine anafikiri?