Pole PakaJimmy

Wanabodi,
Nianze kwa kumshukuru sn mdau pmwasyoke kwa kuwajuza wanajamvi.
Hakika namshngaa mdau huyu, maana simfahamu ambapo yaelekea yeye ananijua vyema. Anyway, JF ni pana sana na yawezakuta ni jamaangu wa karibu.
Ni kweli kabisa wadau nimepata msiba wa baba mkwe wangu na hv sasa ndio naingia mbuga ya Mikumi nikiwahi mazishi hapo kesho. Nawashukuru sana kwa POLE zenu, na niombeeni nifike salama.

Pole sana PakaJimmy Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani. Nakutakia kila la kheri kwenye safari yako na mazishi yote kwa ujumla. Mungu awalinde
 
Last edited by a moderator:
Mkuu pole sana, nilipokiwa guest nilikuwa nakuona sana jukwaani ukitoa hoja za nguvu sana kwa mantiki hiyo nikatokea kukubali. Pole sana mkuu.
 
Mkuu PJ pole sana kwa msiba Mungu akupe moyo wa subira na ampe mkeo moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Mungu yu mwema na mipango yake haina makosa... RIP Baba Mkwe wetu.
 
Wakubwa, kwa wale wanaojua vyema njia ya MOro-Iringa sasa ndio tunaanza Mlima Kitonga. Nashukuru mno kwa sala zenu, maana tunazidi kusonga.
 
Poleni sana, wewe, pamoja na wifi yetu. Na ndugu na jamaa wote walioguswa na na msiba huu. Mungu akawape faraja za mioyo, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha msiba. Safirini salama pia.
 
Shughli ya Mazishi ya Marehemu Mkwe wanngu Jonas CHristopher Mwadende hapo kesho itaanza kwa Misa katika kanisa la RC MWANJELWA au wengine wanaita kanisa la HIJA, MUDA WA saa 4asbh, na kisha mazishi yatafanyika muda wa saa 6mchna katika eneo la UYOLE Iduda.
Aidha msiba uko eneo la Isanga.
Kwa wadau wa Mby karibuni sn tushiriki na Mungu awab ariki.
 
Pole sana Paka Jimmy.
Tunamuombea marehemu malazi mema na wafiwa Mwenyezi Mungu awape nguvu na subira.
 
Back
Top Bottom