Pole kwa watanzania ambao hela imewakataa

ni sahihi 2021 nilipata kazi ila 2025 MUNGU akanijalia kwenda nje ASIA halafu nikapewa kibali wakataka nifanye nao kazi sana ila nachomuomba Mungu cha mwisho nisaidie nipate kazi mashirika ya kimataifa hiko ndo cha mwisho kabisa na hakika kinakwenda kutimia kama ifuatavyo
 
Mwingine akiwa na salio la 1M anaweza kukutukana kwa kupita karibu yake. Na kuna yule ana 500M na bado haoni kama amefika popote.
Yeah, tunatofautiana mkuu, hata bar kuna mtu anaweza kuwa na laki tu, lakini hizo kelele zake na matusi usiombe.

Na kuna yule jamaa akipata hela haonekani nyumbani hata wiki, yupo huko akifanya ufuska. Siku akikosa hela unamuona, anakuwa mpole kama anaumwa. Pesa kila mtu inambadirisha kwa namna yake.

huyo wa 500M kuna namna nae anabadirika, especially kama ndo mara yake ya kwanza kuishika hiyo hela, wengine hupenda kujifungia ndani.
 
Hata kama, sasa ndio atuambie anaogelea kwenye utajiri 🤣🤣🤣
 
Hata kama, sasa ndio atuambie anaogelea kwenye utajiri 🤣🤣🤣


Wewe endelea kusubiria hadi upate 100M ndio uanze kuwaza na kuishi kitajiri. ndege JOHN hana huo muda, anaenda na mambo kadri yanavyokuja huku akiendelea kutarajia makubwa zaidi.

Golf mchezo wa matajiri, sasa unawezapata picha Jamaa anawaza vitu gani kichwani. Watu anaowatamani maisha yao, vitu anavyotaka kumiliki, sehem anazotaka kutembelea, maisha anayoyatamani.

Vitu vizuri haviwezi kuja kama wewe mwenyewe ndani yako hauko tayari kuvipokea.
 
Million 5 nayo hela ?? Unajisifia rab pair 6 na iphone 17. Daaah Wahed Kweli 🤣🤣🤣

Kweli Tunatofautiana, Bado Sana Kijana Tena Mbali Sanaaa

Ni kiasi gani cha pesa au ni vitu gani ukivipata ndio inabadilika kutoka bado na kuwa tayari?

Mwenzetu hapo alipo anaogelea kwenye utajiri na anafurahia maisha.

Kuna mtu ana 1B hana amani na furaha aliyonayo mnyampaa.
 
Watu wote wakifanikiwa inabidi wawe kama huyu jamaa.

Siyo wale wengine ambao wanawaona wenzao hawana akili kisa wao wametoboa.
 
Una kumbukumbu kama mimi. Siku hizi dogo ana swaga kama za Mpwayungu Village. Kusifia mambo ya kipuuzi.
 
Ni kiasi gani cha pesa au ni vitu gani ukivipata ndio inabadilika kutoka bado na kuwa tayari?

Mwenzetu hapo alipo anaogelea kwenye utajiri na anafurahia maisha.

Kuna mtu ana 1B hana amani na furaha aliyonayo mnyampaa.

Blaza aache kusema ana hela, aseme anajimudu yeye maisha yake. Kuja kutambia watu Tsh 5 M, raba pair 6 na iphone 17 huo ji ushamba man 🤣🤣🤣

Zaidi inaonyesha dhiki aliyonayo na asili yake.

Yeye ange toa comment bana nlikua point A nimesogea point B namshukuru Mungu tunge mu appreciate na hata kumsanua mengine mazuri.

Tambo za kishamba kama hizo zinafunga milango mingi kuliko kufungua.

Kingine kuna stage unafika unaona ni vitu vya kawaida (exposure). Real people with real money hawapendagi kujulikana, wachache watanielewa.
 
Ni kweli maana hiyo 100 naweza nisiipate maisha yote. Kawaida ya binamu huwa hatujui kuridhika, ukipata milioni tano unatamani ungepata milioni 10 ila mwenzetu naona amejaaliwa roho ya kuridhika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…